Miili miwili iliyoungua vibaya
aliyoopolewa katika eneo la kituo cha biashara cha Westgate nchini Kenya siku
ya Alhamisi inawezekana kwa kiasi kikubwa ikawa ni ya magaidi walioshambulia
kituo hicho, Mbunge mmoja wa Kenya ameiambia BBC.
Ndung'u Gethenji mwenyekiti wa kamati
ya Bunge inayochunguza shambulio hilo pia amesema mwili mwingine ambao
umepatikana unawezekana kwa kiasi kikubwa ukawa ni wa mmoja wa wanajeshi.
Mamlaka ya Kenya kwa sasa inaendelea
na uchunguzi wa kisayansi wa miili hiyo.
Karibu watu wapatao 67 walifariki
dunia wakati magaidi wanaodhaniwa kuwa ni wa kundi la wanamgambo wa Al Shaabab
waliposhambulia kituo hicho Septemba 21 mwaka huu.
Shambulio hilo lilisababisha eneo
hilo kuzingirwa kwa siku nne ambapo pia sehemu kubwa ya kituo hicho cha biashara
iliharibiwa.
Mamlaka ya Kenya imeyataja majina
manne ya watuhumiwa wa shambulio hilo, japo hawajatoa ufafanuzi zaidi.
Bado haijajulikana kama magaidi
waliofanya shambilizi hilo kama walitoroka au la na pia imekuwa ni vigumu kujua
idadi ya magaidi waliohusika kwenye tukio hilo.
Awali maafisa wa serikali ya Kenya
walisema inakadiriwa magaidi hao walikuwa kati ya 10 na 15 lakini picha za CCTV
zilionyesha magaidi wapatao wanne tu ndo waliokuwepo kwenye tukio hilo.
Tayari Kundi la Kigaidi la Al Shabaab
limeshakiri kuwa ndilo lililohusika na shambulio hilo kufuatia majeshi ya Kenya
kwenda nchini Somalia kupambana na kundi hilo.
Chanzo: BBCswahili
No comments:
Post a Comment