Monday, March 31, 2014

AZAMU FC NJIA NYEUPE

WANALAMBALAMBA Azam FC jana walizidi kudhihirisha kuwa wabishi na kuzidi kujikita kileleni baada ya kuilaza Simba kwa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Wakati Azam FC ikizidi kubaki njia kuu na kulinda rekodi ya kutopoteza mchezo hata mmoja tangu ligi hiyo kuanza msimu huu, mabingwa watetezi Yanga, walichepukia Tanga na kujikuta wakishindwa kulimudu gwaride la Mgambo JKT kwa kukubali kichapo cha mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Mkwakwani katika pambano lililotawaliwa na imani za kishirikina.

Katika Dimba la Taifa, kila timu ilianza kwa kasi na kushambuliana kwa zamu, ambapo dakika ya nane, Azam walilifikia lango la Simba na kumlazimisha kipa Ivo Mapunda kufanya kazi ya ziada kutokea na kumzuia Kipre Tchetche asifunge.

Simba walijibu mashambulizi dakika ya 12, kwa winga wake Ramadhani Singano ‘Messi’ kupiga shuti kali la mbali nje ya boksi na kudakwa na mlinda mlango, Aishi Manula.

Kutokana na kosa kosa hiyo, ndipo ilipobainika kuwa mashabiki wa Yanga walikuwa wakiishangilia Simba, tukio lililojibiwa kwa kuzomewa na mashabiki wa Simba.

Dakika ya 14, Mapunda kwa mara nyingine alifanya kazi ya ziada kupaa juu na kuokoa shuti la Khamisi Mcha ‘Vialli’ lililotokana na adhabu ndogo ‘free kick’.

Baada ya kosa kosa hiyo, Mcha alisawazisha makosa kwa kuifungia Azam bao dakika ya 17 kwa shuti jepesi ndani ya boksi, hivyo kuibua mgawanyiko miongoni mwa mashabiki wa Simba, ambao nusu walilishangilia.

Mashabiki hao walilishangilia kama ishara ya kushangilia anguko la Yanga, ambayo mashabiki wake walikuwa wakiishangilia Simba ili iifunge Azam na kuwajengea mazingira ya kutetea taji la Ligi Kuu.

Dakika ya 22, Singano alikosa bao la kuisawazishia Simba kwa shuti lake kupaa sentimita chache juu ya lango, kabla ya Amisi Tambwe naye kushindwa kufunga kwa kichwa, akiunganisha krosi ya Singano dakika ya 30.

Mcha, dakika 10 kabla ya filimbi ya mapumziko, aliikosesha Azam bao jingine, akishindwa kumalizia kazi maridadi ya Kipre.

Wakati mashabiki wakiamini mpira utaingia mapumziko Azam wakiwa mbele kwa bao 1-0, beki Joseph Owino aliisawazishia timu yake kwa kichwa dakika ya 45, akiitendea haki krosi ya Chanongo ambaye alikuwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya Wanalambalamba.

Kipindi cah pili nacho kilianza kwa mashambulizi, kwa kila upande kusaka bao la ushindi, hivyo kushuhudiwa kosakosa kadhaa.

Kipindi cha pili, Azam waliingia kwa nguvu na dakika ya 57, walipata bao la pili lililofungwa na John Bocco ‘Adebayor’ kwa kichwa, akiunganisha mpira wa ‘tik tak’ ya Kipre iliyogonga mwamba na kurudi uwanjani.

Baada ya kufunga bao hilo, Azam ilionekana kupunguza kasi, hasa baada ya kutolewa Kipre ambaye alikuwa msumbufu katika safu ya ulinzi ya Simba.

Simba ikiwatumia vijana wake Chanongo, Mkude, Singano na wakongwe Uhuru na Tambwe, waliendelea kushambulia bila mafanikio.

Jitihada za Simba kusaka bao la kusawazisha nusura zizae matunda dakika ya 64, pale Tambwe alipokosa bao la kichwa akiwa na nyavu, kuunganisha krosi ya Chanongo.

Hadi mwamuzi Israel Nkongo akihitimisha dakika 90, Azam walitoka kidedea kwa mabao 2-1.

Kwa ushindi huo, Azam FC imefikisha pointi 53 na kuzidi kuitimulia vumbi Yanga iliyosalia na pointi 46.

Azam FC: Aishi Manula, Erasto Nyoni, Michael Gadiel, Aggrey Morris, David Mwantika, Kipre Balou, Himid Mao/ Bryson Rafael, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’, Kipre Tchetche/ Bryan Umony, John Bocco na Khamis Mcha ‘Vialli’/Kelvin Friday.

Simba: Ivo Mapunda, William Lucian, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Joseph Owino, Donald Musoti, Jonas Mkunde, Haruna Chanongo/Awadh Juma, Henry Joseph/Abdulhalim Humud, Amisi Tambwe, Uhuru Suleiman na Ramadhani Singano ‘Messi’/Badru Ally.

Jijini Tanga, Mgambo walianza kujipatia bao dakika ya kwanza, likifungwa na Fully Maganga.

Dakika ya 30, Mohamed Neto alilimwa kadi nyekundu na mwamuzi aliyejulikana kwa jina la Mahadhi, kwa madai ya kukutwa na kinachodaiwa kuwa ni ‘hirizi’ ndani ya nyeti zake. Hadi dakika 45, bao lilikuwa hilo moja.

Kupungua kwa Mgambo, kuliwaongezea nguvu Yanga ambao walizidi kuliandama lango la wapinzani wao na kufanikiwa kupata penalti dakika ya 52 baada ya beki mmoja kuunawa mpira eneo la hatari. Penalti hiyo ilifungwa na Nadir Haroub ‘Canavaro’. Matokeo yaliyodumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili, licha ya Mgambo kuwa pungufu, ilicheza mchezo wa kujihami na kushambulia kwa kushtukiza na dakika ya 64 Kelvin Yondani aliunawa mpira eneo la hatari na kuamriwa penalti iliyofungwa na Malimi Busungu.

