Mwanasiasa na kada mkongwe wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM), Peter Kisumo ameonya kuwa chama hicho kinaweza kuondolewa
madarakani kutokana na kunyamazia vitendo vya ufisadi na matumizi mabaya ya
rasilimali za umma vinavyotokea nchini.
Mzee Kisumo alitoa onyo hilo wiki iliyopita katika mazungumzo maalumu aliyofanya
na Mwananchi nyumbani kwake Dar es
Salaam kuhusu kumbukumbu ya miaka 14 ya kifo cha
Mwalimu Julius Nyerere inayoadhimishwa leo.
Alisema tatizo kubwa la chama hicho
ni kwamba kimemeendelea kuwa chama dola kikikaa mbali na wananchi, huku
kikishindwa kuidhibiti rushwa na kuwajibisha wahusika wa vitendo hivyo.
"Chama kimebaki kuwa cha
walalamikaji, kila mtu amekuwa mlalamikaji. Hata Waziri Mkuu amegeuka
mlalamikaji. Sijaona watu wanaowajibishwa kwa ufisadi," alisema Kisumo na
kuongeza:
"CCM haiwezi kujivunia ufisadi
unaoonekana nchini. Siwezi kusema imeukumbatia, lakini nasema imekuwa CCM bubu,
hata kuukemea ufisadi haiwezi. Utamaduni huu enzi za Mwalimu Nyerere
haukuwapo."
Alisema kutokana na udhaifu huo wa
CCM, kuna uwezekano mkubwa wa chama cha upinzani, na hasa Chadema kutumia
mwanya huo kuwashawishi wananchi na kushinda uchaguzi.
Kisumo ambaye alikuwa Mwenyekiti wa
Bodi ya Wadhamini wa CCM, alisema ingawa Chadema haijaonyesha wazi mambo
kinayoyapigania, kinaweza kutumia agenda ya ufisadi na matumizi mabaya ya
rasilimali za umma kuwavutia wananchi na kuchaguliwa.
Alitoa mfano wa tuhuma za baadhi ya
viongozi wa Serikali kuficha mabilioni ya shilingi kwenye benki za Uswisi, kuwa
zinaweza kuwa kete muhimu ya kuwaingiza Chadema madarakani, iwapo Serikali ya
sasa haitawashughulikia wahusika.
"Wakijitokeza na kuwataja majina
wahusika, wakasema fulani na fulani ndiyo wenye mabilioni haya Uswisi, na
Serikali ikasita kuwachukilia hatua, wakasema tukiingia madarakani
tutawakamata, wananchi wanaweza kuwaamini na kuwachagua," alisema na
kuongeza: "Wakishinda uchaguzi hata kwa viti vichache tu, watakosa nguvu
bungeni, lakini kwa wananchi watakuwa na nguvu sana.
Hii inaweza kuwasaidia kwa miaka
mitano ya kwanza. Wanaweza kupata ushindi mkubwa zaidi kwa mara ya pili na
wakiingia madarakani watawafunga viongozi wa zamani kweli."
Mzee Kisumo anasistiza, "Hili
linawezekana. Anayesema uwezekano wa CCM kushindwa haupo, anajikana mwenyewe.
CCM inabidi ijihami na majibu ya jinsi inavyotumia rasilimali za nchi."
Alionya kuwa si vizuri kuishia
kujinadi kwa mambo mengi mazuri iliyofanya huko nyuma, akitolea mfano kuwa hiyo
ni sawa na nguo nyeupe ambao ikiingia doa moja tu inakuwa haitamaniki tena.
"Sisemi kwamba hawajafanya kitu,
yapo mengi mazuri waliyoyafanya, lakini ufisadi ni sawa na doa kwenye shati
jeupe ambalo huwa linaonekana kuliko weupe na ung'avu wa shati hilo,"alisema Kisumo.
Alisema katika siku za karibuni
ufisadi umekuwa jambo la kawaida, hadi umegeuzwa kuwa wa kitaasisi, ambapo
aligusia hata Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo ulioanzishwa na Bunge kuwa ni sehemu
ya ufisadi.
Alihoji iweje fedha za umma zitumike
kumsadia mtu mmoja kujiimarisha kisiasa, akisema hiyo ni 'Built in Corruption'.
Mzee Kisumo pia alizungumzia mvutano
ambao umekuwa ukijitokeza kati ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) na
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwamba
msingi wa mvutano huo ni kuwapo tabaka la wahalifu wasioweza kuguswa na sheria.
"Unapokuwa na mvutano huo una
maana mbili, kwanza ni hali kwamba huyo mmoja anajua sabababu za watuhumiwa
kutochukuliwa hatua, lakini pili ni kwamba huenda tuna watu wawili katika
nafasi hizi, lakini wana nia mbili tofauti,"alisema Kisumo na kuongeza:
"Ni hatari sana unapokuwa na mfumo kwenye nchi ambao
unawalinda baadhi ya wahalifu, unakuwa na wahalifu wanaoguswa na wengine
hawaguswi, watu wanasubiri pengine itokee siku waone mtu wasiyemtarajia
anafikishwa mahakamani na hapo watajua kwamba kweli nchi imeamua kupambana na
rushwa na ufisadi."
...Aonya Zanzibar
Mzee Kisumo pia alizungumzia mchakato
wa mabadiliko ya Katiba Mpya na kwamba mvutano kuhusu muundo wa Muungano ni
matokeo ya upande wa Zanzibar kuachiwa kufanya
vitendo vingi vinavyoashiria kutafuta uhuru kamili kama
nchi nje ya Muungano huo.
Vitendo hivyo kwa mujibu wa kada huyo
ni mabadiliko ya kumi ya Katiba ya Zanzibar
ambayo yalitamka kuwa Zanzibar
ni nchi, kurejesha bendera yake, wimbo wake wa taifa na mambo mengine.
"Katika hatua sasa Zanzibar wanajiona kwamba wamekaribia kutimiza azma yao, kuelekea katika
'uhuru' kamili, nasema whoever (yeyote) aliyefumbia macho vitendo hivi akiwa
Rais, alifanya makosa makubwa,"alisema Mzee Kisumo na kuongeza:
"Ukitafakari hali hiyo, kama
tukiwa na mfumo wa Serikali Tatu, ni kitu gani kitawazuia Tanganyika nao
wasidai kuwa na Katiba sawa na ile ya upande wa pili? Ikifika hapo mimi sioni
Muungano kuwapo."
Hata hivyo, alionya kuwa masuala yote
yanayohusu Muungano ikiwa ni pamoja na lile la mabadiliko ya kumi ya Katiba ya Zanzibar, yanapaswa
kufanyiwa uamuzi wa busara kwani historia inaonyesha kuwa kuvunja Muungano
wowote ule lazima damu imwagike.
"Muungano wa States (nchi) za
Marekani uligharimu umwagaji damu, United Kingdom (Uingereza) pia damu
ilimwagika, kwa hiyo lazima tujifunze kwamba ikiwa tutafikia hatua ya kuvunja
Muungano wetu, hatuwezi kupita salama katika hili," alisema.
Alisema kinachotokea sasa kuhusu Zanzibar kuwa na mwelekeo
wa kujitenga, ilianza katika chaguzi zilizopita, pale ambapo Mzanzibari
aliyekaa nje ya visiwa hivyo kwa zaidi ya miaka mitano anakosa haki ya kupiga
kura kwa kukosa sifa ya ukaazi.
"Hili nalo ni tatizo kubwa,
Mzanzibari ambaye ameamua kuishi Moshi, Morogoro au kwingineko nchini uhalali
wake wa kuwa Mzanzibari unawekwa shakani, kwani hawezi kupiga kura kama
hajaishi Zanzibar
mfululizo kwa kipindi hicho," alisema Mzee Kisumo na kuongeza:
"Ukiangalia kwa Mtanzania wa
Bara, hakutani na kadhia hii, yeye ataishi popote hata kama nje ya nchi kwa
muda wowote, lakini akirudi nyumbani haambiwi eti si mkaazi, kama
ni Tabora atakwenda kwao au Mbeya".
Mzee Kisumo alisema kutokana na hali
hiyo kuna kundi kubwa la Wazanzibari ambalo linajikuta katika hatari ya kukosa
haki zao na kwamba ikiwa kutakuwa na mfumo wa Serikali Tatu na upande wa
Tanzania Bara kuanzisha utaratibu kama wa Zanzibar, watajikuta kwenye utata wa
uraia wao.
"Tukiwa na Tanzania moja iliyoungana, ambayo watu wake
hawana mwelekeo wa kuangalia masilahi yao
zaidi, haya mambo hayawezi kutokea. Kimsingi mtu yeyote ambaye ni raia wa Tanzania anapaswa kujivunia uraia wake kama Mtanzania na hapaswi kuishi kwa vikwazo vya aina
hii,"alisema Kisumo na kuongeza:
"Kwa hiyo mimi nasema haya mambo
lazima... Lazima tuyatizame kwa upana wake....Maana hawa watu wapo
wanaathirika, sihitaji kutaja majina ya watu hapa, lakini wapo, wanafahamika na
wengine ni wafanyabiashara wakubwa sana nchini,
wametoka Zanzibar
na wameishi Tanzania Bara kwa miaka mingi."
Kisumo alionekana kukerwa zaidi na
pendekezo la kuwapo kwa Serikali ya mkataba na kusisitiza kuwa wanaotoa mawazo
ya aina hiyo wanakusudia kuvunja Muungano kwa masilahi yao binafsi.
... Asema Nyerere alijaa katika mioyo
ya Watanzania
Wakati taifa leo linatimiza miaka 14
tangu kufariki kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Kisumo anasema kuwa
kiongozi hiyo alikuwa na sifa nyingi ambazo zilimfanya kujaa mioyoni mwa wa
Watanzania.
Akizungumzia sifa za Nyerere kabla na
baada ya uhuru wa Tanganyika
iliyokuja kuwa Tanzania
baadaye , Kisumo anaeleza kiongozi huyo alikuwa na uzalendo wa hali ya juu kwa
nchi yake na Bara la Afrika kwa jumla.
Kisumo, ambaye alifanya kazi na
kiongozi huyo kabla na baada ya uhuru, alisema sifa nyingine ya Mwalimu Nyerere
ilikuwa uwezo wake wa kushawishi na kuongoza.

"Vyama mbalimbali kutoka nchi za
Afrika Kusini, Angola,
Msumbiji na Namibia
vilileta watu wao kwa mafunzo ya kijeshi, jambo ambalo lilitutisha wakati
ule," anaongeza Kisumo.
Kisumo alisimulia kuwa Nyerere
alisimamia umoja na ukombozi wa Bara la Afrika na kumfanya ajizolee sifa sawa
na marais wengine kama Gamal Abdel Nasser wa Misri, Ben Bella wa Algeria na
Kwame Nkrumah wa Ghana.
Kisumo alisema kuwa Mwalimu hakuishia
kuunga mkono wapigania uhuru wa Afrika pia aliunga mkono harakati za
Wapalestina kujikomboa kutoka kwa Israel,
ambayo katika miaka ya mwanzo wa Uhuru ilikuwa kati ya wafadhili wakubwa wa Tanzania.
"Nakumbuka Kiongozi wa Chama cha
Ukombozi cha Palestina (PLO), Yasser Arafat alialikwa katika moja ya mikutano
ya chama cha TANU iliyofanyika jijini Dar es Salaam," anaongeza Kisumo.
Sera za uchumi
Kisumo anasema kuwa Nyerere alikuwa
anaamini kuwa Tanzania
itaendelea kiuchumi kama itawekeza vya kutosha
katika kilimo.
"Ndio maana katika miaka ya
mwanzo baada ya uhuru tulikuwa na sera ya 'Siasa ni Kilimo' na baadaye 'Kilimo
cha Kufa na Kupona'," alisema Kisumo.
Kisumo alisema kuwa baada ya kampeni
ya kilimo, Nyerere aliona umuhimu wa kujenga viwanda ili kutumia malighafi
iliyotoka katika kilimo.
"Ndio maana ukaona tukajenga
viwanda vya nguo katika Miji ya Dar es Salaam, Arusha, Musoma na Mwanza pia
kiwanda cha nyuzi pale Tabora," alisema.
Pia Kisumo alisema kuwa Mwalimu
aliweka mkazo katika elimu ya kujitegemea ili kumwandaa kijana wa Kitanzania.
"Hivi majuzi nilisikitika sana baada ya kusikia
ikiwa shule moja huko Kigoma imepokea msaada wa vyoo vya shimo kutoka kwa
Wachina! Hivi kweli imefika mahali wanafunzi wetu wanashindwa kuchimba
vyoo?" alihoji Kisumo kwa masikitiko.
Kisumo alisema kuwa mambo
yalibadilika katika miaka ya 1990 wakati Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza,
Margareth Thatcher alipoanzisha sera za ubinafsishaji na utandawazi.
"Hapo ndio yakabadilika ambapo
mataifa makubwa yakazidi kuzikandamizia nchi changa kupitia misaada ya Benki ya
Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF)," alisema Kisumo.
Kisumo alisema Mwalimu alipambana na
mataifa hayo makubwa na kutaka kuacha kukandamiza nchi changa. Alipambana na
mataifa kupitia Tume ya Kusini 1986, taasisi ambayo ilitokana na uliokuwa Umoja
wa Nchi zisizofungamana na upande wowote (NAM).
Imeandikwa na Neville Meena, Samson
Mfalila na Regnald Miruko
Chanzo:Mwananchi
No comments:
Post a Comment