Friday, August 9, 2013

JENGO LA GHOROFA LA UDONGO KWA KUTUMIA NGUZO POLI HUKO WILAYANI TUNDURU, VIJIJINI

                       PICHA HII IMECHUKULIWA KOTOKA facebook Profile ya Hassan Namlia

Kwa Mara ya Mwisho Jengo kama hili nililiona Tunduru kijiji cha Angalia. Pia Azimio lilikuwepo miaka mingi iliyopita katika tarafa ya Lukumbule. Hii ni technologia ya Watu Wa kusini hasa maeneo ya wilaya ya Tunduru. Usalama wa hizi nyumba ni mdogo sana kwani hujengwa kwa kutumia miti poli ambayo uwezo wake wa kudumu haifiki kumi. Kama unavyoliona hilo jengo na miti yake kama nguzo za nyumba.

Hizi nyumba kwa maonyesho zinafaa lakini si kwa ajili ya kuweka makazi ya kudumu kwa sababu hazina vigezo vya kitaalamu katika ujenzi wake na ni rahisi sana kuporomoka kuto pale mvua zinapoongezeka na matokeo yake ni kuathiri maisha ya binadamu.


No comments: