Wednesday, October 30, 2013

NDUGAI AWATOLEA ‘UVIVU’ WABUNGE

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Bw. Job Ndugai, amesema baadhi ya wabunge hawataki kuheshimu kanuni na miongozo inayotolewa na kiti cha spika hivyo kusababisha vurugu za mara kwa mara ndani ya Ukumbi wa Bunge.

Alisema upo umuhimu wa wabunge kuheshimu kanuni hizo ili kuepusha vurugu zinazojitokeza, kutoa ushirikiano kwa kiti cha spika na kuzingatia miongozo inayotolewa.
Bw. Ndugai aliyasema hayo Mjini Dodoma jana kwenye kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC) na kukanusha madai ya baadhi ya wabunge kudai kiti cha spika hakitendi haki bungeni.

Aliongeza kuwa, wakati mwingine wabunge wakiomba mwongozo, wanataka majibu yatolewe papo hapo mbali ya kujua kanuni zinasemaje kuhusu miongozo hivyo wakati mwingine husababisha vurugu zisizo na tija.
"Niwaombe wabunge wote hasa wapinzani, washirikiane na kiti cha spika ili Bunge letu liendeshwe kwa amani, si dhamira ya spika au Bunge kumtoa nje mbunge yeyote, kama tutafuata kanuni kama inavyotakiwa hakutakuwa na vurugu," alisema.

Alisema kiti cha spika huzingatia zaidi usawa na kutoa fursa kwa wabunge kuchangia mijadala mbalimbali kikizingatia suala zima la jinsia (wanawake kwa wanaume).
Aliongeza kuwa, hadi sasa hakuna muswada au mapendekezo yaliyofikishwa bungeni kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete lakini kama yatafika, wananchi watajulishwa kuhusu jambo hilo.

Aliwataka wabunge kuacha utoro bungeni badala yake wahudhurie vikao vya Bunge kwani ni aibu kuona viti vingi vikiwa tupu badala ya kujazwa na wabunge.
Akilizungumzia Bunge la 13 lililoanza Mjini Dodoma jana, Bw. Ndugai alisema Serikali imepeleka vipaumbele vikuu vitatu ambavyo ni miundombinu, kilimo, viwanda na biashara.

"Hii ina maana kuwa, bajeti kubwa ya mwaka ujao itakwenda kwenye miundombinu ambayo ni uboreshwaji wa reli, ujenzi wa madaraja, barabara, usafiri wa anga, bandari, vivuko na miundombinu ya majitaka," alisema.

Bw. Ndugai alisema licha ya Serikali kupeleka vipaumbele hivyo, wabunge wanaweza kuviondoa na kuweka vyakwao ambavyo wataona ni muhimu kutokana na faida zakeNAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Bw. Job Ndugai, amesema baadhi ya wabunge hawataki kuheshimu kanuni na miongozo inayotolewa na kiti cha spika hivyo kusababisha vurugu za mara kwa mara ndani ya Ukumbi wa Bunge.
 
Alisema upo umuhimu wa wabunge kuheshimu kanuni hizo ili kuepusha vurugu zinazojitokeza, kutoa ushirikiano kwa kiti cha spika na kuzingatia miongozo inayotolewa.
Bw. Ndugai aliyasema hayo Mjini Dodoma jana kwenye kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC) na kukanusha madai ya baadhi ya wabunge kudai kiti cha spika hakitendi haki bungeni.

Aliongeza kuwa, wakati mwingine wabunge wakiomba mwongozo, wanataka majibu yatolewe papo hapo mbali ya kujua kanuni zinasemaje kuhusu miongozo hivyo wakati mwingine husababisha vurugu zisizo na tija.

"Niwaombe wabunge wote hasa wapinzani, washirikiane na kiti cha spika ili Bunge letu liendeshwe kwa amani, si dhamira ya spika au Bunge kumtoa nje mbunge yeyote, kama tutafuata kanuni kama inavyotakiwa hakutakuwa na vurugu," alisema.

Alisema kiti cha spika huzingatia zaidi usawa na kutoa fursa kwa wabunge kuchangia mijadala mbalimbali kikizingatia suala zima la jinsia (wanawake kwa wanaume).
Aliongeza kuwa, hadi sasa hakuna muswada au mapendekezo yaliyofikishwa bungeni kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete lakini kama yatafika, wananchi watajulishwa kuhusu jambo hilo.

Aliwataka wabunge kuacha utoro bungeni badala yake wahudhurie vikao vya Bunge kwani ni aibu kuona viti vingi vikiwa tupu badala ya kujazwa na wabunge.
Akilizungumzia Bunge la 13 lililoanza Mjini Dodoma jana, Bw. Ndugai alisema Serikali imepeleka vipaumbele vikuu vitatu ambavyo ni miundombinu, kilimo, viwanda na biashara.

"Hii ina maana kuwa, bajeti kubwa ya mwaka ujao itakwenda kwenye miundombinu ambayo ni uboreshwaji wa reli, ujenzi wa madaraja, barabara, usafiri wa anga, bandari, vivuko na miundombinu ya majitaka," alisema.
Bw. Ndugai alisema licha ya Serikali kupeleka vipaumbele hivyo, wabunge wanaweza kuviondoa na kuweka vyakwao ambavyo wataona ni muhimu kutokana na faida zake
Chanzo: Majira

No comments: