Wanafunzi 32 walala chini kwa miaka
mitano shuleni
Na. Mohamed Hamad KITETO
JUMLA ya wanafunzi wa kiume 32 wa
shule ya msingi na ufundi Kibaya iliyoanzishwa mwaka 1950 Wilayani Kiteto
Mkoani Manyara, wanalazimika kulala chini kwa zaidi ya miaka mitano kwa kukosa
vitanda.
Akisoma risala kwa mgeni rasmi leo
(jana) kwenye mahafali ya 58 toka kuanzishwa shule hiyo mmoja wa wahitimu hao
alitaja changamoto zinazo wakabili kuwa ni kukosemaka kwa vitanda vya wavulana
bweni
Zingine ni upungufu wa viti 39
vilivyopo 11, na meza 37 za waalimu zilizopo 13, vyumba vya madarasa 5
vilivyopo 8, nyumba za walimu 13 zilizopo 6 pamoja na matundu 23 ya vyoo kati
ya 6 yaliyopo.
Kwa mujibu wa risala iliyosomwa na
mmoja wa wahitimu hao imeeleza kuwa shule hiyo ni ya kutwa na bweni, ina jumla
ya wanafunzi 561 kati ya hao 304 ni wavulana na wasichana 257
"Mheshimiwa mgeni rasmi kwa
heshima kubwa na taadhima mbali na matatizo haya tatizo lingine ni kukosekana
kwa uzio hapa shuleni hivyo watu wanaingia shule kwa muda watakao"
Kwa mujibu wa mwalimu mkuu wa shule
hiyo Bi.Msangi alieleza MTANZANIA kuwa shule hiyo kwa sasa inakusudiwa kufungwa
kwa kukosa choo chenye hadhi hivyo kuhofiwa wanafunzi kudumbukia
Kwa upande wake Simon Parseko
(mwanafunzi) aliwaomba wadau wa elimu wilayani na nje ya Wilaya kuwasaidia
vitanda, magodoro na shuka kwani wamechoka kulala chini kwa zaidi ya miaka
mitano
"Mwalimu alituambia tuwaleze
wazazi watununulie vitanda ili tuje navyo hapa shuleni lakini ilishindikana
kutokana na kutojua aina ya kitanda kinachohitajika hivyo kutulazimu kuendelea
kulala chini"
Naye mgeni rasmi Bakari Mahanyu
ambaye pia ni mmoja wa maafisa wa Elimu Wilayani hapo alitupia mpira Serkali ya
Kijiji kuwa ndio wenye jukumu la kufanya ukarabati shuleni unapohitajika
Alisema Serikali imekwisha sogeza
huduma karibu na wananchi hivyo wenye jukumu la kuendeleza shule ni pamoja na
wadau wa Elimu, wazazi pamoja na Serikali ya Kijiji.
Chanzo: Mjengwablog
No comments:
Post a Comment