Advera Senso- SSP-Msemaji wa Jeshi la Polisi.
--
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA
NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA
DAR ES SALAAM AGOSTI
10, 2013.
1. MNAMO
TAREHE 10, AGOSTI ,2013 MAJIRA YA SAA 8 MCHANA, MAENEO YA SHULE YA MSINGI
KIWANJA CHA NDEGE MANISPAA YA MOROGORO, KULIFANYIKA KONGAMANO LA BARAZA LA
EID LILILOANDALIWA NA UMOJA WA WAHADHILI MKOANI MOROGORO. DAKIKA KUMI KABLA YA
KONGAMANO HILO
KUMALIZIKA ALIFIKA SHEKHE PONDA ISSA PONDA AMBAYE ALIZUNGUMZA KWA
MUDA MFUPI.
2. KONGAMANO HILO
LILIFUNGWA MAJIRA YA SAA 12:05 JIONI AMBAPO WATU WALIANZA
KUTAWANYIKA, BAADHI YAO WAKIWA WAMEZINGIRA GARI DOGO ALILOKUWA AMEPANDA SHEKHE
PONDA. BAADA YA KUTOKA KATIKA ENEO HILO, ASKARI WA JESHI LA POLISI
WALIZUIA GARI HILO KWA MBELE KWA NIA YA KUTAKA KUMKAMATA SHEKHE PONDA AMBAYE
MPAKA SASA ANATUHUMIWA KWA KOSA LA KUTOA MANENO YA UCHOCHEZI SEHEMU
MBALIMBALI HAPA NCHINI YENYE MLENGO WA KUSABABISHA UVUNJIVU WA AMANI.
3. BAAADA YA ASKARI
KUTAKA KUMKAMATA, WAFUASI WAKE WALIZUIA UKAMATAJI HUO KWA
KUWARUSHIA MAWE ASKARI. KUFUATIA PURUKUSHANI HIYO,
ASKARI WALIPIGA RISASI HEWANI KAMA ONYO LA KUWATAWANYA.
4. KATIKA VURUGU HIZO,
WAFUASI HAO WALIFANIKIWA KUMTOROSHA MTUHUMIWA. HIVI SASA
IMETHIBITIKA KUWA SHEKHE PONDA YUKO KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI
AKITIBIWA JERAHA KATIKA BEGA LA MKONO WA KULIA LINALODAIWA ALILIPATA KATIKA
PURUKUSHANI HIZO.
5. KUFUATIA TUKIO
HILO, TIMU INAYOSHIRIKISHA WAJUMBE KUTOKA JUKWAA LA HAKI JINAI IKIONGOZWA NA
KAMISHINA WA JESHI LA POLISI CP ISSAYA MNGULU IMEANZA KUFANYA
UCHUNGUZI WA TUKIO HILO.
No comments:
Post a Comment