Mbali na viongozi hao waliowahi kuwa
wenyeviti wa CCM, pia watakuwapo, Salmin Amour, Amani Abedi Karume, John
Malecela na Pius Msekwa waliowahi kushika wadhifa wa Makamu wa Mwenyekiti wa Zanzibar na Tanzania
Bara.
Wazo la kuunda baraza la wazee
lilitolewa Aprili, 2011 katika kikao cha NEC baada ya wazee kuombwa
kutohudhuriwa vikao vya CC kutokana na kuhitaji safari ndefu za mara kwa mara
wakati wana umri mkubwa.
Kwa ombi hilo, NEC iliridhia mabadiliko hayo ya katiba
wakati wa kikao chake kilichoketi Februari 12, 2012.
Madiwani wa Bukoba kikaangoni
Hatima ya madiwani wanane waliofutiwa
uanachama huko mkoani Kagera itafahamika wikiendi hii wakati CC itakapokutana
leo. Baada ya CC, kikao cha NEC kitafanyika kesho na keshokutwa.
Nape alisema suala la madiwani wa
Bukoba litakuwa miongoni mwa ajenda za kikao cha CC.
Halmashauri ya CCM, Mkoa wa Kagera
hivi karibuni iliwafukuza uanachama madiwani hao kutokana na kushirikiana na
wale wa Chadema na CUF kupinga uongozi wa Meya wa Mji wa Bukoba, Anatory Amani.
Waliofukuzwa ni Richard Gaspar
(Miembeni ), Murungi Kichwabuta (Viti Maalumu), Alexander Ngalinda ambaye pia
ni Naibu Meya (Buhembe), Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya
(Kashai), Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga), Robert Katunzi (Hamugembe), Samwel
Ruhangisa (Kitendaguro) na Dauda Kalumuna (Ijuganyondo).
Baada ya kufukuzwa, Sekretarieti ya
CCM ilitoa taarifa kupinga hatua hiyo ikisema Halmashauri ya Mkoa wa Kagera
haikuwa na madaraka ya kuwatimua madiwani hao.
Ajenda nyingine
Nape alisema ajenda nyingine za CC
zitakuwa kujadili maoni ya wanaCCM juu ya rasimu ya Katiba, hali ya kisiasa na
masuala ya utumishi. Alisema NEC itajadili ajenda moja tu ya maoni ya rasimu ya
Katiba Mpya.
Source: Mwananchi
No comments:
Post a Comment