Aidha halmashauri hiyo imeiagiza Serikali mkoa ihakikishe katika msimu huu
mkulima analipwa malipo yake yote. PICHA|MAKTABA
Na Abdallah Bakari,Mwananchi
Mtwara. Chama Cha Mapinduzi (CCM)
mkoani hapa kimepingana na Bodi ya Korosho Nchini (CBT) juu ya tafsiri ya bei
dira ya zao hilo katika msimu 2013/14, huku kikiwataka wakulima kuwa makini ili
haki na maslahi yao yasiporwe na wajanja wachache.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na
chama hicho kwa waandishi wa habari na kusainiwa na Katibu wa chama hicho
mkoani hapa, Shaibu Akwilombe,uamuzi huo ulifikiwa Oktoba,12 mwaka huu mjini
Mtwara.
Alisema halmashauri kuu ya mkoa baada
ya kukutana katika kikao kilichofanyia mjini hapa, wajumbe walifikia uamuzi wa
kutokubaliana na mwongozo wa mauzo ya korosho uliotolewa na Bodi ya Korosho
Tanzania (CBT) Oktoba, 2013.
Akwilombe katika taarifa yake hiyo
alifafanua zaidi kuwa, kwa mujibu wa tafsiri ya CBT, bei dira sio kinga ya bei
kwa wakulima wa korosho kitendo alichokidai kinatoa mwanya kwa watendaji wasio
waaminifu kujinufaisha na zao hilo. “Tafsiri hii mpyainaondoa na kufuta maana
sahihi ya Mfumo wa Stakabadhi Ghalani bali inajenga mazingira ya kuwandaa
wakulia kudhulumiwa…katika hili tunasema hapana,”.
Aidha halmashauri hiyo imeiagiza
Serikali mkoa ihakikishe katika msimu huu mkulima analipwa malipo yake yote
ndipo makato yanayotozwa na vyama vya ushirika na halmashauri za wilaya yafuate
ili kumlinda mkulima kubeba mzigo wa hasara.
Mkurugenzi wa CBT,Juma Mfaume
Mkanachapa alisema,“Pesa ya malipo ya awali ni ya mkulima mwenyewe, ilitakiwa
mkulima akusanye korosho na kuzikabidhi kwa chama cha ushirika,zikiuzwa afuate
fedha zake kwa mujibu wa soko sio bei dira”alisema.
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment