Katika kipindi cha miaka 16 iliyopita
nchi ya Rwanda
imefanikiwa kuondoa kutoka jeshini wanajeshi watoto wapatao 3,000. Lakini
wakati juhudi hizi zinaendelea Umoja wa Mataifa unasema Kigali
imekuwa ikilisaidia kundi moja la waasi kutoka Congo
la M23 kuwaandikisha watoto nchini Rwanda
na kuwapeleka kuungana na waasi wa M23 kushiriki katika mapambano Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo.
Katika utaratibu wa kuwatoa watoto
jeshi Rwanda
kwanza hupeleka wapiganaji wa zamani wa FDLR kwanza kambi ya Mutobo ambako wapiganaji
wa zamani wote wanaume na wavulana wanakaa kwa miezi mitatu. Wanajeshi wa
zamani watoto kisha wanapelekwa kwenye kituo cha ushauri nasaha ambako
wanapatiwa ushauri, dawa, kurudi tena kwenye masomo yao ya msingi na juhudi zinafanywa za
kuwatafuta ndugu zao.
Lakini wakati Rwanda inafanya kazi
kusaidia watoto kutoka nchini mwake kurudi nyumbani mkuu wa kitengo cha
kumlinda mtoto katika Umoja wa Mataifa-MONUSCO mjini Kinshasa, Dee Brillenburg
Wurth, anasema Rwanda inaandikisha watoto wengine makusudi na kwa mfumo maalumu
ili kuwapeleka kufanya kazi kwa ajili ya kundi la M23 baadhi yao ni watoto
wenye umri wa miaka 11. Wakati MONUSCO haiwezi kufanya kazi nje ya Congo, Brillenburg Wurth anasema wana ushahidi
kwamba nchi ya Rwanda
hivi sasa inaandikisha watoto.
Bi.Wurth anasema kati ya watoto 122
waliohojiwa watoto 37 walikuwa wanyarwanda. Baadhi yao
waliandikishwa katika nchi yao, baadhi nchini Congo. Baadhi
wanafikiri walipatiwa mafunzo na jeshi la Rwanda na wengine hawakufahamu
iwapo walikuwa nchini DRC. "Wengi wao walitekwa nyara, kama
ilivyo kawaida kwa makundi yeyote yenye silaha, unakwenda kupora au unahitajika
kubeba silaha kutoka sehemu moja kwenda nyingine, unachukua watoto kutoka
vijijini na huwapi fursa ya kurudi tena. Watoto wengi takribani wote walianza
maisha yao kama watoto wa M23 wakibeba vifaa
kutoka mpaka wa Rwanda".
Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo anakanusha vikali kwamba Rwanda inaandikisha watoto. "Rekodi zetu katika mfumo wa jeshi ipo wazi. Rwanda haiwezi kuvumilia kuona watoto wanaandikishwa katika makundi yoyote yake yenye silaha, sio tu katika jeshi letu wenyewe."
Mkuu wa MONUSCO alisema mara ghasia
huko mashariki mwa Congo
zikimalizika na makundi yenye silaha yatokomezwe kisha uandikishaji wanajeshi
watoto utamalizika.
Marekani imeweka shinikizo lake yenyewe
kwa Rwanda ikisitisha msaada
wa kijeshi kwenda Kigali
kutokana na shutuma zinazotolewa kwa nchi hiyo kuandikisha kwake wanajeshi
watoto.
Chanzo: voaswahili
No comments:
Post a Comment