Huko Mbeya, Tanzania Prisons ilizidi kukalia kuti kavu baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 kwa Mbeya City, likifungwa na Paulo Nonga, dakika ya pili.

Huko Kaitaba Kagera, maafande wa Ruvu Shooting walilazimisha sare ya bila kufungana na wenyeji Kagera Sugar.

Chanzo: Tanzania Daima

Warioba amshukia Prof Shivji

Dar es Salaam. Mjadala wa Mabadiliko ya Katiba jana ulihamia nje ya Bunge wakati Jaji Joseph Warioba alipomchambua mhadhiri maarufu nchini, Profesa Issa Shivji akimueleza kuwa si mkweli bali mpotoshaji wa Rasimu ya Katiba.

Jaji Warioba, ambaye ni mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, pia amemtuhumu Profesa Shivji kuwa ndiye mwanzilishi wa chokochoko za Zanzibar za kudai serikali tatu, jambo ambalo sasa analigeuka kutokana na kuona hali imekuwa mbaya.

Kauli ya Warioba imekuja baada ya Profesa Shivji kuichambua Rasimu ya Katiba jana asubuhi kwenye Kongamano la Vijana lililoandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo lililokuwa na dhima ya Vijana Katika Kuimarisha na Kuendeleza Muungano Baada ya Miaka 50. Tamasha hilo lilifanyika kwenye hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Plaza jijini Dar es salaam.

Akiwasilisha mada kwenye kongamano hilo, Profesa Shivji alisema katika kujadili Muungano, wananchi hawana budi kuzingatia mambo mawili ambayo ni nchi zinazozungumziwa kwenye Rasimu kuwa ni Zanzibar, Tanganyika au Tanzania, ambayo alisema haina mamlaka katika pande hizo mbili za Muungano.

Pia alisema suala la maadili kwa viongozi halina budi kuangalia kuwa linazungumzia maadili ya viongozi wa Zanzibar, Tanganyika au Tanzania na kwamba rasimu inazungumzia viongozi wa Tanzania ambao hawana mamlaka kwa Tanganyika na Zanzibar.

Katika majumuisho yake, Profesa Shivji, ambaye aliikosoa Rasimu kuwa haiwakilishi matakwa ya Watanzania kwa kuangalia sampuli zilizotumika, alisema kwamba wajumbe wa Tume ya Jaji Warioba walikuwa na nia njema.

Lakini Shivji akaenda mbali zaidi kwa kusema “the road to hell is paved in good intention,” akimaanisha kuwa njia ya kuzimu imetengenezwa kwa nia njema.

Akijibu hoja hizo, Jaji Warioba alisema Profesa Shivji amegeuka maandishi yake yaliyokuwa yanachochea utaifa wa Zanzibar na sasa anaona Tanganyika ndiyo hatari kwa Muungano.

“Shivji ni msomi na mimi najua anaelewa matumizi ya takwimu,” alisema Jaji Warioba, ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wakati alipozungumza na gazeti hili nyumbani kwake jana jioni.

“Nasema hapa, Shivji akiwa msomi, amekuwa intellectually dishonest (si mkweli kiusomi). Anapotosha kwa makusudi.”

Jaji warioba alisema Shivji ndiye amekuwa chanzo cha uchochezi wa kitaifa Zanzibar kupitia maandishi yake. Alisema waliokuwa wanadai serikali tatu kwa muda mrefu walikuwa wananchi wa Zanzibar.

“Shivji alikuwa anasema Tanganyika imejificha kwenye Muungano ili inufaike. Kwa hiyo anasema Tanganyika iwe wazi isijifiche,” alisema Jaji Warioba.

“Na Shivji amechochea hilo… wote wale waliokuwa wanamnukuu walikuwa wanatoa hayo kwenye maandishi yake na kwamba mpaka leo hii kuna watu wa Zanzibar wanaamini Muungano huu si halali kisheria kutokana na Shivji ambaye alisema Baraza la Mapinduzi halikuridhia articles (ibara) za Muungano.”

Alipoulizwa jana usiku kuhusu tuhuma hizo za uchochezi na chanzo cha hisia za utaifa wa Uzanzibari na Utanganyika, Profesa Shivji alisema hawezi kujibu tuhuma hizo kwa kuwa hajamsikia Jaji Warioba akizungumzia hilo.

“Hey, amezungumza lini?” alihoji. “Siwezi kujibu kwa kuwa sijamsikiliza mwenyewe.”

Lakini Jaji Warioba alisema watu walitumia msingi huo kudai utaifa wa Zanzibar na kusisitiza kuwa Shivji amesababisha hisia za utaifa na kwamba haya yanayoendelea sasa yanatokana uchochezi huo.

“Hata kabla ya sisi kuanza mchakato huu, Shivji alikwenda Zanzibar akazungumza na Baraza la Wawakilishi na akawaambia issue kwa Zanzibar ni self determination (kujitambua), Sasa leo anaona kama hatari ni Tanganyika, lakini yeye ndio amechochea nationalism (utaifa),” alisema Jaji Warioba.

Kuhusu takwimu, Jaji Warioba alisema mara ya kwanza Profesa Shivji alizungumzia takwimu za Zanzibar kuhusu muundo wa Muungano akisema kuwa waliozungumzia suala hilo walikuwa 47,000, huku watu 27,000 wakitoka Tanzania Bara na 19,000 kutoka Zanzibar.

 “Safari hii ametaja zile za Tanzania Bara na kusema hiyo ni figure (namba) ndogo sana ukilinganisha na watu 300,000 waliotoa maoni,” alisema Warioba.

