Oscar Pistorius azidiwa na hisia mahakamani
Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini
Oscar Pistorious atauza nyumba yake ili aweze kumudu gharama ya kesi ya mauaji
inayomkabili.
Hii ni kwa mujibu wa wakili wake
Brian Webber ambaye amenukuliwa na Shirika la Wanahabari La Afrika Kusini
(SAPA) akisema kesi hiyo itaendelea kwa zaidi ya wiki tatu zilizotarajiwa kwa
kesi hiyo kukamilika.
Oscar hajaweza kurejea katika nyumba
yake hata baada ya maafisa wa uslama kumruhusu arejee huko zaidi ya mwaka mmoja
uliopita huku uamuzi ukitolewa wa nyumba ile kusalia ikiwa imefungwa hadi pale
kesi hiyo itakapo kamilka.
Kwa Mujibu wa SAPA, hati za kortini
zilizoandikishwa mwaka jana wakati mwanariadha huyo alipokuwa akiwasilisha ombi
la kuachiliwa kwa dhamana zaonyesha kuwa nyumba hiyo iliyo katika mtaa wa
Silverwoods ina thamani ya Randi millioni 5 ambazo ni sawia na dola za marekani
457 000.
Oscar anakanusha madai ya kumuua
mpenzi wake mnamo tarehe 14 mwezi wa Februari mwaka jana huku akisema kuwa
alimpiga risasi kimakosa.
Kesi ya mauaji dhidi yake ambayo kwa
sasa iko katika wiki ya tatu, imehairishwa hadi siku ya jumatatu ambapo
mashahidi wengine watano wa upande wa mashitaka wanatarajiwa kutoa ushahidi wao
kabla ya yeye kupewa fursa ya kujitetea.
Upande wa mashitaka unadai kuwa
Pistorious alimpiga risasi Bi Steenkamp, aliyekuwa mwana mitindo, mtangazaji
maarufu wa runinga na mwana sheria baada ya kinachodahniwa kuwa ugomvi wa
nyumbani.
Huku kwa upande wake, Pistorious
akisema kuwa aliamini kuwa mpenzi wake alikuwa amelala na akidhani kuwa
palikuwa na mwizi nyumbani kwake alifyatua risasi kuelekea chooni asubuhi
mapema mnamo tarehe 14 februari mwaka 2013.
Iwapo mwanariadha huyu mwenye umri wa
miaka 27 atapatikana na hatia , huenda akakabiliwa na kifungo cha maisha.
Chanzo: BBC


No comments:
Post a Comment