Kansela wa Ujerumani Angela Merkel,
ataongoza duru ya pili ya mazungumzo na chama cha watetezi wa mazingira Die
Grüne Jumanne hii, juu ya uwezekano wa kuundwa kwa kile ambacho kinaweza kuwa
mseto wa kihistoria.
Mkutano huo unafanyika siku moja
baada ya Merkel na viongozi wa muungano wa Merkel wa kihafidhina unaoongozwa na
chama chake cha Christian Democratic Union CDU, kukubaliana kufanya duru ya
tatu ya mazungumzo na chama kikuu cha upinzani cha Social Democrats SPD siku ya
Alhamisi.
Hata hivyo, katibu mkuu wa chama cha
CDU Hermann Groehe alisisitiza kuwa mazungumzo na wanamazingira yatachukuliwa
kwa uzito mkubwa. CDU na ndugu zao wanaoongoza jimbo la Bavaria, Christian
Social Union CSU, walipata ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi
uliopita.
Ni mazungumzo ya utafiti tu
Lakini Merkel anahitaji mshirika mpya wa kuunda naye serikali baada ya chama cha Waliberali FDP, walichoshirikiana nacho katika miaka minne iliyopita, kushindwa kuingia bungeni, na muungano wake wa CDU na CSU kushindwa kupata wingi wa kutosha kuuwezesha kuunda serikali kivyake.

Muungano wa Merkel ulifanya
mazungumzo yaliyodumu kwa masaa nane na SPD mjini Berlin, na katibu mkuu wa CDU
Herman Groehe alisema uamuzi rasmi kuhusu duru ya tatu ya mazungumzo
utatangazwa baadae hii leo, baada ya mazungumzo na die Grüne.
Katibu mkuu wa chama cha SPD Andrea
Nahles alisema mazungumzo na CDU yalishadidi sana. "Kwa baadhi ya mada
tunaona tunaelekea sehemu moja, kwa nyingine tunatofautiana, kwa mfano kuhusu
kima cha chini cha mshahara au kodi, alisema Nahles baada ya kukamilika kwa
duru ya pili.
Lakini katibu mkuu wa CDU Hermann
Groehe alisema mazungumzo ya sasa hayalengi kupata tahfifu madhubuti.
"Mazungumzo ya utafiti si sehemu ya kutafuta tahfifu thabiti, lakini kuona
iwapo inaleta maana kushiriki na upande mwingine katika majadiliano ya kuunda
muungano. Kwa hivyo kwangu mazungumzo ya sasa siyo ya kusikiliza yale
yanayotuunganisha au tunayotofautiana."
Raia wapendelea muungano mkuu
Merkel anatumai kuamua wiki hii ni chama gani anataka kuazisha nacho mazungumzo rasmi ya kuunda serikali. Ushirikiano na chama cha die Grüne, kilichopata asilimia 8.4 ya kura mwezi Septemba itakuwa mara ya kwanza kwa wahafidhina na wanamazingira kugawana madaraka kwa ngazi ya taifa nchini Ujerumani. Lakini tofuati kubwa bado zipo kati ya CDU/CSU na chama cha Kijani, zikiwemo juu ya kuendeleza matumizi ya nishati rafiki na mazingira, na katika maeneo kama vile sera ya wakimbizi na haki za mashoga.

Baada ya mkutano wao wa kwanza na
Merkel wiki ilyiopita, viongozi wengi wa Kijani wana mashaka iwapo mazungumzo
ya leo yatasababisha awamu nyingine na CDU na CSU. Mwenyekiti wa chama cha CSU
na waziri mkuu wa jimbo la Bavari Horst Seehofer, wiki hii alirejelea tena
kuelezea kupendelea kwake kuunda serikali ya muungano mkubwa na SPD, kuliko
kuungana na wanamazigira.
Uchunguzi wa maoni uliofayika hivi
karibuni umeonyesha kuwa theluthi mbili ya Wajerumani wangependelea muungano
kati ya vyama vikuu viwili - yaani muungano wa Merkel na SPD.
Mwandishi: Iddi Ismail
Ssessanga/afpe,dpa
Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman
Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman
No comments:
Post a Comment