Kikundi cha viongozi wa dini nchini
Syria kimetoa Fatwa inayowaruhusu watu wanaoishi katika vitongoji vya mji mkuu
Damscus vinavyokumbwa na vita kula nyama ambayo kwa kawaida huwa imeharamishwa
Kwenye kanda ya video, viongozi hao
walisema kuwa watu wanaokumbwa na njaa wanaweza kula nyama ya Paka,Mbwa na
Punda.
Fatwa hiyo imetolewa huku kukiwa na
ripoti za watu kukumbwa na njaa katika kitongoji cha Muadhamiya mjini Damsacus
moja ya vitongoji vilivyotekwa na waasi
Mashirika ya misaada yameitaka
serikali kuruhusu misaada ya kibinadamu kupelekwa katika eneo hilo , ambako
wenyeji wamekwama.
Mamia ya raia , hata hivyo
walifanikiwa kutoroka maeneo hayo mwishoni mwa wiki baada ya vita kusitishwa
kwa muda.
Katika ujumbe wao wakati wa sherehe
za Eid al-Adha viongozi wa kidini waliwashauri wenyeji wa eneo la Ghouta kula
nyama ambazo kwa kaiwada huwa haziliwi katika dini ya kiisilamu.
Viongozi hao walisema huu ni wito kwa
dunia nzima na kuongeza kuwa ikiwa hali itaendelea ilivyo, watu wanalio hai
watalazimika kula wafu.
Sio mara ya kwa fatwa kama hii kutolewa
kwenye mzozo wa Syria.
Fatwa sawa na hii iliwahi kutolewa
mjini Homs na Aleppo wakati mapigano yalikuwa mabaya zaidi katika miji hiyo.
Mashirika ya misaada ambayo yamekuwa
yakitoa msaada wa chakula katika maeneo ya vita yamesema kuwa lazima jambo hilo
liwe muhimu kama ilivyo kuharibu silaha za kemikali za Syria.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment