Na John Nditi wa Globu ya Jamii,
Morogoro.
KATIBU wa Jumuiya ya Kiislamu nchini
, Shekhe Ponda Issa Ponda, alijikuta katika wakati mgumu baada ya kuumizwa na
kitu kinachodhaniwa kuwa ni risasi kwenye bega lake la kulia wakati akiekelea
katika Msikiti wa Mungu Mmoja Dini Moja wa Mjini Morogoro baada ya kumalizika
kwa kongamano ya Dini ya Kiislamu.
Mkasa huyo ulitokea Jumamosi Augosti
10, mwaka huu majira ya saa 12: 15 za jioni eneo la barabara ya Tumbaku karibu
na Fire, mara baada ya kumaliza kwa Kongamano la Kiislamu lililofanyika kwenye
uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege, Kata ya Saba Saba , Manispaa ya
Morogoro.
Shekhe Ponda alishiriki katika Kongamano hilo lililoandaliwa na
Umoja wa Wahadhiri wa Dini ya Kiislamu Mkoani Morogoro na kufanyika siku ya Idd
Pili kuanza saa nane mchana hadi kumi na mbili jioni ya siku hiyo.
Kongamano hilo lilipata baraka zote na Jeshi la Polisi
Mkoani Morogoro, ambalo lilitoa masharti
kadhaa ya kuzingatiwa na wazungumzaji ikiwa ni kutokashifu dini nyingine wala
viongozi wa serikali.
Sakata la kutaka kutiwa mbaroni kwa Shekhe
Ponda lilikuja baada ya yeye kudaiwa kukiuka masharti ya Mahakama aliyopewa
baada ya kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja nje wa kutakiwa asitende kosa lolote la jinai
anapotumikia adhabu hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadalizi ya Kongamano
hilo, Ustaadhi
Idd Msema, alidai kuwa Shekhe Ponda baada ya kutoka ndani ya gari eneo la
Uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege aliofika mita chache katika
barabara ya Tumbaku alitelemka na wakat akitaka kuingia garini ilifayuliwa
risasi iliyompiga begani.
Ustaadh Msema alidai kuwa baada ya kupigwa
risasi begani waumini waliokuwa wameambatana naye walimchukua na kumpakiza
kwenye Piki Piki hadi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ili kupoatiwa
matibabu.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, baada ya kufika
hospitali, waliona anacheleweshwa kpatiwa matibabu na ndipo walipoamua
kumwondoa na kumpekea kwenye Hospitali binafsi ambayo hakupenda kuitaja.
Akizungumzia kwa kina hali ya Shekhe
Ponda baada ya kujeruhiwa huko, alisema kuwa yu hai licha ya kuumia vibaya
begani na kwamba wanatarajia kumpekela eneo jingine hususani Jijini Dar es
Salaam kupata matibabu zaidi.
Alisema viongozi wa Umoja huo hauwezi
kuweka wazi sehemu anakotibiwa kwa kuwa jambo hilo ni la kiusalama zaidi hasa wakati huu
ambapo kumekuwa na sinto fahamu.
Baadhi ya walinzi wa Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Morogoro waliozungumza juu ya tukio hilo , walikiri kuwa Shekhe Ponda aliletwa
hapo kwa usafiri wa Piki piki zikiambatana na nyingine zaidi ya 50 na kuishia
getini.
Walisema walimwingiza adi mapokezi na kwamba
walipoona umati mkubwa upo getini waliamua kutoa taarifa Polisi kuwa wamevamiwa
na watu ambapo muda si mrefu Polisi wa FFU waliwasili na gari lao Hospitalini
hapo.
Hata hivyo walinzi hao walisema, baada ya
kuona Askari wamefika Hospitalini hapo, baadhi ya wafuasi wa Shekhe Ponda
waliamua kumyanyua na kumbeba mabegani na kutoka naye mlango mwingine
wakimlazimisha mlinzi kuwafungulia mlango na baadaye wakatokomea naye kwa
usafiri wa Pikipiki kusikojulikana.
Kufikishwa kwa Sheshe Ponda katika
Hosipitali ya Rufaa kulithibishiwa pia na Mwenyekiti huyo ambaye alidai kuwa waliamua kumwondoa baada ya
kuchekewa kupatiwa huduma.
Baada ya tukio hilo, uvumi ulisambaa meneo mbalimbali nchini
ukidai kuwa Shekhe Ponda amepigwa risasi na Polisi na kufariki dunia. Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Feustine Shilongine akizungumza na Mwandishi wa
Habari hizi majira ya saa tatu usiku wa Augosti 10, baada ya kutokea kwa tukio
hilo, alisema kuwa hapakuwa na taarifa juu ya kutokea kifo cha Shekhe Ponda.
“ Nimepingiwa simu zaidi ya 50 , zikiulizia
jambo hili...kuwa Ponda amefariki dunia ...Binafasi nami ninazisikia , ujumbe
umesambazwa kwenye simu za watu mbalimbali...tumezunguka kila mahali hakuna
kifo wala maiti yake ...na vijana wangu wanaendelea kulifuatilia suala hili”
alisema Kamanda huyo.
Juhudi za kufuatilia sakata la uvumi
kifo cha Shekhe Ponda uliendelea kufanyiwa kazi na Ripota a wetu huyu na usiku
wa saaa tano Mwenyekiti wa Kamati huyo aliweka wazi kwa kusema kuwa Shekhe
Ponda yu hai isipokuwa ameumia vibaya sehemu ya bega .
“ Nipo katika eneo ambalo Shekhe Ponda
anapatiwa matibabu...sehemu ambayo hatuwezi kupataja kiusalama , isipo kuwa
ameumia vibaya kwenye bega lake. Lakini yu hai wala hajafa” alisema Msema.
Polisi Mkoani hapa bado haijatoa taarifa rasmi kuhusiana na sakata hilo, nasi twaendelea
kufuatulia kwa ukaribu.
PICHA MBALIMBALI ZILIZOPIGWA WAKATI WA TUKIO HILO HIZI HAPA
Source: http://mwanaharakatimzalendo.blogspot.com
No comments:
Post a Comment