Mtandao wa kijamii wa , Twitter,
unafungwa nchini Uturuki , saa chache baada ya waziri mkuu , Recep Tayyip
Erdogan, kuahidi kuuondoa .
Bwana Erdogan -- ambaye anakabiliwa
na kashfa kubwa ya ufisadi aliwaambia maelfu ya wafuasi wake katika mkutano wa
uchaguzi kuwa hajali kuhusu namna jamii ya kimataifa itakavyochukulia hatua
yake .
Neelie Kroes, ambaye ni naibu rais wa
tume ya muungano wa Ulaya amesema umamuzi wa kufungwa kwa mtandao huo ni wa
kulaumiwa .
Serikali ya Bwana Erdogan imekuwa
ikilalamika kuwa mtandao wa Twitter ulipuuza uamuzi wa mahakama ulioitaka
viunganishi vya taarifa zake vinashukiwa kurekodi mawasiliano yake binafsi.
Chanzo: BBC Swahili


No comments:
Post a Comment