Wajumbe wanaoshiriki katika mazungumzo
Mataifa matano makubwa duniani pamoja
na Ujerumani yaanza mazungumzo na Iran juu ya mpango wao wa nyuklia, huku
wanadiplomasia wakisema nafasi ni ndogo ya kusuluhisha utata wa takriban muongo
mmoja juu ya mpango huo.
Mataifa hayo sita yenye nguvu duniani Marekani, Urusi, China,
Ufaransa, Uingereza na Ujerumani yataiwekea msukumo mkali Iran katika
mazungumzo ya siku mbili yanayofanyika mjini Geneva.
Mataifa hayo yanataka kuishawishi Iran kukubali kuachana na
mpango wa nyuklia ili waweze kundolewa vikwazo vya uchumi walivyoekewa.
"Mazungumzo yameanza," alisema mmoja wa
wanadiplomasia wa nchi za Magharibi.
Rais wa Iran Hassan Rouhani
Awali Iran imekuwa ikikataa kushiriki katika mazungumzo hayo
na ikipuuzilia mbali shutuma za Magharibi kwamba wanapanga kutengeneza silaha
za nyuklia.
Lakini tangu kuchaguliwa kwa rais mpya wa Iran Hassan Rouhani
mwezi Juni mwaka huu kumekuwa na matumaini makubwa kuwa huenda kukawa na maafikiano
hasa ikizingatiwa kuwa vikwazo ilivyoekewa Iran vinazidi kuyumbisha uchumi wa
nchi hiyo.
Hata hivyo kuhusiana na suala zima la utengenezaji wa silaha
za nyuklia Iran inaendelea kukanusha hilo huku ikisema kwamba mpango wake ni
kwaajili ya matumizi ya amani.
Iran yasema iko tayari kushiriki kikamilifu katika mazungumzo
Kulingana na maafisa wa Iran, wako tayari kuridhia matakwa ya
kimataifa ya kupunguza shughuli zao za nyuklia ili kujenga uaminifu kati yao na
mataifa ya Magharibi.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Iran Javad Zarif na mkuu wa
sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton ni miongoni mwa wanaohudhuria
mazungumzo hayo.
Mkuu wa sera za kigeni wa EU Catherine Ashton na waziri wa
mambo ya nchi za nje wa Iran Mohammad Javad Zarif Mkuu wa sera za kigeni wa EU
Catherine Ashton na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Iran Mohammad Javad Zarif
Ashton amesema kwa sasa Iran imetoa mpango mpya wa kutatua
hali ya wasiwasi kati yake na mataifa ya Magharibi. Naye Msemaji wa Umoja wa
Ulaya Michael Mann hakutoa maelezo zaidi juu ya mpango huo lakini akasema
ujumbe ulioandamana na Ashton utaliangazia jambo hilo kwa kina.
Huku hayo yakiarifiwa Israel imesema mataifa hayo sita
yanayoendelea na mazungumzo na Iran yanapaswa kuhakikisha kuwa Iran inaachana
kabisa na mpango wake wa nyuklia na kutoiondolea vikwazo .
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema mtambo wa kutengenezea nyuklia wa iran unapaswa kufungwa na zana vyote ziliomo ndani kusafirishwa hadi mataifa ya ulaya.
Mwandishi: Amina Abubakar/dpa/Reuters
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman
No comments:
Post a Comment