Na Chiwambo Ausi,
Zengwe la kumwagia Tindikali watu wa
aina Mbalimbali Tanzania
sasa limekuwa janga la kitaifa na ni wimbo wa Taifa kwa sasa. Huko nyuma tulitumia
kwa shughuli za Kimaabara na mahospitalini lakini leo matumizi ya tindikali
yamegeuzwa na kuwa silaha ya kuwaalibu watu sura zao, kuua kwa kutumia
tindikali au kumwagia tindikali. Kwa sasa tindikali Tanzania imegeuzwa kuwa silaha
dhidi ya watu fulani.
Katika miaka ya hivi karibuni Tanzania
tumeshudia namna watu wa aina Mbalimbali walivyomwagiwa Tindikali pasipo
kukamatwa mtu yeyote yule. Kwa mfano, hivi majuzi Wazungu wawili kutoka
Wiingereza wamemwagiwa tindikali na watu wasiofahamika. Pia katika chaguzi
mbalimbali nchini ikiwemo ule wa Igunga ulitawaliwa na mada ya Tindikali.
Pia Waandishi wawili wa Gazeti la
Kila wiki la Mwanahalisi (Lililofungiwa na serikali) akiwemo Saed Kubenea na
mwenzake mmoja walimwagiwa Tindikali wakiwa ofisini. Watanzania Tujiulize,
kwanini haya yanatokea? Kwanini wahalifu hao hawakamatwi? Je huu ni uzembe wa
nani? Serikali haina budi kutafuta chanzo cha tatizo na kuzuia moja kwa moja.
Kwa miaka michache iliyopita
Tindikali ilikuwa ni suala la kitaifa tu, ila kwa sasa wamevuka mipaka na
kuwamwagia Tindikali hadi Wageni waliofika Tanzania kutoka nchi nyingine.
Watanzania tulaani Vikali sana
sulala hili kwani ni aibu ya kitaifa.
Mwandishi wa RFI Kiswahili Ndugu
Emmanuel Richard Makundi alilipoti taarifa ifuatayo; Raia hao wawili wasichana
wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 wanaaminika kuwa walikuwa wakifanya kazi
za kujitolea visiwani humo na kwamba tukio hili ni la kwanza kufanywa kwa raia
wa Kigeni.
Kaimu kamanda wa Polisi Visiwani Zanzibar, Mkadam Khamis
amewaambia waandishi wa habari visiwani humo kuwa watu wawili waliokuwa kwenye
pikipiki waliwakaribia wasichana hao na kisha kuwamwagia tindi kali.
Wizara ya mambo ya nje ya Tanzania
imekiri kuwa na taarifa hizo na kwamba wanafanya kila linalowezekana
kuhakikisha raia hao wanapatiwa matibabu ya haraka kuwanusuru na madhara zaidi
ya acid hiyo.
Polisi wanasema bado wanaendelea na
uchunguzi na kwamba mpaka sasa watu waliohusika na shambulio hilo hawajafahamika ila uchunguzi bado
unaendelea na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano kubaini wahusika.
Wizara ya mambo ya nje imesema kuwa
zaidi ya raia elfu 75 wa Uingereza ambao huetembeala Tanzania kila mwaka, hivi karibuni
kumekuwa na mashambulizi yakuwalenga raia wakigeni jambo ambalo linahatarisha
usalama wao.
Wizara hiyo imeongeza kuwa kumekuwa
na matukio ya uporaji wa mizigo ya raia wa kigeni hasa kwenye baadhi ya mitaa
ya jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine hali ambayo hivi sasa inaonekana
kuota mizizi.
Hivi Karibuni watu wasiofahamika
walimwagia tindi kali mufti msaidizi wa Zanzibar
pamoja na kumpiga risasi padri wa kanisa Katoliki.”
Ni matumaini yangu kuwa serikali
itasikiliza kilio hiki na kuchukua hatua stahiki ili lisije kujirudia na uwe
wimbo uliopita na muda “The Song of the past”.
No comments:
Post a Comment