Bi. Arodia Gebasaki
ambaye ni mjane akisimulia jinsi mila ya kutakasa wajane inavyofanyika kwa
mwandishi wa makala haya (hayupo pichani) ambapo yeye alikataa kufanyiwa mila
hiyo na hakuna madhara yoyote aliyopata tangu kufiwa na mume wake, miaka 14
iliyopita
Baadhi ya wajane
wakiwa katika picha ya pamoja na mwandishi wa makala haya baada ya kufanya
mahojiano kuhusu mila ya kutakasa wajane wilayani Ukerewe, Mwanza. Wajane hao
wameipiga vita mila hiyo kutokana na kumdhalilisha mwanamke.
MWANDISHI Reuben Kagaruki
"Udhalilishaji
huu uliojificha katika mila inayoitwa Okusomboka kwa Wakerewe ni tendo ambalo
hufanyika kwa maana ya kuhitimisha uhusiano wa ndoa kati ya mume na mke
aliyefiwa. Mila hiyo huhitaji uhusiano huo uhitimiswe hivyo sababu ulianzishwa
kwa tendo la ndoa.BIBI a l i b a kwa , mama
akabakwa, dada amebakwa na mke wangu atabakwa nitakapofariki.”
Huo ndiyo uhalifu mkubwa uliojificha kwenye mila ya
Okusomboka (kutakasa) kwa wakazi wa Ukerewe hasa kwa Wakara na Wajita.Kwa
Wakerewe ubakaji ni jambo la kawaida na unatukuzwa kwa mikono miwili kupitia
mila ya Okusombaka.
Hayo ndiyo maisha ya kawaida kwa wakazi wa Ukerewe mkoani
Mwanza wanaotukuza ubakaji, mbakaji anapomaliza tendo hilo, wakati mwingine anashangiliwa kwa
kupigiwa vigelegele na akina mama akionekana shujaa wa kuondoa watu mikosi
kupitia ubakaji, ingawa wao hutafsiri kuwa wanasomboka.
Ubakaji huo kupitia mila ya Okusomboka ni sehemu ya maisha
ya kawaida kwa wakazi wa Ukerewe na unaheshimiwa kiasi kwamba wale wanaokataa
kubakwa wanatengwa na kunyooshewa vidole kila wanapopita.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili wilayani Ukerewe Mkoa wa
Mwanza juu ya mila ya Okusomboka (utakasaji) umebainisha vitendo vya ubakaji
vimekuwa vikitendeka tangu enzi na enzi na kuingia katika karne hii ya sayansi na
teknolojia.
Ambapo
ubakaji huo, unalenga wanawake wajane na unafanyika siku ya nne ya matanga
tangu kutokea kifo cha mwanaume ndani ya familia.Bila kujali uchungu anaokuwa
nao mjane wa kupoteza mume wake, anatafutiwa mbakaji (Omwesya-yaani mtakasaji)
ambaye anakodiwa na kulipwa ujira ili kutekeleza kitendo hicho cha kubaka
mjane, ambacho kwa Ukerewe ni cha heshima, katika kuhitimisha uhusiano kati ya
mume aliyekufa na mjane aliyebaki.
Ingawa
sheria ya Makosa ya Kujamiiana ya Mwaka 1998 inatoa adhabu kali kwa watu
wanaopatikana na hatia ya makosa ya ubakaji, kwa Ukerewe hawajui kama Okusomboka ni kubaka, hivyo kukiuka wazi wazi sheria
hiyo inayotolewa kwa watu wanaofanya vitendo hivyo.
Ubakaji
unafanyika kwa uwazi na wameenda mbele zaidi kwani kuna watu maalumu ambao
wanalipwa fedha na wakati mwingine hata mifugo kwa ajili ya kuwabaka wanawake
wanaofiwa na waume zao kwa hoja kwamba wanatimiza sharti la mila hiyo.
Mbakaji
kabla ya kuanza kitendo hicho, huwa anaandaliwa chakula maalumu ikiwemo pombe
ambayo huwa anakunywa na kuchangamka na hapo ndipo anaaza kubaka.
Kutokana
na hali hiyo wanawake wengi walioolewa wilayani Ukerewe ni wabakwaji watarajiwa
na wale watakao kataa kubakwa, basi wajiandae kutengwa na ndugu, kunyooshewa
vidole na jamii inayowazunguka na mali za marehemu waume zao
kutotolewa urithi.
Pia,
mjane anayekataa kutakaswa ajiandae kutopata mwanaume wa kumuoa.
Vi kwa
z o h i v y o , n d i v y o vinavyowashinikiza wakubali kubakwa na watu maalumu
ambao hukodiwa kwa fedha au kulipwa mifungo kwa ajili ya kubaka wajane.
Katika
mila hii, mwanamke analazimishwa kufanya tendo la ndoa bila ridhaa yake tena na
mtu asiyemfahamu na haandaliwi kwa namna yoyote ile kwa ajili ya tendo hilo.
Wakati
kwenye majumba ya utakasaji unafanyikwa kwa njia ya maombi, kwa Ukerewe
unafanyika kwa njia ya ubakaji.
Okusomboka
ni tendo la ndoa linalohusisha watu wawili, mjane ambaye amefiwa na mume au mke
na mwingine ambaye yupo kwa ajili ya kazi hiyo.
Mfano
leo hii ikitokea mwanamke akafiwa na mume wake, baada ya mazishi yanafanyika
matanga ambapo siku ya nne ya matanga, anakodiwa mtu kutoka miongoni mwa watu
wanaokodishwa kwa ajili ya kutakasa mjane na kufanya naye tendo la ndoa tena
bila hiari ya mjane.
Ubakaji
uliojificha kwenye mila ya Okusomboka (kutakasa) kwa Wakerewe ni tendo ambalo
linafanyika kwa maana ya kuhitimisha uhusiano wa ndoa kati ya mume na mke
ulioanzishwa kwa tendo la ndoa, hivyo ni lazima uhusiano huo uhitimishwe kwa
tendo hilo kutokana na mmoja wa wanandoa kuwa amefariki.
Utakasaji
huo unafanyika kwa pande zote yaani mwanake na kwa mwanaume, lakini
unatofautiana mazingira unapofanyika.
Mfano,
mwanamke anapofiwa na mume wake anakodishwa mtu maalumu wa kufanya naye tendo
la ndoa na hapo kunakuwa hakuna maridhiano yoyote kati ya mtakaswaji na
mtakasaji, bali maridhiano yanatokana na kile anacholipwa mtakasaji ndipo
anafanya tendo hilo.
Lakini,
mwanaume anapofiwa na mke wake anaenda mwenyewe mtaani kutafuta mwanamke wa
kufanya naye tendo la ndoa wakati mwingine akisindikizwa na wapambe
watakaothibitisha kwamba, alipata mwanamke na kufanya naye tendo la ndoa, hivyo
anakuwa ametakasika.
Wanafanya
hivyo, kwa kuamini kwamba, marehemu wakati anafikwa na mauti hakupata fursa ya
mwisho ya kufanya tendo la ndoa hilo
na mwenzi wake.
Kwa
msingi huo, wanafanya hivyo kama ishara ya
kuhitimisha uhusiano wa wanandoa hao, yaani marehemu na yule aliyebaki hai.
Wakerewe
wanaamini kuwa, mjane au mgane akishatakaswa ile mikosi yote iliyosababisha
kifo cha marehemu inakuwa imeondolewa yote.
Pia
wanafanya hivyo kwa kuamini kwamba, marehemu wakati anafikwa na mauti hakupata
fursa ya mwisho ya kufanya tendo hilo
na mwenzi wake.
Hiyo
inakuwa ni ishara ya kumalizika kwa uhusiano wa wanandoa hao, yaani marehemu na
yule aliyebaki hai.
UBAKAJI
WENYEWE
Mmoja
wa wazee anayefahamu mila hiyo ambaye pia aliwahi kufanyiwa mila hiyo, Juma
Mtallo (83) mkazi wa Nkilizi katika Kijiji cha Mmakeke wilayani Ukerewe,
anasema pindi mwanamke anapofiwa na mumewe, kama kawaida yanafanyika matanga
kwa siku kati ya tano na saba kulingana na uwezo wa wafiwa.
Katika
kipindi hicho, mjane huyo anatakiwa kuhudumiwa na kuandaliwa chakula na mtu
aliyewahi kufiwa na mwenzi wake.
“Anakuwa
ndani ya nyumba amefunikwa nguo na wanaoenda kumsalimia na kumhudumia ikiwa ni
pamoja na kumpikia chakula ni wale waliowahi kufiwa,” anasema Mtallo.
Anasema,
kwa kipindi hicho anakuwa hajaoga. “Siku ya nne ndipo wanaanza taratibu za
kumuogesha na akishamaliza ndipo anapelekwa kwa mbakaji (mtakasaji).”
Anaongeza
kwamba baada ya mtakasaji kumaliza kazi hiyo, anaondoka kwa majigambo na wakati
mwingine akiimba; “Wanaume wafe wanawake wabaki…wanaume wafe wanawake wabaki,”
anasema huku akiongeza huwa anaimba hivyo ili wanaume wazidi kufa na yeye azidi
kupata kazi ya kubaka wajane.
SIKU YA
UBAKAJI
Kwa
mujibu wa mila hiyo, siku ya kubaka, mbakaji huwa anaandaliwa chakula kizuri
pamoja na vinywaji hasa pombe kwa gharama za familia inayotakaswa.
Mmoja
wa wanawake waliowahi kutakaswa, Anna Sebastiane mkazi wa Tarafa ya Ukara Kata
ya Bukungu, wilayani Ukerewe anasema, siku mtakasaji anapoenda kutakasa mjane,
anapokelewa kwa heshima kubwa.
Anaeleza
kwamba wakati mwingine anaweza kumwambia mtakaswaji; “Hebu cheza nione kama unaweza,” anasema yaani aoneshe umahiri wa kutikisa
nyonga wakati wa tendo la ndoa.
Anafafanua
kwamba, endapo ataona mjane hawezi kutikisa nyonga, anaongeza gharama. Mfano
endapo aliwatoza fedha basi atapenda aongezewe kiasi atakachoona kinamfaa au
kama ni mifugo kama vile mbuzi, atataka
aongezewe mwingine kwa jinsi atakavyoona inafaa.
Hata
pale asipovutiwa sura ya mtakaswaji, mtakasaji anapandisha gharama kwa jinsi
atakavyoona inafaa.
Anasema,
endapo utakasaji utafanyika nyumbani kwa marehemu basi ndani ya nyumba inabidi
wawepo watoto wake ambao hawajaolewa.
“Wakati
utakasaji unafanyika (ubakaji) watoto wanakuwa wanasikia jinsi Omwezya
(mtakasaji) anavyonguruma (akitoa maelekezo kwa sauti nene akimwelekeza mjane
jinsi anavyotaka alale au namna ambavyo anataka atingishe nyonga yake) na hapo
kitanda kinachokuwa kinatumika ni cha marehemu,” anasema Sebastiane.
Anapoulizwa
kama watoto wanasikia hiyo sauti? Sebastiane anacheka kwanza huku akivuta
pumzi, kisha anasema;
“Sio
watoto peke yake, hata wanaokuwa nje wanafahamu kinachoendelea …si unaona hali
ya nyumba zetu (mbovu kiasi kwamba nyingi hazina faragha). Anasema anakuwa
anahimiza mtakaswaji atingishe nyonga ili apate raha.
“Watakasaji
wengine, hawakuwa na staha na tendo la ndoa, kwani walipokaribia mshindo (kutoa
mbegu za uzazi) walipiga kelele kwa kunogewa na uhondo wakati huo huo
akiashiria kwamba kazi aliyopewa amehitimisha,” anasema na kuongeza kuwa
akishamaliza anavaa nguo na kutoka nje ya nyumba kwa mbwe mbwe kisha kulipwa
chake.
Anasema,
watakasaji wengine waliondoka wakiimba; “wanaume wafe wanawake wabaki..wanaume
wa f e wa n awa k e wa b a k i . ” Anasema hiyo kwa kufurahia kile
walicholipwa. “Wakati anaondoka anapigiwa vigelegele na akina mama kwa
kufurahia kuhitimisha mila hiyo…mila hii unaweza kuiona ni mbaya, lakini
yakishakufika utaona umuhimu wake,” anasema Sebastiane.
Hata
hivyo, anasema: “ Mila hii (Okusomboka) ni aibu kwa watoto wanaokuwa ndani ya
nyumba wakisikiliza mama yao
akitakaswa, huku akihimizwa atingishe nyonga… tendo la ndoa linahitaji faragha,
lakini utakasaji hauna faragha na unamdhalilisha mwanamke,” anasema na kuongeza
kuwa ni jambo la aibu ndiyo maana tendo la ndoa linahitaji faragha.
Sebastiane
anapoulizwa kama mtakasaji anatumia kondomu ili kujikinga na magonjwa, anasema
jambo hilo
halipo.
Pia
anasema, mtakasaji na mtakaswaji wanatakiwa wafanye tendo moja la ndoa (yaani
mshindo mmoja) na wasifanye tena tendo hilo
maishani mwao, endapo wakirudia watakuwa wamekiuka sharti la mila hiyo hivyo
mikosi inaweza kurudia familia ya mjane.
“Kwa
hiyo atalazimika atakaswe (abakwe) upya na mtakasaji mwingine, vinginevyo
wanaamini kuwa familia yake itaendelea kuandamwa na mikosi,” anasema .
Anataja
mikosi hiyo kuwa ni pamoja na familia kuandamwa na vifo na kuugua mara kwa
mara.
MASHAHIDI
Mashahidi
wanaoshuhudia tukio hilo, wanasema wanakuwepo
kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tendo hilo
limefanyika, ili kuondoa wasiwasi wa wajane kudanganya.
Mjane
mwingine, Arodia Gabaseki (64) mkazi wa Kata ya Ulagala, Tarafa ya Masonga
wilayani Ukerewe anasema mashuhuda wanakuwa nje katika mazingira ambayo
watakuwa na uhakika kuwa tendo hilo
linafanyika.
Anasema
kwamba, kutokana na wajane kuogopa mikosi, lazima wakubali na kwamba mgurumo wa
mtakasaji nao kwa wakati mwingine ni ishara nzuri kwao.
Anaeleza
kwamba, mara baada ya kutakaswa anarejea nyumbani akiwa ameinamisha kichwa
chini na kupokewa kwa furaha na wanandugu waliopo kwenye matanga, kwa kuwa
wanaamini kuwa uhusiano kati ya mjane na marehemu umehitimishwa na hakuna
matatizo yoyote yanayoweza kuwapata.
SIFA YA
MTAKASAJI
Ofisa
wa Taasisi ya Kuboresha Mila na Desturi katika Jamii ya Ukerewe (KUMIDEU),
taasisi ambayo inajihusisha kutoa elimu ya kutokomeza mila ya kutakasa wajane,
Musiba Kakulu anasema mtakasaji ni mtu anayeonekana hakubaliki ndani ya jamii
kutokana na matendo hayo.
Anasema,
watakasaji wengi ni walevi, wachafu, wasiokuwa na wanawake na mara nyingi
walitegemea kuendesha maisha yao
kwa kutegemea malipo wanayopata kwa njia ya utakasaji.
“Kutokana
na umuhimu wa mila ya kutakasa, mtakasaji (Omwezya) anakuwa hana umuhimu ndani
ya jamii,” anasema Kakulu. Sifa nyingine anasema ni mtu anayejua dawa na
anayependa kusimamia mila na desturi.
Pamoja
na kuwa na hali hiyo, lakini thamani yao
inaonekana pale walipohitajika kutakasa, kwani watu wenye heshima zao ndani ya
jamii hawakubali kabisa kutakasa watu ambao tena haijulikani wenzi wao
wamefariki kwa magonjwa gani.
“Mtakaswaji
kama ni bibi kikongwe, anapata shida kwani mtakasaji anatoza gharama kubwa kama vile ng’ombe wakati uwezo anakuwa hana, lakini ndugu
lazima wachangishane ili wampate ng’ombe huyo,” anasema.
Anasema,
wakati mwingine mtakasaji anapotakiwa kwenda kwa mtakaswaji na ni mzee sana analazimika
atafutiwe usafiri hadi nyumbani kwa mjan
CHANZO: Gazeti la Majira
No comments:
Post a Comment