MAANDAMANO ya amani yaliyokuwa yameandaliwa na chama cha demokrasia na
maendeleo(chadema) yamegeuka shubiri kwa wakazi wa jiji la Mwanza baada ya
kuibuka mapambano makali baina ya waandamanaji hao na jeshi la polisi mkoani
Mwanza na kusababisha polisi kutumia nguvu kuwatawanya wafuasi wa chama hicho.
Maandamano hayo ya amani ambayo yalianzia katika eneo la Buzuruga nje
kidogo ya jiji la Mwanza yalikuw ayakiongozwa na wabunge Highness Kiwia wa
Ilemela pamoja na Ezekiel Wenje kuelekea katika viwanja vya Furahisha
yalilenga kumshinikiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ernest Ndikilo kutoa barua
zinazodaiwa kuandikwa na ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi kuwarejesha madiwani
watatu waliotimuliwa katika Manispaa ya Ilemela kutokana na kushindwa
kuhudhuria vikao vitatu mfululizo.
Polisi wenye silaha pamoja na askari kanzu walianza kutanda katika
eneo hilo la
Furahisha wakiongozwa na Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa Mwanza
RCO Konyo ambaye alikuwa akitumia gari lenye namba za usajili DK 068EXV aina ya
Toyota Land Cruiser
Maandamano hayo ambayo awali yalionekana kana kwamba yangelimalizika
salama yaliwasili katika viwanja vya Furahisha majira ya saa 5.38 huku
yakiongozwa na gari la polisi lenye namba za usajili za nchi ya Uganda 779
UAG likiwa nimesheheni polisi wenye silaha nzito ikiwa ni pamoja na mabomu ya
machozi na bunduki pamoja na askari kadhaa ambao walikuwa katikati ya
maandamano hayo.
Baada ya maandamano hayo kuwasili katika viwanja vya Furahisha kwa
amani,waandamani hao ambao walikuwa na mabango mbalimbali yaliyosomeka kuwa
‘Matata hatutaki uendelee kuwa Meya wa Ilemela rudia kazi yako ya awali, na
jingine Jaji Sumari tumechoka kuahirisha mara kw amara kesi dhidi ya Matata na
jingine lililosomeka kuwa RD Ndikilo tunahitaji barua za kurejeshwa
kwa madiwani wetu.
Hata hivyo tofauti na ilivyokuwa imetangazwa kuwa maandamano hayo ya
amani yangelipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ernest Ndikilo,hakukuwa na
kiongozi yoyote wa Serikali ambaye alikuwepo uwanjani hapo kupokea maandamano
hayo.
Kufuatia kutoonekana kwa kiongozi yoyote wa Serikali,viongozi wa
chadema pamoja na wabunge wao walikutana kwa faragha kwa dakika kadhaa kwa
ajili ya kujua hatima ya maandamano hayo ambapo Mbunge wa Nyamagana Ezekiel
Wenje alipanda jukwaani saa 6.45 na kuwaeleza maelfu ya waandamanaji kuwa
wameamua kumtuma Mbunge wa Ilemela Highnes Kiwia kwenda ofisini kwa Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza kuchukua majibu kwa ajili ya kuwaletea wananchi walioandamana
juu ya hatima ya madiwani hao.
Hata hivyo saa moja baadae Mbunge huyo alisimama jukwani na
wakuwaeleza waandamani hao kuwa simu ya Mbunge Kiwia ilikuwa haipatikani hivyo
kuwataka kuandamana kwenda kwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza kujua kulikoni na hapo
ndipo hali ya hewa ilipochafuka.
Jeshi la polisi baada ya kuona wandamanaji hao wameanza kuelekea
katika ofisi za Mkuu wa mkoa liliwataka kutawanyika ambapo waandamanaji hao
walikaidi ndipo jeshi la polisi lilipoamua kutumia mabomu ya machozi
kuwatawanya wafuasi hao.
Vurugu hizo ambazo zilianza majira ya saa 7.30 zilisababisha kufungwa
kwa baadhi ya barabara kutokana na waandamanji hao kuweka vizuizi vya mawe na
kuchoma matairi,ambapo pia maduka na ofisi mbalimbali zililazimika kufungwa kwa
muda kupisha vurugu hizo.
