Sunday, March 23, 2014

NEWZZZZZ: Jumba la wafu na wafungwa la Nigeria

Polisi wa Nigeria wanasema wamegundua miili kadha iliyooza, mafuvu na viungo vengine vya binaadamu katika jengo lilohamwa katika mji wa Ibadan, kusini magharibi mwa nchi.

Watu kadha wanaotapia mlo wamekutikana karibu na hapo, na vyombo vya habari vya Ibadan vimeripoti kuwa watu kama 15 wamekutikana wamefungwa minyororo kwenye uwa wa jengo hilo.

Polisi wamewakamata watu kadha, lakini washukiwa wakubwa bado hawakupatikana.
Maiti hao waligunduliwa baada ya madereva wa pikipiki za boda-boda kuripoti kuwa wenzao kadha wametoweka.

Chanzo: BBC Swahili

No comments: