Friday, August 9, 2013

KATIKA SAFARI YANGU YA TUNDURU NILIKUTANA NA SHIDA YA MAJI KATIKA BAADHI YA VIJIJI.

 Hii ni Picha ya milima katika bonde la magemani lililopo Kijiji Cha Azimio kata Ya Mtina Wilayani Tunduru. Umbali wa Kutokea makao makuu ya Wilaya hadi hapo ni Maili 10. Huko chini ndiko yanakopatikana maji ya kunywa katika kijiji hicho.
 Hii ni Njia ndefu kulelekea yanakopatikana Maji. Maji hapa kijijini yanapatikana Umbali wa kilomita 2.5 kutoka mahali kijiji kilipo.
 Zile chini sio nyumba za Kuishi binadamu bali ni mashimo ya maji yanayotumiwa na Wananchi wa Kijiji Hicho cha Azimio
                                           Huu ni mwonekano wa Mbali yanakopatikana maji
 hii ni hali halisi yanakopatikana maji. Foleni za kuzidi. Hapa Neti zimegeuzwa na kuweza kusaidia kufunika visima vya maji ili takataka na Wadudu wasinywe maji na kuchafua nyakati za usiku
                                         Weusi wa jengo la miti ndilo shimo la maji yenyewe
                           Hili ni Shimo Halisi Na juu ni Ndoo ya Kutekea maji. na maji hapa ni foleni

 Foleni ya ndoo za maji zikisubili kupata maji katika bonde hili ili kukidhi haja ya majumbani




                        Baadhi ya Wakazi wa kijiji hicho waliokutwa wakifua karibu na mashimo ya Maji

 Huyu Ni mwnafunzi Wa shule ya Msingi Azimio akiwa amebeba maji kichwani ndoo mbili za maji
PICHA HIZI ZIMEPIGWA NA Ausi Chiwambo Wiki Nnne zilizopita baada ya kutembelea Huko Tunduru na kujionea Mengi aliyojionea


NA CHIWAMBO AUSI
Katika kijiji Hicho cha Azimio tatizo la maji ni la kihistoria. Kwa miaka mingi sana maji yamekuwa tatizo kupindukia huku hali ya majengo ya shule nayo ni ya kusikitisha. Kwa mara ya kwanza maji ya Visima vya DANIDA vilichimbwa miaka ya 1990-1993, ilifuata TASAF miaka ya 2000.

Asili ya eneo hili lipo juu ya mlima mkubwa na kipo juu ya mlima na aina ya udongo au mchanga unaopatikana hapo ni mwepesi na hufukia visima vya maji au mashimo ya maji. Maji hapa yanauzwa ndogo Sh 300 Tsh. Kule yanakotoka pia yananunuliwa. Idadi ya Mabomba ya kuchimbwa yanayofanya kazi ni machahce sana na hayana uwezo wa kudumu wiki Tatu bila ya kuhalibika. Mabomba au Visima viko vinne vyenye uchakavu wa vifaa.

Serikali ichukuwe tahadhari mapema kabla hali haijawa kubwa zaidi. Umbali kutoka mto mkuwa wa Msinjewe unaomwaga maji Mto Ruvuma kutoka kijiji hicho ni kilomita tatu.

No comments: