Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia
na Maendeleo, CHADEMA, Dk Wilbrod Slaa leo Jumapili 13 Oktoba amesafiri kurudi Tanzania
baada ya ziara yake iliyomchukua wiki tatu nchini Marekani.
Dk Slaa aliwasili nchini Marekani
tarehe 21 Septemba 2013 akiambatana na mkewe mama Josephine Mushumbuzi
na kupokelewa na Uongozi wa Chadema DMV.
Tarehe 22 Septemba 2013 Dr Slaa
alifanya mkutano uliojumuisha wanajumuia ya Watanzania waishio katika Majimbo
ya Washington, Maryland
na Virginia.
Katika ziara yake Dk Slaa alitembelea
majimbo ya North Carolina na Alabama ambako alitembelea Vyuo Vikuu na
Taasisi mbalimbali na kujifunza Shuguli nyingi za Maendeleo katika Sekta
mbalimbali ikiwemo Kilimo, Afya, Nishati na Uchumi.
Akizungumza akiwa uwanja wa Ndege wa
Dulles mjini Washington Dk Slaa alisema alichojifunza akiwa Marekani anatarajia
kupeleka maarifa hayo Tanzania
ili yaweze kumkomboa Mtanzania kutoka katika Umaskini. Moja katika mambo ambayo
amejifunza ni namna ya kutumia nishati ya Jua kuzalisha umeme hasa kwa wakazi
wa Vijijini.
Dk Slaa amekamilisha ziara yake ya
wiki tatu nchini Marekani iliyopewa jina la "Vision Tanzania"
baada ya kualikwa na Umoja wa Vyuo vikuu nchini Marekani.
Taarifa hii imetolewa na waratibu wa
CHADEMA Blogs
No comments:
Post a Comment