Tuesday, October 29, 2013

Mugabe aonya mawaziri dhidi ya 'nyumba ndogo'



Rais wa zimbabwe, Robert Mugabe ameonya mawaziri wake dhidi ya kuwa na 'nyumba ndogo' akisema kuwa mawaziri hao wanatumia mali zao nyingi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na wanawake wengi wasio wake zao.

Mugabe alitoa matamshi hayo wakati wa harusi ya mpwa wake.
Huku akiwasihi wanandoa kuwa waaminifu katika ndoa yao, Mugabe alionya dhidi ya kile alichokijata kama tabia ya wanaume kuwa na 'Nyumba ndogo' nchini Zimbabwe akisema kuwa mawaziri wake aliowatarajia kuwa watu wenye maadili mema , pia walikuwa na tabia ya uasherati.

Kwa mujibu wa jarida la New Zimbabwe, Mugabe alisema kuwa "mali ambayo baadhi ya waziri wanayo ndio chanzo cha matatizo kwenye ndoa. Nyumba ndogo sio jambo jema na alisema anajua kuwa mawazri wake wote wana tabia ya uasherati ambalo sio jambo jema katika jamii.''

"nawasihi muachane na tabia hiyo . Mwanamume mmoja na mke mmoja bila shaka itafanikisha ndoa zenu,'' alisema Mugabe.
Rais huyo wa muda mrefu ametoa changamto kwa wanawake kukataa tabia hiyo kwa kutojihusisha na wanaume walio kwenye ndoa.

"wanawake lazima wapigane dhidi ya tabia hii mbovu, lakini wao ndio walioko katika nyumba ndogo,'' alisema Mugabe.
Alisisitiza kuwa usawa wa kijinsia haupaswi kumaanisha kutupilia mbali tamaduni na maadili.

Mugabe alisema kwa mzaha kuwa japo hualiakwa kwa harusi nyingi, wakati waume na wake wanapotalikiana, huwa hajulishwi.
Alisema tabia hii ndio chanzo cha kuenea kwa ugonjwa wa ukimwi kwani anawafahamu mawaziri wengi wanaougua ugonjwa huo.

RAIS wa Zimbabwe, Robert Mugabe, ameonya mawaziri wake dhidi ya kuwa na ‘nyumba ndogo’, akisema kuwa wanatumia mali zao nyingi katika uhusiano wa kimapenzi na wanawake wengi wasio wake zao.
Alisema tabia hiyo ndiyo chanzo cha kuenea kwa ugonjwa wa ukimwi, kwani anawafahamu mawaziri wengi wanaougua ugonjwa huo.

Mugabe ambaye ameiongoza nchi yake tangu ilipojinyakulia uhuru wake mwaka 1980, alitoa matamshi hayo Jumamosi iliyopita wakati wa harusi ya mpwa wake.
Huku akiwasihi wanandoa kuwa waaminifu katika ndoa yao, Rais Mugabe alionya dhidi ya kile alichokitaja kama tabia ya wanaume kuwa na ‘nyumba ndogo’ nchini Zimbabwe, akisema kuwa mawaziri wake aliowatarajia kuwa watu wenye maadili mema pia walikuwa na tabia ya uasherati.

Kwa mujibu wa jarida la New Zimbabwe, Mugabe alisema kuwa mali waliyonayo baadhi ya waziri ndiyo chanzo cha matatizo kwenye ndoa. Na kwamba nyumba ndogo si jambo jema katika jamii.
“Nawasihi muachane na tabia hiyo. Mwanamume mmoja na mke mmoja bila shaka kutafanikisha ndoa zenu,”' alisema Mugabe.

Mugabe pia alitoa changamto kwa wanawake kukataa tabia hiyo kwa kutojihusisha na wanaume walio kwenye ndoa.
“Wanawake lazima wapigane dhidi ya tabia hii mbovu, lakini wao ndio walioko katika nyumba ndogo,” alisema.

Alisisitiza kuwa usawa wa kijinsia haupaswi kumaanisha kutupilia mbali utamaduni na maadili.
Mugabe alisema kwa mzaha kuwa japo hualikwa kwenye harusi nyingi, wakati waume na wake wanapotalikiana huwa hajulishwi.
                             

No comments: