Chama cha walinzi wa mazingira cha
Ujerumani kimejiondoa katika mazungumzo ya serikali ya mseto na muungano wa
kihafidhina unaoongozwa na kansela Angela Merkel, baada ya kushindwa kupata
muafaka juu ya masuala muhimu.
Maafisa wa Chama cha mazingira
walioshiriki katika mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto.
Maafisa wa Chama cha mazingira
walioshiriki katika mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto.
Akizungumza na waandishi wa habari
baada kushindwa kwa mazungumzo kati ya chama chake na chama cha Christian
Democratic, CDU, cha Angela Merkel, mwenyekiti wa chama cha walinzi wa
mazingira Claudia Roth alieleza bayana kuhusu hatua inayofuata. ''Chama cha
walinzi wa mazingira hakitaki tena kuzungumza juu ya kuundwa kwa serikali ya
mseto'', alisema mwenyekiti huyo.
Viongozi wa chama cha walinzi wa
mazingira na wenzao wa muungano wa kihafidhina unaoongozwa na Angela Merkel,
waliyataja mazungumzo yaliyokwama kati yao kuwa ya wazi na mazito.
''Mazungumzo yamekuwa marefu, na
magumu. Badala ya kuzungukazunguka, yametuwama kwenye masuala muhimu. Hata
hivyo, tumeamua kwamba katika mkutano wetu wa chama, hatutalijadili suala la
kuunda serikali ya mseto.'' Alisema Claudia Roth.
Pengo kubwa kimtazamo
Hata hivyo pande hizo mbili
zilishindwa kupata maridhiano juu ya masuala muhimu kama vile kodi kwa watu
wenye kipato kikubwa, mageuzi katika bima ya afya, na kiwango cha chini cha
mshahara.
Claudia Roth, mwenyekiti wa chama cha
mazingira, Die Grüne. Claudia Roth, mwenyekiti wa chama cha mazingira , Die
Grüne.
Licha ya hayo, katibu mkuu wa chama
cha CDU, Hermann Gröhe, amesema mazungumzo kati yao na chama kinachotetea
mazingira ambacho ni hasimu wao mkubwa, yalikuwa hatua nzuri. ''Nadhani
mazungumzo yalikuwa na azma inayolenga mbali kupita siku za hivi karibuni; kila
upande kusikiliza mwenzake na kujaribu kupata muafaka. Hiyo ni hatua nzuri kwa
kazi tunayoifanya bungeni.'' Alisema.
Claudia Roth alisema haikuwepo haja
ya kuingia katika mkondo wa tatu wa mazungumzo, kwa sababu baada ya mikutano
miwili ambayo imeyajadili masuala yote kwa kina, hakuna upande ulioelekea
kulegeza msimamo wake. Kwa kuzingatia hali hiyo, amesema Bi Roth, hakuna msingi
imara kwa serikali ya mseto kati ya vyama hivyo.
Kukubali kutokubaliana
Kwa upande wake katibu mkuu wa chama
cha CDU, Hermann Gröhe, amesema anaamini pengo lililopo katika mitazamo ya
vyama hivyo linaweza kuzibwa. ''Nataka kusisitiza kuwa pamoja na tofauti za
kimtazamo, hakukuwa na kipengele katika mazungumzo ambacho tumekiona kama kitu
kisichowezekana kabisa'', amesema Gröhe.
Katibu Mkuu wa CDU, Hermann Gröhe
Katibu Mkuu wa CDU, Hermann Gröhe
Baada ya kupewa kisogo na chama cha
walinzi wa mazingira, Bi Merkel sasa anabaki na chaguo moja tu, nalo ni
kujadiliana na chama kikuu cha upinzani, SPD. Haitakuwa mara ya kwanza kwa
vyama hivyo kuwa katika serikali ya mseto, kwani vilifanya hivyo katika muhula
wa kwanza wa Angela Merkel.
Kura ya maoni ya umma iliyofanywa
hivi karibuni, imeonyesha kuwa wajerumani wengi wanapendelea serikali ya mseto
kati ya vyama hivyo vikubwa. Bi Merkel amekuwa akiwasaka washirika wa kuunda
serikali ya mseto tangu Septemba 22, baada ya chama chake kushinda uchaguzi
mkuu, lakini kikiwa na upungufu wa viti 5 bungeni kuweza kuunda serikali peke yake.
Mwandishi: Daniel Gakuba/DW English
Website
Mhariri: Josephat Charo
DW.DE.
No comments:
Post a Comment