Wednesday, October 30, 2013

Kiongozi Muslim Brotherhood Misri akamatwa



Wafuasi wa Muslim Brotherhood wakiandamana kupinga kuondolewa kwa Rais Mohammad Morsi

Vyombo vya habari vya Misri vinaripoti kuwa serikali ya nchi hiyo imemtia mbaroni mwanasiasa maarufu Essam El Arian ambaye pia alikuwa ni mwanachama wa Muslim Brotherhood na Makamu Mwenyekiti wa chama cha Justice and Freedom ambacho pia ni sehemu ya Muslim Brotherhood.

Bwana El Arian ametiwa mbaroni katika mji mkuu wa Kairo.
Hapo awali mwendesha mashtaka wa nchi hiyo aliagiza Essam El Arian akamatwe tangu mwezi July baada ya Rais Mohammad Morsi ambaye pia alikuwa ni mwanachama wa Justice and Freedom kuondolewa madarakani.
Kukamatwa kwa kiongozi huyo ni moja ya hatua ya serikali iliyopo madarakani kudhibiti hatakati zinazoendeshwa na kundi hilo lenye itikadi kali za kiislamu ambazo zimepigwa marufuku.

Shirika la habari la serikali la Misri, Mena, limesema Bwana Erian anatarajiwa kufikishwa mahakamani wiki ijayo pamoja na Rais aliyoondolewa madarakani Mohammad Morsi na maafisa wengine wa Muslim Brotherhood.
Msemaji wa Muslim Brotherhood ameimbia BBC kuwa Bwana Erian alikamatwa siku ya jumatano akiwa nyumbani kwake mjini Cairo.

Picha zilizosambazwa kwenye vyombo vya habari vya Misri zinaonyesha kitendo cha kukamatwa kwake ambapo Bwana Erian anaonekana akiwa na tabasamu amesimama karibu ni mifuko miwili.
Mwandishi wa habari wa BBC aliyepo Cairo Orla Guerin anasema kabla ya Bwana Erian kwenda mafichoni alikuwa ni mwanachama maarufu wa Muslim Brotherhood.
Chanzo: BBCSwahili

No comments: