WARENO 1500 – 1800
Ukiristo uliletwa kwa mara ya mwanzo Zanzibar na Wareno. Wareno wakielekea
juu kutoka kusini baada ya kufanikiwa kuizunguka Rasi ya matumaini mema – Cape
of Good Hope katika mwaka 1488 walifanya jaribio la nguvu la kudai bandari,
njia za biashara na raslimali kiasi cha maili 2000 za mwambao wa Afrika.
Mara tu ya kuwasili Zanzibar Wareno katika mwaka 1499 walianzisha Ujumbe
wa Kanisa la Kikatoliki na kituo cha biashara ndani ya mji wa Zanzibar. Wareno kwa miaka 200
iliyofuata walihodhi njia za baharini za meli za Afrika Mashariki na
walijitahidi kuanzisha msururu wa makaazi katika eneo la mwambao. Mabaki
ya makaazi ya Wareno bado yanaweza kuonekana karibu na Fukuchani Kaskazini
Unguja na Kisiwani Pemba. Ngome Kongwe
ambayo ipo karibu na bandari ya mji wa Zanzibar
ilijengwa juu ya eneo lilipokuwepo kanisa dogo la kikatoliki la mwanzo baada ya
kutekwa na Jeshi la Oman.
Jeshi hili la Oman
inasemekana liliitwa na wenyeji wa Zanzibar na Pemba ili kuwasaidia kuwangóa Wareno waliokuwa makatili
na madhalimu.
Baada ya miongo ya vita na maangamizo ambayo yaliyoshuhudi kuwaka
moto mji wa Mombasa,
Wareno walirudi nyuma, na kurejea kuendea kusini, mbali na mafikio ya
mashambulizi ya moja kwa moja ambayo yaliyotokana na pepo za miongo za jahazi
(waarabu).
PICHA ZA WATUMWA MJINI ZANZIBAR
OASISI YA UVUMILIVU (OASIS OF
TOLERANCE)
Katika mwaka 1841 mpiganaji wa
Kioman/Oman Sultan, Seyyid Said alivutiwa sana
na visiwa hivyi vya Zanzibar kwa hiyo
alihakikisha anahamishia makao makuu yake Zanzibar
kama ni mji mkuu. Malezi yake katika maisha ya Jangwani
yalimshajiisha yeye kwa nguvu zake zote kuviendeleza visiwa hivyi vyenye
ustawi. Sultan Seyyid Said aliona Zanzibar kama kama ni
Oasisi katika bahari. Alisimamia
mipango mikubwa ya upandaji miti,
alichimba visima vya maji vyingi tu na kujenga nyumba nyingi ambazo zilitosha
mamia ya wageni.
Sultan alitambua wageni
watakaa na kujiliwaza katika Oasisi. Na
alijua kwamba biashara itakuwa na kufanyika katika eneo hili ikiwa
litaimarishwa kwa vitu na mambo mengine pamoja na usalama. Vile vile alitarajia na kutambua kwamba
angelipata asilimia fulani inayotokana na shughuli za kibiashara zitakazo
endeshwa Visiwani kama ni malipo ya kuviimarisha visiwa hivyi. Aliwakaribisha na kuwaomba wafanyabiashara
kutoka India kufungua matawi
ya ofisi zao ndani ya Zanzibar
ili kuimarisha biashara. Wafanyabishara
hawa wengi kutoka India
walikuwa ni raia wa kiingereza hii ilikuwa ni kwa sababu ya kutekwa India na
Uingereza.
Kwa maana hiyo, alianza
kuwakaribisha maofisa wa kiingereza visiwani ili kuwakilisha maslahi ya raia
hawa wahindi wa kiingereza. Mara tu tena
baadae alianza kuingia katika mikataba rasmi ya kibiashara na Serikali ya
kiingereza na Serikali nyengine za Magharibi.
Majengo ya biashara yalijengwa ndani
ya Mji Mkongwe na Kampuni za Kimarekani, Kijerumani, Ufaransa na na
Kiingereza. Bandari ya Zanzibar ilitoa huduma za fueli na kufanyia
matengenezo Meli za kivita na vyombo vya usafiri vya wafanyabiashara. Meli hizi zilileta mapote ya ziada ya watu wa
magharibi ndani ya Zanzibar. Kama ni
makaribisho mema ya wageni wengi katika Oasisi yake. Sultani aliruhusu watu wa imani zote
kuendesha shughuli zao za kidini walivyopenda.
Akiwa Muislamu mwenye imani kamili,
Sultani alionyesha mfano bora wa uvumilivu juu ya mahitajio ya kidini ya watu wengine. Wakati huo huo akijenga furaha na imani
katika dini ya mababu zake, kwa bidii zote.
Warithi wake alifuata utaratibu wa Sultani Seyyid, wakiruhusu kuanzishwa
mahekalu mengi tu ya kihindi, makanisa mawili, moja la kikatoliki na
kiprostanti, sehemu za kimazishi za zoroastriani na misikiti kwa kila dhehebu
kuu au dogo la kiislamu ndani ya mji mmoja.
1800 – 1900
WAKATOLIKI, MAKUNDI YA WAKIRISTO
WASIOPENDA MIKUTANO ASMI, VITA AU GHASIA (QUAKERS) NA UJUMBE WA VYUO VIKUU KWA
AFRIKA YA KATI ( UMCA)
Baada ya Wareno kurudi nyuma
Wakiristo kidogo tu Wakigoa ndio waliobakia Zanzibar.
Wakiristo hawa hawakuwa na kanisa la kufanyia Ibada lakini waliweza
kuifanya hai jumuia yao
kwa kwa kuifanya ibada zao kibinafsi.
Baadae katika miaka 1800 makundi ya watu wa wamagharibi yalianza
kujumuisha wamisionari na wachungaji wamisionari waliokuwa wakipita pita mara
chache na wachungaji katika meli bandarini.
Katika mwaka 1844 wamisionari wa kikiristo zaidi wa kudumu waliwasili
Afrika mashariki kwa kupitia mchungaji wa kilutheri Joseph Krapf na wafuasi
wawili ambao walifanya kazi kwa ajili wa Jumuia ya kimisheni ya kanisa la
kiingereza (English Church Missionary Society).
Wakifanyakazi, Mombasa, walitembelea Zanzibar na miaka
michache mbeleni walitoa kamusi bora kabisa la Kiswahili lakini hawakuwahi
kuanzisha kanisa ndani ya visiwa hivyi.
Ukuwaji wa harakati dhidi ya utumwa
ndani ya Uingereza ulishajiisha raghba ya wamisionari wakiristo, ikikuzwa na
hotuba ya David Livingstone aliyoitoa mwaka 1857 akiomba Uingereza kupeleka
wamisionari na wafanyakazi Afrika. David
Livingstone alilingania kwamba mwisho wa utumwa utakuwepo tu kupitia “ biashara
na ukiristo”. Baadae Livingstone
alitumia siku nyingi tu Zanzibar
ambao alipatiwa nafasi ya kutumia nyumba ya Sultani.
Hotuba zake zilipelekea kuundwa kwa
ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati
(UMCA). Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika
ya Kati ulikuwa ni mashirikiano baina ya kitivo na wanafunzi waliopitia vyuo
vikuu vya Oxford and Cambridge,
ambao baadae tu waliungana na mashabiki kutoka vyuo vikuu vya Durham
na Dublin. Katika mwaka 1860 walimchagua Charles
Mackenzie kama ni “Askofu wa Afrika ya kati”
na ilipofikia mwezi wa Oktoba wa 1860 alikuwa njiani kuelekea huko Afrika ya
Kati.
Lengo la ujumbe wa vyuo vikuu kwa
Afrika ya kati (UMCA) lilikuwa ni kufikisha dini ya kikiristo kwa watu wengi sana waliokuwa Afrika ya
Kati, kuzunguka ziwa Nyasa, ambalo Livingstone alilizungumzia kwa ufanisi. Kwa ajili hiyo, baada ya kufika Afrika Kusini
Askofu Mackenzie na wafuasi aliokuwa nao walisafiri kwa boti mpaka mto Zambezi
na baadae hadi mto shire kuasisi ujumbe wa mwanzo wa ujumbe wa vyuo vikuu kwa
Afrika ya Kati katika Afrika katika sehemu iliyojulikana kama
Magomero.
Wakati ujumbe huu na eneo lake ulichukuana
na jina na ari ya jumuia mama, Ujumbe huu ulishuhudia kushindwa kwa aina yake kutekeleza malengo
yake. Maradhi na njaa na ukame
uliwakumba wamisionari wa mwanzo na kupelekea kufa kwa askofu. Kundi hili lililazimika kuondoka katika eneo hilo ndani ya kipindi
cha miaka mitatu kwa sababu eneo hilo
lilikuwepo mbali sana na upatikanaji wa bidhaa kutoka nje na vituo vya
mawasiliano, eneo hilo halikuwa na mazingira mazuri ya kiafya kwa wale ambao
hawana uzoefu na mazoea na hali ya hewa ya hapo na pia eneo halikuwa na utulivu
wa kisiasa. Askofu mpya, George Tozer,
kwanza alijaribu kuupeleka ujumbe maili 200 mafikio ya mtiririko wa mto
kuelekea eneo la muanuko lakini hata hivyo eneo hilo mara tu
liligundulika kuwa halikuwa na mazingira mazuri ya kiafya na kwa hiyo
lilihamwa kwa miezi hivi tu.
Wakichukua bidii za makusudi, ili
kutorejea makosa yaliyopita viongozi wa ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati
(UMCA) waliangalia uwezekano wa kituo au eneo jengine ambalo litatumika kuweza
kufika kati kati ya Afrika. Maeneo mbali
mbali yalifikiriwa kutumika kama Kisiwa cha Johanna, maeneo katika mwambao wa Afrika Kusini lakini
kwa bahati Zanzibar ilikubalika kutumika kutokana na muundo mzuri wa njia za
mawasiliano, upatikanaji mzuri wa bidhaa za chakula na wingi wa upatikanaji
nguvu kazi bora. Ujumbe wa Vyuo Vikuu
kwa Afrika ya Kati (UMCA) uliobakia uliwasili Zanzibar tarehe 31/08/1864.
Ujumbe huu ulipowasili ulipokewa na
wamisionari wakatoliki wa Kifaransa.
Wamisionari wa kikatoliki waliwasili mwanzo Zanzibar kwa kiasi ya miaka minne kabla ya
wamisionari wa kiingereza. Katika mwezi
Septemba mwaka 1860 Abbe Favat ambaye alikuwa Mfaransa mdini maarufu mwenye nguvu alitiliana mkataba na
Seyyid Said kumruhusu yeye Abbe Favat kuhamishia Makao Makuu yake katika Kisiwa
cha Reunion na kuwa Zanzibar kufikia mwezi Disemba kikundi chake cha “mapadri
wawili wasio watawa na watawa sita wa kike” (“Filler de Marie”) walikuwa
wakiishi katika makaazi ya watawa ambayo pia yalikuwa na kanisa dogo hapo
Shangani.
Jengo hili la watawa
linasemekana na lilijengwa katika mwaka 1860, lakini ujenzi huu inawezekana
ulikuwa ni matengenezo makubwa ya nyumba iliyokuwepo kabla. Kanisa dogo katika jengo hili lilikuwa ni
kanisa la kwanza lililojengwa Zanzibar
kwa miaka 200.
Ruhusa iliyotolewa na Sultan Majid
kwa Wafaransa hawa kuanzisha duka ndani ya Zanzibar
ilitafsiriwa kama ni juhudi za Sultani za
kuweka “ uwiano wa nafasi kubwa waliokuwa nao Waingereza Zanzibar kwa
kuwakaribisha wapinzani wao wakuu wa kizungu.”
Ikiwa ushindani wa kisiasa ndio uliompelekea Sultan Majid za kukaribisha
pamoja matawi tofauti ya wamisionari wakiristo hata hivyo matokeo hayakuwa hayo
kwani kwa upande wa wamisionari hawa hakukuwa na msuguano wowote. Mahusiano yao mazuri makundi hayo mawili ya wamisionari
ulitokana na ukweli kwamba Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati wa
kianglikana (UMCA Anglicans) ulikuwa ni ujumbe wa watu watukufu ambao wenye
mafunzo ya kikatoliki ya kiengereza (Anglon Catholic Learnings)
Wamisionari wakifaransa walikuwa
makini kuepuka matatizo yoyote Zanzibar “kwa kutambua uhalisia wa maisha ulivyo
ndani ya nchi ya kiislamu ya Zanzibar, Wafaransa kuanzia 1862 wafuasi wa Holy
Ghost Order, waliamua kujikita katika maeneo maalum kama ya elimu, shughuli za
uchungaji kwa jumuia ndogo ya mjini ya magoa wakatoliki na huduma za afifu na walifungua
hospitali ya mwanzo iliyopendekezwa na Sultani ya kizungu. Kwa hili waliojenga maoni mazuri kwa warabu.
Juu ya ukarimu wa watu wa Zanzibar, Wazanzibar hawa
kidogo hawakuwa na azma yoyote kufuata imani ya wageni hawa wapya. Wamisionari wa kikatoliki walilielewa hili
lakini waliamini kwamba kundi kubwa la wafuasi wapya wa dini hii ya kikiristo
litaweza kupatikana masafa machache kuvuka mlango bahari wa Zanzibar huko Tanzania Bara. Walipeleka ujumbe mdogo Bagamoyo katika
mwambao wa Tanzania Bara katika
mwaka 1868 na kwa sehemu kubwa walitumia nafasi walizonazo Zanzibar
kama ni makao makuu ya kuzidisha harakati zao
Tanzania Bara. Harakati hizi ikiwemo
ujenzi wa “ Hospitali ya Kifaransa”
ndani ya Bagamoyo.
“ Hospitali ya Kifaransa” ndani ya Zanzibar ilijengwa mkabala na jengo la
watawa. Hospitali ilimalizwa kujengwa na
kuanza kazi kufikia mwaka 1890. Kipindi
hicho wakatoliki walien delea kutumia uhusiano mzuri na majirani zao wa Zanzibar, wakipata ruhusa
ya kujenga kanisa la mtakatifu Joseph katika mwaka 1894. (Cathedral of Saint
Joseph in 1894). Jiwe la msingi la
kanisa hili kuu liliekwa tarehe 10 Julai 1896.
Misa ya mwanzo katika kanisa hili kuu jipya iliendeshwa na Askofu
Allegeyer katika usiku wa krismas 1898.
Kadri ya wakati ulivyokuwa ukienda,
hospitali hii ya Zanzibar ilipungua umuhimu wake
na jengo hilo
likafanywa kuwa ni skuli. Hii ilikuwa ni
skuli ya kitawa ya mtakatifu Joseph (St.
Joseph Convent School).
Wamisionari wa Ujumbe wa Vyuo Vikuu
kwa Afrika ya Kati (UMCA) hawakuzubaa katika kipindi hichi. Akianzia kwanza kuishi katika nyumba Mambo
Msiige, katika eneo la Shangani, ambapo haikuwa mbali na ujumbe wa Kifaransa,
Muingereza mchapa kazi shupavu alianzisha ustawi wa majengo ya ukubwa wa
kuvutia na ya aina tofauti. Kwanza walinunua sehemu ya ardhi ya kilimo Kiungani
pembezoni mwa mji wa Zanzibar Kaskazini.
Ujenzi wa “bweni kwa ajili ya vijana watumwa walioachiwa huru”
uliendelea katika eneo hilo
kufikia mwaka 1866. Karibu ya hapo mava
sehemu ya kuzikia ilianzishwa, na hadi leo mava hii inayo baadhi ya mabaki ya
wakiristo wa mwanzo wa Zanzibar.
Baadae ilinunuliwa ardhi nyengine
katika mwaka 1873, ardhi hii ilikuwa karibu na kitovu cha mji ambalo ni jengo
kubwa zima la mjini ambalo liliwahi kuwa uwanja wa soko kongwe, ambapo watumwa
walikuwa wakiuzwa, Mara wito ulitolewa
wa fedha kusaidia ujenzi wa kanisa katika eneo hilo ambao uovu huo wa biashara ya utumwa
ulifanyika. Huu ulikuwa mwanzo kanisa
kuu la kristo (Christ Church Cathedral).
Mwaka uliofuata Ujumbe wa Vyuo Vikuu
kwa Afrika ya Kati (UMCA) walinunua ardhi ya kilimo Mbweni kusini mwa mji
karibu na bahari.
Wamisionari wa Ujumbe wa Vyuo Vikuu
kwa Afrika ya kati (UMCA) walipanga kujaza milki zao kwa majengo ya kidini na
yasiyokuwa ya kidini. Katika mwaka 1882
walianzisha ujenzi wa kanisa la parokia la mtakatifu John (St. John’s Parrish
Church) huko Mbweni. Karibu ya kanisa hilo walijenga kijiji na shamba dogo kwa
ajili ya waliokuwa watumwa zamani na pia walijenga “Makaazi ya watoto wadogo wa
kiume wa kilimani”, ambayo baadae
iligeuzwa skuli ya wasichana. Huko Mbweni walijenga karakana nyingi tu za
elimu amali kwa ajili ya kuwafunza wafuasi wapya wa dini stadi muhimu na baadae
kuwa Chuo cha kidini cha Mtukufu Mark,
ambacho baadae kilihamishiwa kiungani.
Jiwe la msingi la kanisa kuu la
ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati (UMCA Cathedral) liliekwa mwaka 1873
katika siku ya siku kuu ya krismas katika eneo la mjini. Uwanja wa soko kongwe ulianza kujazwa majengo
ya ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati.
“Jumba la Mkunazini” lilijengwa
katika mwaka 1875 na kanisa mara baada ya kujengwa jumba la kunazini
lilihamisha makao makuu yake kutoka Mambo Msiige na kuwa Mkunazini. Zahanati ilijengwa katika mwaka 1877, hatimae
iligeuzwa kuwa hospitali yenye kutoa huduma kamili katika mwaka 1893. Skuli ya
Mtakatifu Mon`ica,
nyumba ya kasisi mkuu na Askofu ilijengwa katika uwanja wa soko kongwe. Jengo hilo la
skuli ya Mtakatifu Monica bado mpaka leo linatumika kama
ni hostel/dahalia Mtukufu Monica.
Mwenye kustahiki sifa ya mafanikio
haya ilikuwa hakika ni kanisa kuu la kristo. Mradi usio wa kibiashara ambao
ulisimamiwa binafsi na Askofu wa tatu wa Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya
Kati Edward Steere, utabakia kuwa moja ya mifano ya kuvutia na bora wa usanifu
majengo ndani ya Afrika uliofanywa na wakiristo wa mwanzo.
Wakati eneo lake lilijazwa
na haiba nzuri ya shinikizo la kidini, ukaribu wake na kijito kidogo chenye
manukato ilisababisha baadhi ya watu kutia wasiwasi juu ya athari zake kwa afya
za wamisionari. Kijito hicho kidogo
ambacho kilitambulika kama ni mfano wa mfereji wa venice huko Italy (Venetian
Canal) kwa maelezo ya kikanisa kilikuwa kiukweli hasa ni topetope zenye kunuka
wakati wa kupwa kwa maji. Eneo hili
liliacha kutoa moshi wenye kunuka na kudhuru katika miaka ya 30 (30’s) baada ya
kijito hicho kufunikwa na barabara, moshi ambao uliendelea kujitokeza kwa
masiku wakati wa kujaa na kupwa maji.
Haiba binafsi ya ushiriki katika
ujenzi wa Daktari Steer unaweza kuonekana na wengi juu ya mabadiliko
aliyoyafanya kwa ramani zilizoletwa kutoka Uingereza na juu ya majaaliwa ya
nguzo za mawe ambazo husimamishwa karibu na nyuma ya ukumbi wa kanisa. Nguzo hizi zilitiwa kipindi ambacho Askofu
alikuwa safarini Tanzania Bara kwa kazi za kanisa. Kwa hivyo, utiaji huo wa nguzo hizo ulikosa
usimamizi wake. Wafanyakazi hao
walizitia nguzo hizo kwa kusimamisha wima kama
alivyoelekeza Askofu lakini kwa bahati mbaya walizigeuza juu chini juu. Baada kurejea Askofu alizichunguza na kuamua
zibakie kama zilivyo,kama zinavyoonekana
leo. Hii ilitokana na azma yake ya
kushindikiza kazi iendelee bila ya kurudi nyuma.
Thamani hasa kubwa ya juhudi zake za
usanifu majengo ni Paa la kanisa kuu.
Akikumbuka matokeo yasiopendeza
wakati akijaribu kufanya matengenezo la paa lililooza la kanisa lake kongwe
la Kiingereza, Askofu Steer alidhamiria kujenga paa kwa kutumia muda mrefu.
Aliamua kujenga paa la zege badala ya
kutumia mbao kwa sababu ya kuhofia mbao hizo kuharibiwa na mchwa na hatari ya
moto na hakuweza kujenga paa hilo kwa kutumia vifaa vya chuma kwasababu hakuwa
na fedha ya kugharimia.Alitumia vifaa vya kienyeji katika ujenzi, alichanganya
saruji na kokoto katika juhudi zake za kujenga paa kubwa lenye upana wa futi
28.5. Ilikuikamilisha kazi hii alitumia
mbea moja ya chombo kilichotengenezwa Uingereza mbacho kililetwa hali ya kuwa
hakijaunganishwa pamoja.
Mashine hii
iliekwa kwenye eneo la ujenzi ikiwa na viringi vilivyotiwa ili kuweza
“kuzungushwa zungushwa kutoka sehemu moja kwenda nyengine pale ambapo kipande
kimoja cha paa kinapomalizika kutiwa”.
Pale ambapo muhimili unapotaka kuondoshwa kundi kubwa la watu ilibidi
kukusanyika pamoja. Mkusanyiko huu wa
watu unakuwa unatweta wakati vifaa vya kujengea jukwaa vinabomolewa, na huachwa
kushangaa na kidogo na kukata tamaa pakiwa hapakutokea lolote. Paa ambalo watu wote hawakutegemea kuchukua muda bila ya kuanguka
sasa limeweza kubakia zaidi ya karne moja/miaka 100.
Mfalme ambae kwa wakati huo alikuwa
Seyyid Barghash alivutiwa sana
na aliamua kutoa saa kubwa, ili kuupamba mnara wa kengele ambao uliwekwa pembe
ya kusini magharibi ya jengo. Kwa bahati
mbaya haikuwepo saa katika ramani ya mwanzo.
Uamuzi wa busara wa kisiasa kupokea na kuiweka zawadi ya Sultani
ulipelekea marekebisho kufanywa juu ya mnara na kuufanya mwembamba na mrefu
zaidi. Uamuzi huo kwa upande mwengine
uliathiri pia zawadi zawadi nyengine ya seti nzuri ya kengele 25, seti za mlio
wa saa ambazo ziliweza kupiga milio mirefu.
Hata hivyo ukubwa na uzito wa
seti hizo ulikuwa hauwezi kubebwa na mnara huo mwembamba. Kengele 13 tu zilitiwa kwenye mnara huo na
kengele zilizobakia zilitawanywa kwa
makanisa mengine na maskuli.
Wakati shughuli zote hizi zikiendelea
katika kisiwa mama, wamisionari kutoka jumuia ya kirafiki ya kidini, the
Quakers walianzisha makaazi karibu kabisa na kisiwa cha Pemba. Quakers walifika Zanzibar
mapema kufikia mwaka 1865, wakati huo walikuja kama
ni waajiriwa wa kampuni za kibiashara za watu wa Magharibi. Lakini Juu ya hivyo, mpaka ilipofikia tarehe 20/Januari/1897 ndipo ujumbe wa kudumu
wa Quaker ulianza mahala panapoitwa Banani ambapo ni karibu na kitivu cha ghuba
ya Chake Chake mwambao wa Magharibi ya Pemba.
Kama
vile ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati, kichocheo cha fedha kwa
ajili ya ujumbe wa Pemba zilitokana na raghba
za vita dhidi ya utumwa alizokuwa nazo kila Quaker. Kuanza hapo tena baadae utumwa ulipigwa
marufuku rasmi katika visiwa hivyi ingawa maisha ya wengi waliokuwa watumwa
kabla hayakubadilika.Kwa wale watumwa waliohama katika maeneo ya wale waliokuwa
wakiwamiliki walikosa makaazi ya kuishi na hofu kubwa ilienea juu ya kuwepo
vikundi visivyofuata utawala wa sheria vikizunguka zunguka sehemu za ma shambani.
Ujumbe wa Quaker, kwa maana hio
ilibidi uwe ujumbe “Chapakazi” ili watumwa walioachiwa huru waweze kupata kazi
na kusoma biashara. Kiongozi wa ujumbe
huu Theodore Bartt bila hata ya kufika Pemba, alisema katika ukumbi wa mkutano
ndani ya Uingereza “Ni jambo mwafaka na sahihi kwake yeye mtu alieachiwa huru
kumiliki shamba kubwa ndani ya Kisiwa hichi na kuonyesha dunia/ulimwengu kwamba
watu walioachiwa huru watafanya kazi kwa bidii na uaminifu na kuwa
wastahamilivu na kujitahidi kujenga maisha yao."
Theodore Buft aliamini kwamba
biashara na ukiristo ilikuwa ndio njia ya uongofu na kuweza kuweza kuelimika.
Watumwa na Waliobadili Dini
Ujumbe wa Quaker kwa Pemba ulikuwa ni
mlolongo wa karibu zaidi wa wakiristo wa uasisi wa “Mji huru” ndani ya Afrika ya Mashariki kwa ajili ya
makaazi ya watumwa walioachiwa huru. Kwa
miaka, jeshi la majini la kifalme walileta makundi kwa makundi watumwa kwa kwa
ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya waliowakamata kutoka bahari kuu. Watu hawa walioachiwa huru walikuwa rahisi
kwao kugeuzwa na kuwa wakiristo na kwa kweli wengi katika wao waligeuka kuwa
wafuasi wa dini ya kikiristo.
Lakini juu ya hivyo, wingi wa
wakiristo hawa wapya na mahitaji yao
maku bwa yalikuwa ni changamoto kwa raslimali na subira ya wafadhili wao. Wakiangalia demografia wamisionari waliona
njia pekee ya kuwahudumikia wakiristo wapya ni kuanzisha chimbuko la Padri wa
kiafrika.
Kwa hivyo wote wakatoliki na
waprotestanti walifanya bidii kuwajumuisha makundi ya kienyeji shughuli na
mambo ya kanisa na hii yote ilipelekea kujua na kufunza mtumishi bora kwa ajili
ya kuendesha shughuli za kidini.
Kwa Zanzibar harakati zote hizi
zilikuwa katika eneo la Kiungani ambapo kwanza ilianzishwa “dahalia kwa watumwa
vijana walioachiwa huru”, na baadae “Chuo cha Mafunzo ya ualimu cha Mtakatifu
Andrew” na baadae “Chuo cha kidini/theolojia” kila moja kati ya hivyo
kilijaribu kuwafunza na kutathmini matokeo ya vijana wa kiafrika. Kiasi cha wanafunzi 50 kwa kipindi kimoja cha
wakati waliishi na kusoma Kiungani.
Mitaala ilisisitiza heshima, elimu, imani na michezo. Wanafunzi wazuri walifanywa kuwa walimu na
wanafunzi bora kuliko wote walifanywa kuwa mapadri.
Jambo moja la kuvutia juu ya michezo
iliyoanzishwa kwa ajili ya wanafunzi wa Kiungani ni kwamba ilifanya baadhi ya
mashindano ya kwanza ya timu mjumuisho ndani ya Afrika. Timu hiyo ya skuli mara walicheza dhidi ya
makundi ya mabaharia wazungu. Mchezo wa
Kriketi ulianzishwa mwanzo katika mpira wa miguu lakini hata hivyo mchezo wa
mpira wa miguu ulipendwa zaidi kwani makundi kwa makundi ya watu walikuwa
wakikusanyika kuangalia mpira wa miguu.
Inaaminika kwamba kanisa iliendeleza michezo kusaidia kuwafunza waafrika
maadili mapya ya jumuia, ufuataji wa sheria, kuweka wakati, kufanyakazi kwa
pamoja na mashirikiano na maofisa husika.
Wanafunzi wa kizanzibari walicheza mechi/michezo hii kwa hamu na raghba
na umahiri wao wa mchezo wa mpira ulijenga mshangao na fadhaa kwa wapinzani
wao. Lakini lisilosahaulika zaidi
walilojifunza ni kwamba wao wanaweza kufanikiwa katika mchezo wowote na sio
mpira wa miguu tu.
Source: http://www.zanzibarhistory.org
No comments:
Post a Comment