Rais Bashar al-Assad akisalimiana na wanajeshi wake mjini Damascus hivi karibuni.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry ametoa matamshi yanayoashiria mashambulizi dhidi ya Assad yako njiani.
Kufuatia shambulizi la silaha za sumu
lililoua mamia nchini Syria, yaonekana muda wa kutafuta suluhu ya muafaka
umekwisha. Marekani inaona msitari mwekundu umevukwa, na inapima uwezekano wa
kuingilia kijeshi.
Baada ya kutokea shambulizi
linalodhaniwa kuwa la kemikali, ambalo liliwauwa mamia ya raia na kujeruhi
zaidi ya 3000 nchini Syria kwa mujibu wa shirika la misaada la madaktari wasio
na mipaka, mataifa mengi ya magharibi na hasa Marekani, yanaaamini kuwa rais
Bashar al-Assad ndiye anawajibika kwa shambulizi hilo. Kwa sababu kwa miezi
kadhaa rais wa Marekani, Barack Obama, alionya kuwa matumizi ya silaha za
kemikali yatamaanisha kuwa msitari mwekundu umevukwa, katika mazingira haya,
laazima utawala wa Assad uchukuliwe hatua nzito. Kwa mujibu wa vyanzo vya
Usalama vya Marekani, Ikulu ya mjini Washington inajadili njia tatu za
kuchukuwa.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry ametoa matamshi yanayoashiria mashambulizi dhidi ya Assad yako njiani.
Eneo la kuzuiwa kuruka ndege linaweza
kuwasaidia pakubwa waasi. Eneo la kuzuiwa kuruka ndege linaweza kuwasaidia
pakubwa waasi.
Eneo lisiloruhusiwa ndege kuruka
Njia ya kwanza ni ku
weka eneo lisiloruhusiwa ndege kuruka
nchini Syria, hii ikimaanisha kuwa Wamarekani watazipiga marufuku ndege na
helikopta za utawala katika baadhi ya maeneo. Hii itamaanisha kuwa vikosi vya
Assad havitaweza tena kuwashambulia waasi kupitia angani. Hans-Joachim Schmidt,
kutoka taasisi ya amani na utatuzi wa migogoro ya Hessian, anasema hatua hii
ingekuwa ya msaada mkubwa kwa waasi kwa sababu "Assad hangeweza
kuwashambulia waasi kwa kutumia helikopta na ndege zake za kivita. Hii
ingewanufaisha moja kwa moja waasi."
Lakini Paul Rogers, mtaalamu wa
masuala ya usalama kutoka shirika la ushauri la Oxford Reseach Group la
Uingereza, anasema Marekani laazima izime mifumo ya ulinzi wa angani ya Syria,
jambo ambalo anasema litakuwa ghali na la hatari sana kwa kuzingatia kuwa Urusi
iliahidi kuipatia Syria mitambo ya kisasa. Juu ya wasiwasi huo, Hans-Joachim
Schmidt anasema ikiwa kweli Urusi imekwisha iuzia Syria mitambo hiyo ya kisasa,
basi Wamarekani watapata taabu sana. Lakini anasema haoni uwezekano mkubwa kwa
Marekani kutumia mkakati huu, kwa sababu utawavuta zaidi katika mgogoro huu,
kitu ambacho serikali ya Marekani haitaki. Wakati huo huo, kanda isiyoruhusiwa
kuruka ndege laazima iidhinishwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, na
huko Urusi na China bila shaka zitatumia kura ya turufu kuizuia.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani
John Kerry ametoa matamshi yanayoashiria mashambulizi dhidi ya Assad yako
njiani. Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry ametoa matamshi
yanayoashiria mashambulizi dhidi ya Assad yako njiani.
Mashambulizi dhidi ya maeneo ya
kimkakati
Njia nyingine ni kushambulia maeneo
ya kimkakati kwa makombora na maroketi kama vile viwanja na njia za kurukia
ndege, na hivyo kudhoofisha uwezo wa jeshi la angani la Syria. Marekani ina
meli kadhaa za kivita na nyambizi katika bahari ya Mediterannean, ambazo
zinaweza kutumiwa kutekeleza mashambulizi ya namna hii na kufanya vigumu kwa
ndege kuruka na kutua.
Lakini uharibifu kwa njia za ndege
unaweza kukarabatiwa haraka. Schmidt anaiona njia hii kuwa ndiyo yenye
uwezekano mkubwa zaidi wa kutumiwa, licha ya ukweli kuwa nayo itahitaji
kuidhinishwa na baraza la usalama. "Wamarekani hawataki kujiingiza moja
kwa moja katika mgogoro huu, hivyo shambulio la kijeshi lingekuwa ishara yenye
ufanisi, japokuwa yenye mipaka, ya kuzuia matumizi zaidi ya silaha za
kemikali," anafafanua mtafiti wa amani na utatuzi wa migoro Hans-Joachim
Schmidt.
Kuwapatia waasi silaha
Njia ya tatu inaweza kuwa kuwapatia
silaha waasi. Hadi sasa Marekani haijawapatia msaada wa silaha waasi,
ukiachilia mbali misaada ya kawaida kama vile vifaa vya tiba. Lakini Rogers
anasema waasi wamekuwa wakipokea vifaa vya kijeshi kutoka Saudi Arabia na Umoja
wa falme za Kiarabu kupitia Uturuki na Jordan. Lakini anasisitiza kuwa
uwezekano wa waasi kupatiwa silaha moja kwa moja na Marekani ni mdogo sana, kwa
sababu watahitaji kupewa mazoezi kwanza kabla hilo halijafanyika. Hofu nyingine
kuhusiana na hili, ni silaha hizo kuangukia mikoni mwa kundi lenye itakadi kali
la Al-Nusra Front.
Rais Bashar al-Assad akisalimiana na
wanajeshi wake mjini Damascus hivi karibuni. Rais Bashar al-Assad akisalimiana
na wanajeshi wake mjini Damascus hivi karibuni.
Na diplomasia je?
Lakini Uingiliaji wa tahadhari bado
unabaki kuwa uingiliaji, na kwa hivyo Marekani bado inasita kufanya hivyo, kwa
kuzingatia madhara yake. Tayari rais Bashar al-Assad ameonya kuwa hatua yoyote
ya kuingilia kati kijeshi itasababisha moto utakaoizingira kanda nzima ya
mashariki ya kati. Iran nayo inaweza kuliimarisha kundi la Hezbollah dhidi ya
Israel na kundi la Taliban linaweza kuzidisha mashambulizi dhidi ya maslahi ya
Marekani.
Schmidt kwa hivyo anapendekeza njia
ya nne ambayo haizungumzwi katika vyombo vya habari kwa sasa: Shinikizo la
diplomasia. Hata hivyo, mtaalamu huyo anahisi kuwa uamuzi wa kuishambulia Syria
kijeshi umekwisha chukuliwa na kinachosubiriwa ni lini na vipi. Kinachoonekana
sasa ni kwamba Marekani inatafuta washirika katika operesheni hii.
Mwandishi: Jansen Klaus
Tafsiri: Iddi Ismail Ssessanga
Mhariri: Josephat Charo
Chanzo: Dw/de/swahil
No comments:
Post a Comment