Baadhi ya wananchi ambao walikuwa wakitumia usafiri wa umma
walionekana wakishuka kupitia katika madirisha ya magari hayo na kukimbia kwa
hofu ya kujeruhiwa na mabomu pamoja na mawe ambayo yalikuwa yakirushwa na
waandamanji hao kwa jeshi la polisi.
MKUU WA MKOA WA MWANZA ALONGA.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza akizungumza na Mbunge Kiwia pamoja na viongozi
wa chadema ofisini kwake alisema kuwa ameshangazwa
na uvumi huo kuwa ofisi yake imekalia barua a kurejeshwa kwa madiwani
Abubakar Kapera(Nyamanoro),Dan Kahungu(Kirumba) pamoja na Marietha
Chenyenge(Ilemela).
RC Ndikilo alisema kuwa Serikali imekuwa ikifanya kazi zake kwa
maandishi na sio kwa kufuata maneno ya mtaani na kueleza kuwa hana barua yoyote
toka ofisi ya Waziri Mkuu inayomualifu kuhusu kuwarejesha madiwani hao baada ya
kukata rufaa.
“Hata Mbunge kuna siku ulinipigia simu ukiniuliza juu ya kuwepo kwa
barua hizo name nilikujibu kuwa kwa kuwa uko hapo Bungeni Dodoma ambapo pia
kuna ofisi ya Waziri Mkuu nilikujibu kuwa ni muhimu ukawaona viongozi wakuu wa
Tamisemi ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu,pia nilikushauri kuwa wakupe japo
nakala ya barua hiyo”,alisema RC Ndikilo.
“Lakini cha kushangaza nimekuwa nikisikia maneno ya ajabu kuwa
nimeficha barua za madiwani hao,ikumbukwe kuwa madiwnai hao hawakukata rufaa
kwangu bali walikata rufaa ngazi ya juu kabisa,ili kukata mzizi wa fitina
naomba kati ya tarehe 26 hadi 27 wewe Mbunge pamoja na mimi twende TAMISEMI
kukutana na viongozi ili kukata mzizi wa fitina na tuje tuwaeleze wananchi
ukweli uliopo”,alisema RC Ndikilo.
Kuhusu suala la Meya Henry Matata kutoondolewa madarakani RC Ndikilo
alisema kuwa hawezi kulizungumzia suala hilo
kw akuheshimu mamlaka ya mahakama na kuwataka chadema kuvuta subira hadi pale
mahakama itakapotoa maamuzi yake.
KAULI YA MBUNGE KIWIA.
Akizungumza katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Kiwia alisema kuwa
waliamua kuitisha maandamano hayo kutokana na kuelezwa na Waziri Hawa Ghasia
kuwa tayari barua hizo zimeishatumwa mkoani Mwanza.
“Mheshimiwa Mkuu wa mkoa hawa madiwani waliosimamishw ani wawakilishi
wa wananchi,wamekaa nje kwa miezi saba sasa na uchaguzi wa Meya haukuwa halali
ndio maana tuliamua kuitisha maandamano kwa ajili ya kuhakikisha madiwani hawa
wanarejeshwa.
RPC MANGU.
Akizungumza kwa simu juu ya kutokea kwa vurugu zilizosababisha kupigw
akwa mabomu ya machozi,Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ernest Mangu alisema
kuwa polisi walifanikiwa kudhibiti vurugu hizo na hadi sasa hawezi kusema ni
wananchi wangapi ambao walikamatwa kuhusu vurugu hizo.
WANANCHI WAWALAUMU VIONGOZI NA WANASIASA NA KUWAFIFU POLISI.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na Mtanzania juu ya vurugu zilizotokea
waliwaonyoshea kidole wanasiasa pamoja na viongozi wa mkoa wa Mwanza kutokana
na kushindwa kusema ukweli juu ya tukio hilo.
Baadhi walisikika wakisema kuwa kama barua zipo kweli madiwani hao
wanapashwa kupewa na kama ahzipo basi
walioeneza maneno hayo wachukuliwe hatua kali kutokana na uchochezi.
Wananchi hao pia walilipongeza jeshi la polisi kutokana na kutumia busara badala ya nguvu kuhakikisha maandamano hayo yanakuwa ya amani.
SOURCE: http://paparaziblog.blogspot.com
No comments:
Post a Comment