Alisema Tume ilitumia takwimu zinatokana na watu waliozungumzia suala ambalo wameliwekea asilimia na si kwa ujumla na ndio maana anaona Profesa Shivji anataka kupotosha kwa makusudi.

Warioba alimuelezea Profesa Shivji kuwa sasa ameamua kueneza propaganda za serikali mbili kwa kuponda Rasimu ya Katiba ambayo inaonyesha kuwa muundo wa serikali tatu ndio unaoifaa Tanzani kwa sasa.

Aidha, Warioba alisema msimamo wa Profesa Shivji ni kwamba Zanzibar haikukosea kubadilisha Katiba mwaka 2010.

“ Nimeshangazwa na Shivji kusema kwamba kitendo cha Zanzibar kubadili Katiba yao kuwa ‘Zanzibar ni Nchi’ halikuwa jambo la ajabu,” alisema Warioba.

Alisema Shivji ni msomi ambaye anafahamu kitendo cha kubadilisha Katiba kilikuwa na madhara makubwa katika muundo wa Muungano.

“Nadhani mnakumbuka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipoulizwa Bungeni kama Zanzibar ni nchi au siyo nchi, alijibu kuwa Zanzibar siyo nchi, vurugu zake mnakumbuka,” alisema.

Alisema lakini msomi kama Shivji haoni kama suala hilo la ‘Zanzibar ni nchi’ lina madhara makubwa katika mstakabali wa taifa letu.

Jaji Warioba alisema kama serikali tatu hazitakiwi, basi kinachotakiwa kufanywa ni kwa Zanzibar kubadili Katiba yake ili iseme kwamba Zanzibar ni sehemu ya Muungano, vinginevyo haiwezekani.

“Maana kama ni kusahihisha, ni lazima kwanza Katiba ya Zanzibar itumie maneno yale yale yaliyo kwenye Katiba ya Muungano. Yaani Zanzibar iwe sehemu ya nchi. Zanzibar wakubali hilo,” alisema.

“Zanzibar wakubali Rais wa Muungano ana madaraka nchi nzima maana mabadiliko ya 2010 yamemuondolea Rais wa Jamhuri ya Muungano madaraka yake.”

Akitoa mfano wa mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, Jaji Warioba alisema amekuwa akidai takwimu hazionyeshi uhalisia wa maoni ya wananchi.

“Kwa mfano, Jimbo la Simanjiro linakuwa na watu 100,000 lakini waliojiandikisha kupiga kura ni watu 20,000 na waliopiga kura ni watu 15,000. Hii ina maana ushindi wake utakuwa katika watu waliopiga kura na siyo idadi ya watu wa Simanjiro,” alisema Warioba.
Chanzo: Mwananchi


WALIMU NA MITIHANI MIGUMU KATIKA ELIMU

                            Photo from: Mpagaze

Mahabusu 21 wauawa Nigeria

Polisi Nigeria wamesema wafungwa 21 waliuawa
Wafungwa 21 waliuawa walipojaribu kutoroka kutoka kwenye makao makuu ya Kitengo cha Jinai cha jeshi la polisi la Nigeria lililoko Abuja.
Hadi kufikia sasa haijabainika iwapo waliokufa wote ni wafungwa au la .
Msemaji wa kitengo hicho cha jinai Marilyn Ogar , amesema maafisa wawili wa kitengo hicho walijeruhiwa vibaya ,mahabusu walipowavamia kwa pingu zao.

Watu walioshuhudia wanasema milio ya risasi ilisikika karibu na kasri la rais punde baada ya jeshi la taifa kuingilia kati kuzima jaribio hilo la kutoroka kwa mahabusu.

Vyombo vya habari nchini humo vimesema kuwa gereza hilo linakisiwa kuwa limehifadhi wapiganaji wa kundi lililopigwa marufuku, la Boko Haram. Chanzo: BBC

Hakuna mwafaka kati ya Marekani ,Urusi.

John Kerry akutana na Serguei Lavrov kuhusiana na taharuki kuhusu Ukraine

Waziri wa mashauri ya Nchi za kigeni wa Marekani John Kerry, amesema kuwa hakuna makubaliano yaliyoafikiwa baina yake na mwenzake kutoka Urusi Sergei Lavrov, katika mkutano wa
dharurakuhusu mzozo wa Ukraine.

Marekani inasisitiza kuwa hatua ya urusi kutwaa eneo la Crimea baada ya kura ya maoni sihalali.
Bwana Lavrov ametoa masharti makali yasiyoegemea upande wowote huku akitaka uhuru wa Ukraine kama taifa utambuliwe.

Waziri wa Urusi amesema kuwa ni jukumu la Kiev kuandaa katiba mpya ili kuwezesha hilo lifanyike, mbali na kulinda maisha ya waukraine wachache wanaozungumza kirusi dhidi ya uvamizi kutoka kwa
waukraine wanaounga mkono kujiunga na jumuiya ya Ulaya.
Marekani imetaka hatua ya kuongeza wanajeshi zaidi wa Urusi katika mpaka mashariki ya Ukraine kukomeshwa mara moja.

Mazungumzo ya Paris siku ya ijumaa yalifuatwa na mazungumzo ya simu kati ya Rais Vladimir Putin wa Urusi na Rais Obama wakati aliposimama kwa muda akiwa njiani kuelekea Washington siku ya
Jumamosi, Bwana Kerry alibadilisha mkondo na kuelekea Paris.
Ukraine inasisitiza kuwa Urusi ina njama ya kuigawanya Ukraine na kulisambaratisha kama taifa.

Waandishi wanasema kuwa Maafisa wa Marekani wamegawanyika iwapo mazungumzo hayo yaliyopangwa yametokana na nia halisi ya Urusi ya kujaribu kupunguza taharuki iliyopo au ni mipango ya
hatua zaidi ya kijeshi.


Pentagon inaamini kuwa maelfu ya wanajeshi wa Urusi wamekita kambi karibu na mpaka na Ukraine kwa niya ya kuwatishia viongozi wa Ukraine .
Chanzo: BBC

INTERNATIONAL POLITICS: Erdogan: poll win a blow to immoral politics

Turkish prime minister claims victory in local elections, saying results are a rejection of "aimless, immoral" rivals.

Turkey's prime minister has has declared victory in local elections that had become a referendum on his rule, calling the results a blow to the "immoral, aimless politics" of his rivals.

Recep Tayyip Erdogan warned his rivals would "pay the price" for their loss as preliminary results on Sunday showed his Justice and Development party, known as the AKP, took up to 47 percent of all votes cast.

The main opposition Republican People's Party, known as the CHP, had 28 percent and the Nationalist Movement Party, or MHP, had 13 percent, the Anatolia news agency reported late on Sunday.

The elections, which were being held amid corruption allegations and damaging security leaks that have shaken the 12-year rule of the AKP government, were widely seen as a vote of confidence for the rule of Erdogan.

At a rally in Ankara in the early hours of Monday, Erdogan said that "democracy and free will" had won.

"These poll results show more than who won, it shows how lost," he said. "Immoral politics have lost. Politics on tapes, on false recordings have lost. Immoral and aimless politics have lost."

He took aim at rivals who sought to capitalise on the leaked recording in their campaign against him, and the press.

"I ask the leader of the opposition if he didn't have the recordings, what would you have said on your campaign? You only utter lies and false statements."

He gave warning that his foes would "pay the price". "From tomorrow, there may be some who flee," he said.

Hectic campaigning

More than 50 million voters were eligible to cast their ballots in Turkey's local elections.

The AKP, which swept to power in 2002 on a platform of eradicating the corruption that blights Turkish life, hopes on Sunday to equal or better its overall 2009 vote of 38.8 percent.

Erdogan crisscrossed the nation of 77 million during weeks of hectic campaigning to rally his conservative core voters, during which he temporarily lost his voice.

His government has purged thousands of people from the judiciary and police since December following the anti-corruption raids targeting businessmen close to Erdogan and sons of ministers.

The prime minister said that those behind the investigations were trying to form a "state within a state" or "parallel state", blaming the movement of Fethullah Gulen, the US-based Turkish cleric whose followers are apparently highly influential in Turkey's police forces and judiciary.

Many analysts say that the two sides used to be allies in the past in their struggle against Turkey's politically dominant military.

The CHP portrays Erdogan as a corrupt "dictator" ready to hang on to power by any means. Capture of the capital Ankara or Istanbul would allow them to claim some form of victory, although no result has been declared in either city.

Source: Al-jazeera

Sunday, March 30, 2014

MICHEZO: YANGA SC HATARINI KUKOSA MWANA NA MAJI YA MOTO, MBEYA CITY WAWANIA NAFASI YAO

Na Prince Akbar, Dar es Salaam
YANGA SC sasa wapo hatarini kukosa mwana na maji ya moto- hiyo inafuatia Mbeya City kuilaza Prisons bao 1-0 jioni ya leo Uwanja wa Sokoine, Mbeya na kurejea rasmi kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Bao pekee la Mbeya City leo limefungwa na Paul Nonga dakika ya kwanza tu ya mchezo na sasa timu hiyo ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya inatimiza pointi 45 baada ya kucheza mechi 23.

Yanga SC baada ya kufungwa na Mgambo JKT mabao 2-1 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga leo inabaki na pointi zake 46 za mechi 22, wakati Azam FC ipo kileleni kwa pointi 53 za mechi 23 baada ya kuifunga Simba SC mabao 2-1 leo.

Ikiwa sasa inaizidi pointi moja tu Mbeya City, Yanga SC inarejea Dar es Salaam kucheza na JKT Ruvu na baadaye Kagera Sugar kabla ya kucheza na JKT Oljoro na Simba SC.

Matokeo mengine ya leo, Kagera Sugar imelazimishwa sare ya bila kufungana na Ruvu Shooting, Mtibwa Sugar imeifunga mabao 3-1 Coastal Union na JKT Ruvu imeichapa 3-1 Rhino Rangers.

 Chanzo: Bin Zubery

SAFARI YANGU YA MATESO TUNDURU-SONGEA NA Chiwambo's Blog


Hii Ndio Barabara ya Mtwara Korido maarufu kwa jina la Tunduru-Songea
MAOMBI YA WANATUNDURU NI KUONDOKANA NA HII KERO
                          Miongoni mwa hao ni Mwenyekiti wa Chiwambo's Blog Ndugu Ausi Chiwambo.
 Picha Hii ni Barabara ya Tunduru Songea Mbele ya kijiji cha Namwinyu huko Wilayani Tunduru.
               Safari Wakati wa mvua zinakuwa hivi kama muonavyo kwenye hiyo TDI Defenda. Hapa ilikuwa baada ya kuharibikiwa na gari.
 Picha juu ni Stendi ya Namtumbo tayari kwa kuanza safari ya Tunduru
Baada ya Kuharibikiwa na Gari. Ausi Chiwambo ni Mwenye Shati jeupe na kachuchumaa chini kuonyesha hali imekuwa Mbaya


Ndivyo ilivyo barabara ya Tunduru-Songea, Kodi za wananchi zna kwenda wapi, makaa ya mawe Mbinga, uranium Namtumbo, madini aina nyingi 2nduru, gesi Mtwara, mazao ya chakula na biashara asilimia kubwa huzalishwa kusini, Nini hatima ya Mtwara coridal? Tunduru,Masasi na Mbambabay wataijua lami lini? 

Serikali inamtazamo gani kutanua majiji sehemu nyingine? Kwanini kung'ang'ania kuhamishia malighafi Dar badala ya kujenga viwanda pale malighali yalipo? Serikali isaidie watu kupata ajira kutokana na malighafi zilizo kwenye mazingira yao na co kuhamisha, wananchi hunyanyasika kwa maamuzi yasiyo ya ridhaa yao.

UKWELI BARABARA YA TUNDURU-SONGEA NI HATARI KWA USALAMA WA ABIRIA.  KULALA NJIANI NI JAMBO LA KAWAIDA NYAKATI ZA MVUA KALI. Picha na Ausi Chiwambo-Tunduru

KATUNI YA LEO


SIASA TZ: CCM wazidi kulia na Warioba

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimezidi kuilaumu iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa kuandika rasimu iliyojaa mawazo ya wajumbe wake waliotaka muundo wa serikali tatu.

Lawama hizo zilitolewa jana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo uliandaliwa kwa lengo la kumpongeza Rais Jakaya Kikwete, kwa hotuba aliyoitoa bungeni Machi 21, ambapo Kinana alisema tume hiyo iliyokuwa chini ya kada wao Jaji Joseph Warioba, haikueleza ni makundi mangapi yalitaka serikali tatu.

Kinana alisema Tume ya Mabadiliko ya Katiba walisubiri Mwalimu Julius Nyerere afe ndipo waseme serikali tatu, kwani walikuwepo enzi hizo.

“Muungwana angesema nani kasema nini wakati wa kuchukua maoni, tume haijasema katika mabaraza 171 ni mangapi yalitaka serikali tatu, ukiwauliza mara makaratasi yamepotea, hatukumbuki.

“Tusitoane meno na macho kwa ajili ya Katiba, kwani ikishatengenezwa itawekwa kabatini na viongozi wataendelea kula kuku, umaskini upo palepale, ufisadi upo palepale, alichokisema Rais Jakaya Kikwete ni tahadhari tu, yapo maisha baada ya Katiba,” alisema.

Kinana alibainisha kuwa wamepata taarifa kuwa baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu kutoka upinzani wamedhamiria kuvuruga vikao vya Bunge ili Katiba mpya isipatikane.

Alisema wajumbe hao wanafanya hivyo baada ya kuona hawawezi kuingiza matakwa yao, kwakuwa wingi wa wajumbe wa CCM unawatisha.

Katika hatua nyingine, Kinana alisema kuwa ziara yake ya siku nne jijini Dar es Salaam ya kukagua miradi imeonyesha namna CCM ilivyopiga hatua katika utekelezaji wa ilani.

Alisema kuhusiana na suala la maji alitembelea Ruvu Chini na Juu na kubaini kuwa ifikapo mwaka 2015 asilimia 72 ya wakazi wa Dar es Salaam watapata maji ingawa Wizara ya Maji inakabiliwa na uhaba wa fedha.

Akizungumzia masuala ya umeme, Kinana alisema anayetaka umeme wa bei nafuu ahamie kijijini, kwani gharama za umeme mijini na vijijini ni tofauti.

Kuhusu mji mpya wa Kigamboni, alisema kuwa watalizungumza suala hilo ili kulipatia ufumbuzi.

“Hatujawahi kuona mji mpya unajengwa kwa kuhamisha watu, kama serikali imeamua mbona hawakuuliza wananchi?” alihoji.

Alisema kuwa matatizo ya walimu yataendelea kutatuliwa ikiwemo serikali kuendelea kujenga nyumba za walimu na kuwapunguzia makali ya ugumu wa maisha.

Kawa upande wa tatizo la ajira, aliitaka serikali kutafuta mbinu zisizo za kawaida za kutengeneza ajira nyingi zaidi ili watu wengi waajiriwe, hasa watu wa chini kwa kutengeneza viwanda vingi.

“Watu wanaojiajiri wapewe nafasi, si mgambo kuwasumbua na kuwadai kodi zisizo na msingi, kodi ndogondogo zinasumbua watu na kupoteza muda,” alisema.

Kuhusiana na tatizo la wizi wa dawa hospitalini, Kinana alisema kuwa serikali imepata suluhisho ambapo dawa zote zitaandikwa Serikali ya Tanzania.

Kinana alisema ifike mahali matatizo yanayoikabili nchi yatatuliwe, kwani wao kazi yao ni kuisimamia serikali na kuwajibishana pale panapokosewa.

Naye Mbunge wa Ilala, Idd Zungu, alisema Bunge halikutunga sheria kandamizi kwa bodaboda na wafanyabiashara bali Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini  (Sumatra) ndio waliotunga kanuni kandamizi.

Chanzo: Tanzania Daima

Wanane wauawa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Vikosi vya Umoja wa Afrika nchini Jamhuri ya afrika ya kati vinasema kuwa watu wanane wameuawa na vikosi vya Chad katika mji mkuu wa Bangi.
Vyombo vya habari hatahivyo vimeiweka idadi hiyo kuwa juu zaidi.
Vikosi hivyo ambavyo vilikuwa vimewasili mjini humo ili kuwatorosha raia wa Chad wanaoishi nchini humo vinadaiwa kuwafyatulia risasi wakaazi wanaoishi katika maeneo ya wakristo ya mji wa Bangi.

Chad imeshtumiwa kwa kuwaunga mkono waasi wa kiislamu wa seleka ambao mwaka uliopita waliipindua serikali.
Taifa hilo la Jamhuri ya afrika ya kati limekumbwa na ghasia za kidini tangu kupinduliwa kwa rais Franswa Bozize.

Chanzo: BBC Swahili

Wamisri wanaomtusi El-Sisi waonywa

Wizara ya mambo ya ndani ya nchi ya Misri imesema kuwa inachunguza maneno yanayoandikwa kwenye mitandao ya kijamii yakiwa na kitambulisho, yaani "hashtag", yanayomtusi waziri wa ulinzi aliyestaafu ili kugombea urais, Field Marshall Abd-el-Fattah el-Sisi.

Heshtegi hiyo ambayo tafsiri yake ni "mpigie kura kuwadi", imesambazwa kwenye Twitter zaidi ya mara 100-milioni na imependwa na watu zaidi ya 40,000 kwenye Facebook.
Inaarifiwa kuwa wizara ya mambo ya ndani ya Misri imesema itawakamata watu wanaoitumia sana heshtegi hiyo.

Maneno hayo piya yamekuwa yakichorwa kwenye kuta za mjini Cairo chini ya mabiramu ya picha za Bwana Sisi.
Field Marshall E-Sisi aliipindua serikali iliyochaguliwa kwa njia za kidemokrasi ya Mohamed Morsi wa Muslim Brotherhood mwezi Julai mwaka jana.

Chanzo: BBC Swahili

Wajumbe wa Bunge Maalum wasusia Bunge

Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Esther Bulaya ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) akipiga kura ya siri juzi wakati Bunge hilo lilipokuwa likipitisha utaratibu wa kupiga kura za aina mbili ya siri na wazi. Picha na Salim Shao 
Dodoma/Dar. Wakati Bunge Maalumu la Katiba linatarajia kuanza kujadili Rasimu ya Katiba kesho, baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo wameanza kuondoka bungeni, kupinga mwenendo wa Bunge hilo.

Hatua hiyo ya wabunge hao inakuja wakati Bunge Maalumu la Katiba juzi lilipitisha azimio la kutumia kura ya siri na wazi katika kuamua vifungu vya rasimu.

Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samia Saluhu alisema baada ya kupitishwa kwa utaratibu wa kupiga kura za siri na wazi katika Bunge hilo, kuanzia Jumatatu wataanza kujadili sura ya kwanza na sita ambayo inahusu Muundo wa Muungano.

Katika sura ya kwanza, mambo ambayo yanatakiwa kujadiliwa ni Jina, Mipaka, Alama, Lugha na Tunu za Taifa wakati sura ya sita mambo ambayo yanapaswa kujadiliwa ni Muundo wa Muungano.

Lema atangaza kurudi jimboni Arusha

Mjumbe wa Bunge hilo, Godbless Lema alisema anakusudia kuondoka bungeni, kutokana na kutoridhishwa na maridhiano ya kupiga kura za siri na wazi katika kufikia uamuzi katika Bunge hilo.

Akizungumza na Mwananchi jana, Lema alisema hakubaliani na utaratibu uliopitishwa, kwani unalenga kulazimisha kila jambo ambalo chama tawala kinalitaka lipitishwe.

“Huu utaratibu wa kura kupigwa kwa wazi na siri katika kitu kimoja, haupo sehemu yoyote duniani. Sasa sisi kukubali ni kuwasaliti wananchi, kwani hata Dodoma tunaandaa rasimu ya Katiba ya wananchi wote siyo ya CCM pekee,” alisema Lema.

Alisema pia hakubaliani na utaratibu wa kujadili rasimu ya Katiba, ambao umetolewa na Kamati ya Uongozi kwa kuanza na sura ya kwanza na ya sita, kwani vinalenga kufumua Rasimu ya Jaji Warioba.

“Hapa CCM wanataka kulazimisha Serikali mbili kwa kujadili kwanza vifungu hivi, kama vitapita basi watakuwa na uwezo wa kubadili rasimu yote kitu ambacho mimi siwezi kukaa kwenye Bunge hili na kusaliti wananchi waliotoa maoni kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba,” alisema Lema.

Jussa atabiri Bunge kuvunjika.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mjimkongwe, Ismail Jussa, alisema uchaguzi wa vifungu hivyo ambavyo ndivyo vinabeba Rasimu ya Katiba, vinaashiria kuvunjika kwa Bunge hilo katika hatua za awali.

“CCM msimamo wao ni Serikali mbili na sisi ni Serikali tatu na tunaanza kujadili vipengele vinavyobeba Katiba na hakuna atakayekubali kuachia msimamo wake na hapo ndipo Bunge litakapovunjika,” alisema.

Kuhusu utaratibu wa kupiga kura za wazi na siri, Jussa alisema utaratibu huo utaleta mgawanyiko mkubwa, kwa sababu ya msimamo wa CCM ni kura za wazi na hivyo hakuna mjumbe wa chama hicho atakayethubutu kupiga kura ya siri.

Mnyika

Naye mjumbe mwengine wa Bunge hilo, John Mnyika, alisema, CCM ina mpango wa kubadili rasimu kutoka Muungano wa Serikali tatu kuwa wa Serikali mbili ili kufanikisha msimamo wao na maelekezo ya Rais kwenye hotuba yake bungeni.

Mnyika alieleza kuwa kwa mazingira hayo, Ukawa unahitajika kutetea maoni ya wananchi na kwamba CCM wakiendelea na njama zao wakati wa kujadili sura ya kwanza na ya sita, itawalazimu kurudi kwa wananchi ambao ndiyo wenye nchi.

“Hatua ya kurejea kwa wananchi inatarajiwa kuchukuliwa kabla ya kuendelea na sura zingine mbili za Rasimu ya Pili ya Katiba,” alisema Mnyika.

Mnyika alisema mpango huu ulianza kwa wajumbe wa Bunge Maalumu kutoka CCM wakati wa kujadili rasimu ya kanuni waliwasilisha majedwali ya marekebisho kutaka ibara zipangwe mbili mbili zinazofanana.

Katibu wa Bunge

Hata hivyo, Katibu wa Bunge Yahya Khamis Hamad akizungumzia kuondoka kwa baadhi ya wabunge alisema, suala hilo amelipata jana kupitia Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge lakini si msimamo wa kundi.

“Taarifa hii tulipata kwenye kamati, lakini tukaulizana kama kuna kundi linataka kuondoka, ikabainika hakuna kundi.”

