KOCHA wa Manchester United, David
Moyes amepeleka ujumbe kwa Chelsea kwamba Wayne Rooney hatahamia Stamford
Bridge majira haya ya joto kufuatia mchezo wa usiku huu wa miamba hao
uliomalizika kwa sare ya bila kufungana kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Rooney alianza katika kikosi cha
kwanza baada ya tetesi za muda mrefu majira haya ya joto kwamba atajiunga na
Jose Mourinho Magharibi mwa London, lakini alipiga soka ya uhakika leo akiwa na
uzi mwekundu.
Chelsea ilianza bila washambuliaji
wake Fernando Torres na Romelu Lukaku walioanzia benchi, lakini gumzo zaidi ni
kila upande kulalamikia kunyimwa penalti katika mechi hiyo.
Katika mchezo huo wa kwanza wa Ligi
Kuu ya Enlgand baina ya timu hizo, United ilianzisha washambuliaji watatu,
Welebeck, Rooney na Van Persie.
Dakika ya 65 Lampard alishika kabisa
mpira kwenye eneo la hatari kufuatia shuti la Cleverley, lakini refa
'akapeta'.
Dakika ya 71 Ashely Cole alianguka
kwenye eneo la hatari wakati akikabiliana na Jones na akalilia penalti na hata
Mournho akaonekana kulalamika akiwa kwenye benchi.
Mchezo ulikuwa mkali na timu hizo
zilishambuliana kwa zamu na baada ya mechi wachezaji walipongezana kwa mchezo
mzuri.
Jose Mourinho alisema baada ya mechi
mchezo ulikuwa wa haki na hadhani kama kuna iliyomzidi mwenzake uwezo, wakati
Moyes alilalamikia penalti ya Lampard kuunawa mpira na kuwapongeza vijana wake
kwa soka nzuri.
Kikosi cha Man United kilikuwa: De
Gea, Jones, Ferdinand, Vidic, Evra, Valencia/Young dk67, Cleverley, Carrick,
Welbeck/Giggs dk78, Rooney na Van Persie.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill,
Terry, Cole, Ramires, Lampard, De Bruyne/Torres dk60, Oscar, Hazard/Azpilicueta
dk93 na Schurrle.
No comments:
Post a Comment