Asema mwanamke atakayevaa hereni za meno
ya tembo kukamatwa
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro
Nyalandu, amesema kuanzia sasa mwanamke yeyote atakayekutwaa amevalia urembo
uliotengenezwa kwa nakshi na malighafi ya meno ya tembo atakamatwa na
kuchukuliwa hatua za kisheria.
Nyalandu aliyasema hayo jana wakati
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mara baada ya kusaini makubaliano na Taasisi ya Kimataifa
ya Uhifadhi kutoka Marekani (ICCF), kwa ajili ya kuimarisha ulinzi pamoja na kuweka
ushirikiano katika sekta ya wanyama hasa kuzuia ujangili unaoendelea kwa
sasa nchini.
Waziri Nyalandu alisisitiza kuwa mtu
yeyote atakayekutwa na mapambo yanayotokana na nyara hizo hata akiwa kigogo
amevalia hereni au shanga, atakamatwa na hatua za kisheria dhidi yake
zitachukuliwa ikiwa ni sehemu ya harakati za kutokomeza ujangili nchini.
Chanzo: Tanzania Daima

No comments:
Post a Comment