Kuhusu uamuzi wa kuanza kujadili sura ya rasimu ya kwanza na sita alisema tayari yalifikiwa na Kamati ya Uongozi na kwamba kwa mujibu wa kanuni ya 58 kifungu kidogo cha tatu, Kamati ya Uongozi ndiyo yenye jukumu la kupanga utaratibu wa kujadiliwa rasimu.

Kuhusu CCM kuwa na rasimu yake

Akizungumzia taarifa kuwa CCM ina rasimu yake ambayo ndiyo wanataka ijadiliwe alisema hakuna suala hilo.

“Mimi binafsi sijalisikia hilo na sitegemei kuwapo, kwani wajumbe watajadili rasimu iliyo mbele yao ambayo ni ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba,” alisema Hamad.

Wasomi

Wasomi nchini wamesema mfumo wa kupiga kura ya wazi na siri uliopitishwa na Bunge Maalumu la Katiba, hautapunguza nguvu ya mijadala katika Bunge hilo katika vipengele muhimu ikiwa ni pamoja na aina ya muundo wa Serikali.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, wasomi hao walisema kuwa badala yake mfumo huo utawalazimisha baadhi ya wajumbe wasiokubaliana na misimamo ya vyama vyao kupiga aina ya kura wasiyoitaka.

Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa George Shumbusho alisema mjadala mkali unatarajiwa kuendelea bungeni hasa katika hoja ya aina ya muundo wa Serikali, kwa kuwa hotuba ya Rais Jakaya Kikwete iliashiria kutotaka muundo wa Serikali tatu.

Profesa Shumbosho alisema kuwa kuna baadhi ya wajumbe wa CCM hawakubaliani na muundo wa Serikali mbili, lakini watalazimika kupiga kura ya wazi ili kukiridhisha chama chao.

“Kuna watu hawana ujasiri. Ndani ya CCM wapo wanaopenda Serikali tatu lakini wanaogopa,” alisema Profesa Shumbusho.

Pia, alisema kuwa kwa namna hali inayoonekana kuendelea bungeni, kuna dalili kuwa maoni ya rasimu ya CCM kuhusu Katiba ndiyo yatakayopita na hivyo kurudisha mambo mengi yaliyopo katika Katiba ya sasa.

Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Gaudence Mpangala alisema kuwa upigaji kura wa wazi au siri hautazuia wajumbe kuendelea na misimamo yao na kwamba badala yake mjadala utakuwa mkali zaidi kuliko ilivyokuwa awali.

Alisema ingawa yapo baadhi ya mambo ambayo wajumbe wanaweza kukubaliana bila kupiga kura, suala la Muungano litakuwa na mvutano kwa kuwa tayari hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba na Rais Kikwete bungeni, zimeshaleta ‘msuguano’.

“Mjadala utakuwa mkali, suala lenyewe tu limeanza kuwa kali tangu mwanzo. Warioba alieleza Serikali tatu, Rais Kikwete akapinga,” alisema Profesa Mpangala.

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria, Hamad Salim alisema suala la kupiga kura ya siri au wazi limechukua muda mrefu kujadiliwa bila sababu za msingi.

Akifafanua, Salim alisema kuwa wanaotaka kura ya wazi wanajenga hoja kuwa wanataka masuala yote yawe wazi kwa wananchi, lakini wanashindwa kusema ni lini walipewa maoni hayo na wananchi.

“Sikubaliani na kura ya wazi, hawakutumwa na wananchi, walitakiwa kuridi kwao na kuwauliza aina gani ya kura wanataka,” alisema Salim na kuongeza:

“Kwa muda mrefu upigaji kura ulikuwa wa siri, sasa imekuwaje leo wanataka kura ya wazi?”

Sendeka

Mjumbe wa Bunge hilo, Christopha Ole Sendeka alisema matokeo ya kura za kupitisha kanuni ya 37 na 38 ya upigaji kura yamewashangaza Ukawa, lakini muhimu kwao ni kukaa bungeni na kujenga hoja.

“Matokeo ya jana (juzi) yamewakatisha tamaa kwa ushindi wa idadi nzuri ya kura, walidhani CCM haina theluthi mbili, lakini licha ya wabunge wengi hatohudhuria tumeshinda,” alisema Sendeka.

Alisema wingi wa CCM siyo ndani ya Bunge tu, kwani hata nje wengi wanakiunga mkono chama hicho.

“Vizuri wangekaa tu kwani CCM inaweza kupitisha mambo kwa kura nyingi zaidi, lakini wakiwepo tunaweza kufikia maridhiano katika baadhi ya mambo,” alisema Sendeka.

Umoja wabunge Wanawake

Naye Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wabunge, (TWP), Suzan Lyimo alisema utaratibu wa kura za wazi na siri utaleta vurugu na utekelezaji wake ni mgumu.

“Utaratibu huu ni mgumu kutekelezeka sasa sijui wanaopiga kura za wazi watakaa upande wao na wale wa siri upande wao, lakini ni mgumu kutekelezeka na hakuna nchi ambayo umeshawahi kutumika,” alisema.

Akizungumza na vyombo vya habari kwa niaba ya wabunge wanawake kutoka vyama vya upinzani, Suzan Lyimo alisema hotuba ya Rais Jakaya Kikwete imeleta madhara makubwa kwa wananchi hasa wale ambao hawana itakadi za vyama.

“Hotuba hiyo imeleta mpasuko mkubwa miongoni mwa Watanzania..., sisi kama wajumbe wa Bunge hili tunawahakikishia wananchi kwamba tutajadili Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayotokana na maoni ya wananchi,” alisema.

Kwa upande wake, Sabrina Sungura alisema mchakato huo wa Katiba unaweza usifike mwisho na kwamba mtu wa kwanza wa kulaumiwa ni Rais Kikwete ambaye alitoa hotuba ya kuwagawa wabunge.

“Tulipaswa kuambiwa kuwa Rais anatumia nafasi yake kama sehemu ya Bunge kuleta maoni yake na si kulizindua Bunge kama tulivyoambiwa katika ratiba,” alisema.

Naye Moza Abeid ametaka kurekebishwa upungufu uliojitokeza katika mchakato wa Katiba ili wananchi waweze kupata Katiba waitakayo.


Mussa Juma,Sharon Sauwa na Edith Majura, Goodluck Eliona. Chanzo: Mwananchi

Watu 12 wa familia moja wafa ajalini

Lori la mizigo aina ya Fusso likiwa limegongana na  gari ndogo aina ya Toyota Hilux Pick Up katika eneo la Hedaru, wilayani Same, Kilimanjaro, juzi na kusababisha vifo vya watu 12.  Picha na Alex Shirima

Moshi. Mji wa Hedaru uliopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro, jana ulizizima kwa vilio na simanzi baada ya waombolezaji 12 wote ndugu, kufariki dunia kwa ajali ya barabarani.

Waombolezaji hao wanawake, walipewa lifti ya gari na Diwani wa Kata ya Hedaru, Gerard Mgwena (CCM), kwa ajili ya kuwapeleka msibani eneo la Majengo ambako mtu mmoja alifariki kwa kusombwa na maji.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro (RPC), Robert Boaz alithibitisha ajali hiyo akisema ilitokea juzi saa 2:00 usiku na kwamba ilikuwa mbaya zaidi tangu kuanza kwa mwaka 2014.

“Ni ajali iliyohusisha magari matatu kwa wakati mmoja…; watu 11 walifariki pale pale na mwingine alifariki dunia leo (jana), asubuhi Hospitali ya Rufaa ya KCMC,”alisema Boaz.

Hata hivyo, alisema hakuwa na nafasi nzuri ya kufafanua kwa undani ajali hiyo kwa vile alikuwa nje ya Mkoa wa Kilimanjaro na kuelekeza atafutwe Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa (RTO), Joseph Mwakabonga.

Akizungumza kwa niaba ya RPC, Mwakabonga alisema, lori aina ya Mitsubish Fusso lililokuwa likitokea Moshi kwenda Dar liligonga kwa nyuma gari aina ya Toyota Hilux Pick-Up.

Alisema kuwa baada ya kuligonga gari hilo lililowabeba waombolezaji hao, nalo lilisukumwa na kwenda kuligonga lori aina ya Scania lililokuwa na tela lake.

Lori hilo aina ya Scania lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Moshi likiendeshwa na dereva wake, Gabriel David. Madareva wawili wa Toyota Pick-Up na Toyota Fusso wote hawajulikani waliko.

Taarifa zilizopatikana baadaye, zilisema dereva wa Fusso alikuwa amelazwa katika Hospitali ya KCMC, wakati Kigogo wa CCM aliyekuwa amewabeba waombolezaji akilazwa hospitali moja jijini Arusha.

Mwakabonga aliwataja waliofariki kuwa ni Stella John(45), Salma Kizoka (33), Marry Senzige (49), Neema Daniel (52), Rehema George (29) na Sophia Mbike (51).

Wengine ni Ritha Kalani (55), Mama Kalani Stephano (55), Kolina Mmatha(55), Bahati Daud(25) na Farida Kiondo mwenye umri wa miaka 25.

Majeruhi mmoja, Maria John (33) ambaye ni miongoni mwa watu 10 waliojeruhiwa, alifariki dunia jana asubuhi katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC alikolazwa kwa ajili ya kuokoa maisha yake.

Kwa mujibu wa watu walioshuhudia ajali hiyo, watu hao walipata ajali hatua 10 kutoka katika eneo ambalo ndugu yao aliosombwa na maji na kufa, ambapo maiti yake iliokotwa eneo hilo.

Alex Shirima mmoja wa mashuhuda alisimulia kuwa gari la diwani lilikwama kweye tope katikati ya Barabara ya Moshi Dar es Salaam.

Alisema, kabla ya kushuka kuangalia namna ya kulinasua gari lake, likatokea lori gari aina ya Fuso kwa nyuma ambalo liliigonga gari lake iwani na kulisukuma mita kadhaa mbele ambako lilikutana uso kwa uso na lori lingine aina ya Scania lililokuwa likitokea Dar es Salaam.

Alisimulia kuwa kutokana na ukubwa wa ajali hiyo, eneo hilo lilitapakaa viungo vya binadamu na damu.

Shirima ambaye ni dereva aliyefika katika eneo hilo dakika mbili baada ya ajali kutokea, alisema eneo hilo ni hatari kwa madereva kwa kuwa mvua zikinyesha, barabara hujaa maji na matope.

Hali ilivyo kijijini

Mmoja wa watoto ambaye mama yake mzazi amefariki katika ajali hiyo, Sebali Mkwizu alisema kuwa kijiji chao kimekumbwa na ukimya na majonzi, huku wakishindwa kuamini kilichotokea.

Alisema kuwa ajali hiyo imechukua maisha ya ndugu zake wanane na kati ya hao, saba walikuwa wakiishi kijijini hapo kwenye nyumba tofauti zinazofuatana.

“Nimepoteza mama yangu mzazi, mama mdogo, shemeji zangu watatu, mke wa ndugu yangu na watoto wawili. Hapa nyumba saba zina msiba,” alisema Mkwizu.

Alibainisha kwamba mazishi ya wanawake hao yanatarajiwa kufanyika leo katika eneo la pamoja kijijini hapo.

“Tumeambiwa watazikwa eneo moja, lakini bado hatujajua ni sehemu gani, hadi kesho (leo) ndiyo tutapata taarifa kamili,” alisema.

Chanzo: Mwananchi