Polisi watatu wanaolinda makazi ya
waziri mkuu wa Pakistan wamesimamishwa kazi kwa muda baada ya Paka kumuua Tausi
wa waziri mkuu.
Mtunza bustani alipata Tausi mmoja
amekufa katika moja ya bustani za makazi ambapo ndege hao huvinjari , lilieleza
gazeti la Express Tribune.
Mmoja wa maafisa waliosimamishwa kazi
amesema wengine 21 waliitwa kujieleza baadae. Imeripotiwa kuwa maafisa hao
walisema walikuwa kazini usiku ule , lakini hawakutegemea kuwa Paka wangemla
Tausi.
Maafisa 18 hawakubainika kuwa na
hatia, gazeti lilieleza.
Lakini watatu waliosalia wote
walipewa onyo na kuadhibiwa kwa uzembe
Makazi ya waziri mkuu wa Pakistani
Nawaz Sharif yako Raiwind, viungani mwa mji wa Lahore.
Chanzo: BBC

No comments:
Post a Comment