Katika mechi ya Yanga iliyopigwa
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Vijana wa Jangwani walitawala mchezo tangu
mwanzo mpaka mwisho, huku Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora Rangers
wakilazimika kukomboa mabao baada ya kutangulia kufungwa mara mbili.
Iliwachukua Yanga dakika 10 tu tangu
kuanza mchezo kufunga bao la kwanza lililowekwa kimiani na Jerryson Tegete
aliyemalizia kwenye kamba pasi nzuri ya Simon Msuva na kumtungua kipa wa
Ashanti, Ibrahim Abdallah.
Hussen Sued kuzuiwa na Tegete kabla
ya kuvuka mstari huku tayari Kipa Ally Mustapha akiwa ameshapitwa na mpira.
Ashanti walikuwa na nafasi nyingine
ya kusawazisha dakika ya 24 kufuatia shuti kali la Sued kumlazimisha Mustapha
kufanya kazi ya ziada kulipangua na kuwa kona.
Dakika tatu baada ya kuanza kipindi
cha pili, Msuva aliipeleka Yanga mbele na kufanya matokeo kuwa 2-0, kabla ya
Tegete kufunga bao la tatu dakika ya 57, na kisha Haruna Niyonzima kufanya
matokeo kuwa 4-0 dakika ya 73.
Ashanti walifunga bao la kufutia
machozi dakika ya 90 kupitia kwa Shaaban Juma, kabla ya Nizar Khalfan kufunga
nao la tano.
Akijitetea na kipigo hicho, Kocha wa
Ashanti Hassan Banyai alisema kikosi chake kinahitaji muda zaidi.
Tabora:
Mjini Tabora, Simba wakishangiliwa na
umati mkubwa, walibanwa vilivyo na wageni wa Ligi Kuu, Rhino Rangers na
kulazimisha sare ya mabao 2-2 kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Katika mechi hiyo iliyochelewa kuanza
kufuatia utata wa vibali vya wachezaji, Joseph Owino, Abel Dhaira na kukosekana
kwa leseni ya Betram Mwombeki, timu zote zilishambuliana kwa zamu.
Iliwachukua Msimbazi dakika 8 tangu
kupulizwa filimbi ya kuanza mchezo kufunga la kwanza kupitia Jonas Mkude
aliyeunganisha kwenye kamba kwakichwa kona maridadi ya Issa ‘Baba Ubaya’
Rashid.
Wenyeji Rangers walisawazisha bao
hilo dakika ya 35 kupitia Iman Noel
aliyepiga mpira wa adhabu ndogo na
kwenda moja kwa moja wavuni, kabla ya dakika moja baadaye Simba kuongeza bao la
pili likifungwa na Mkude kwa kiki ya penalti.
Penalti hiyo ilitokana na kiungo Amri
Kiemba kuchezewa faulo ndani ya eneo la hatari na beki wa Rangers, Daniel
Manyenya, aliyeishia pia kuonyesha kadi ya njano kwa kosa hilo.
Sekunde chache kabla ya mapumziko,
Rangers walifunga bao la kusawazisha, ambalo lilikataliwa na Mwamuzi Amos Paul
kutoka Mara kwa madai kuwa kabla ya bao hilo, kipa wa Simba alifanyiwa
madhambi.
Kipa wa Rangers, Abdul Mtumwa
alifanya kazi kubwa kuokoa mpira wa kichwa kutoka kwa Joseph Owino kufuatia
kona iliyochongwa na Baba Ubaya dakika ya 20.
Kipindi cha pili, Rangers
walibadilika na kufanya mashambulizi makali na kufunga bao la kusawazisha
dakika ya 70 kupitia Stanslaus Mwaktos aliyefunga kwa kiki ya adhabu ndogo
iliyomponyoka kipa wa Simba.
No comments:
Post a Comment