Shirika la Kimataifa la Msalaba
Mwekundu (ICRC) limesema watu wenye silaha wamewateka wafanyakazi sita wa
shirika hilo na mfanyakazi mmoja wa kujitolea wa
shirika la Mwezi Mwekundu huko kaskazini-magharibi mwa Syria.
Shirika hilo limesema halijapata mawasiliano yoyote
na wateka nyara hao, kwa mujibu wa msemaji wa ICRC.
Awali, vyombo vya habari vya serikali
ya Syria
vilieleza kuwa watu hao wenye silaha walishambulia wafanyakazi wa Red Cross
waliokuwa wakisafiri kwa gari kati ya Sarmin na Saraqeb kwenye jimbo la Idlib.
Shirika la ICRC limesema limekuwa
likipata ugumu wa kuyafikia maeneo mengi ya Syria
kufikisha misaada kwa watu waliojeruhiwa au kuyakimbia makazi yao.
No comments:
Post a Comment