Saturday, October 26, 2013

--------------------TANGAZO KWA WADAU--------------



Hadi kufikia Mwezi januari 2014 siku ya Mwaka mpya, Chiwambo’s Bblog inayopatikana kwa http://chiwambo.blogspot.com itabadilishwa Wavuti  hiyo  na kuwa http://chiwamboblog.co.tz chini ya Mlipa Media Group ambayo itakuwa rasimi kama Wavuti utakayotoa taarifa, Habari, Matukio na Michezo kila siku katika wilaya ya Tunduru pamoja na matukio mengine nje ya Tunduru.

Lengo la kuweka Wavuti huu ni kuwawezesha wanatunduru kujipatia taarifa za wilaya yao na inakuwa kama Online Newspaper, Pia mtu au taasisi yeyote inaweza kutangaza bidhaa zake pamoja ili kuongeza ushindani wa kibiashara huko Tunduru na maeneo mengine hapa nchini.

Pia Mlipa Media Group itafanya kazi ya Utafiti wa shughuli mbalimbali yaani “Research” kwa lugha ya kiingereza na kuziandikia. Hadi kufikia mwanzoni mwa mwaka 2015 tunatarajia Kuzindua kitabu kitakachoandikwa kwa lugha mbili yaani kiingereza na Kiswahili kitakachokuwa na jina “THE HISTORY OF YAO PEOPLE OF SOUTHERN TANZANIA” AU “HISTORIA YA KABILA LA WAYAO WALIOPO KUSINI MWA TANZANIA”. 

Ni matumaini yangu kuwa, wadau wa maendeleo Tunduru na wanaoitakia mema Tunduru na nchi yetu watashirikiana moja kwa moja na Mlipa Media Group katika shughuli zake zitakazoanzia rasmi 2014 siku ya mwaka mpya. 

Historia Fupi ya Wavuti “Website” ya Chiwambo’s blog imeanzia mwaka 2011 ikijulikana kwa jina la mimi na wewe, http://mimiwewe.blogspot.com, baadaye ilibadilishwa na kupewa jina la BASO Blog “http://sociologist-baso.blogspot.com, na Mwaka 2012 mwishoni ilibadilishwa na kuwa Chiwambo’s Blog  http://chiwambo.blogspot.com, na sasa ipo hatua za mwanzo za kuibadilisha blog hii na kuwa independent Website ambayo itaitwa chiwambo’s blog kama kawaida ila itapatikana kwa anuani ifuatayo; www.chiwamboblog.co.tz
 
Imetolewa na
AUSI CHIWAMBO,
Mwenyekiti wa Mlipa Media Group inayomiliki Chiwambo’s blog kwa sasa

No comments: