Baraza la Congress nchini Marekani,
limepitisha mswaada utakaowezesha serikali kuendelea ma majukumu yake ya
kifedha na kuongeza muda wake wa kulipa madeni yanayoikabili. (HM)
Hatua hii imekuja masaa kadhaa kabla
ya serikali kutumbukia kwenye mkwamo wa kifedha.
Baraza la senate lenye waakilishi wengi wa Democtrats lilishinda kura ya mswaada huo kwa kura 81 dhidi ya 18
Mswaada ulipitishwa kwa kura 285 dhidi
ya 144 katika bunge la waakilishi ambapo wabunge wa Republican waliunga mkono
mswaada huo shingo upande.
Afueni hii kwa serikali ya Rais
Barack Obama imekuja masaa kadhaa kabla ya makataa ya kuongeza kiwango cha deni
la serikali hadi dola trilioni 16.7.
Mswaada huo sasa utawezesha serikali
kuendelea na majukumu yake ya kifedha na hata kuomba pesa zaidi kutoka katika
hazina ya serikali hadi Februari tarehe saba.
Pia itawezesha serikali kupata pesa
hadi Januari kumi na tano na kufungua mashirika ya kifedha katika majimbo na
kuwaresha kazini maelfu ya wafanyakazi wa serikali.
Ikulu ya White house sasa imewataka
wafanyakazi wa umma kurejea kazini leo.
Mswaada huo hata hivyo ni afueni ya
muda na sio suluhu kwa matatizo ya bajeti ya serikali ambayo yaliwagawanya
wanasiasa wa Republican na Democrats.
Baada ya mswaada kupitishwa, Rais
Barack Obama aliwaambia waandishi wa habari kuwa atasaini mswaada huo na
kuufanya sheria.
Chanzo: voaswahili
No comments:
Post a Comment