Wednesday, March 26, 2014

MTOTO AFANYIWA MAUAJI YA KIKATILI USINGIZINI

MTOTO Hollo Dida (5), mkazi wa Kitongoji cha Igombwe, Kijiji cha Masweya, Kata ya Mtunduru, Tarafaya Sepuka, Wila yaya Ikungi, mkoani Singida, amekutwa amekufa akiwa amekatwa pua na kunyofolewa jicho lake la kulia.

Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, ACP Thobias Sedoyeka, alisema mtoto huyo alikuwa amelala na babu pamoja na bibi yake, tukio likihusishwa na imaniza kishirikina.
Alisema tukio hilo limetokea Machi 23 mwaka huu, saa mbili usiku katika kijiji hicho ambapo baada ya babu na bibi yake kuamka, walimwona mjukuu wao akiwa hana pua wala jicho.

"Polisi walipopata taarifa za tukio hili , walifika eneo la tukio na kufanya uchunguzi wa awali... walibaini mtoto huyo alikatwa pua na kitu chenye ncha kali na kuondolewa jicho lake la kulia.

"Babu wa mtoto huyu ni Lutonja Tambezi (60) na bibi yake Nyamizi Keja (55), woteni wakazi wa kijiji hiki ambao baada ya kuhojiwa na polisi, walisema walikuwa wamelala na mjukuu wao na walipoamka walishangaa kumwona amefariki dunia akiwa hana baadhi ya viungo vyake kama pua na jicho," alisema Kamanda Sedoyeka.

Kutokana na tukio hilo, jeshi hilo linawashikilia babu na bibi wa mtoto huyo kwa uchunguzi zaidi na ukikamilika watafikishwa mahakamani kujibu shtaka linalowakabili. Jeshi hilo limetoa wito kwa wananchi kuacha kujihusisha na mambo ya kishirikina ambayo yanachangia vitendo vya ukatili.

Chanzo: Majira

No comments: