Wednesday, October 30, 2013

Breaking News: 8 wauawa kwenye ajali ya treni Nairobi



Watu wanane wamethibitishwa kufariki katika ajali iliyohusisha treni na basi iliyokuwa imewabeba watu wakielekea kazini katika mtaa wa Umoja viungani mwa mji wa Nairobi.
Basi hiyo inayoaminika kuwa na watu 33 iligongwa na treni kwenye njia ya reli kuelekea mjini.

Walioshuhudia ajali hiyo wanasema kuwa basi hilo lilisukumwa umbali wa mita hamsini baada ya kugongwa.
Inaarifiwa watu sita walifariki papo hapo na wengine wawili kufariki baadaye kutokana na majeraha waliyoyapata.
Wengine wengi wamejeruhiwa kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu

No comments: