Uwezekano wa Umoja wa Mataifa
kuidhinisha mashambulizi dhidi ya Syria ni mdogo sana, lakini tayari Marekani
na washirika wake wanafanya maandalizi ya mashambulizi kupitia dhana ya
uwajibikaji wa kimaadili.
Wiki moja baada kutokea shambulio
linalodaiwa kuwa la kemikali nchini Syria, mataifa kadhaa yameanza kupeleka
vikosi kujiandaa na mashambulizi. Siku ya Jumatatu waziri wa mambo ya kigeni wa
Uingereza William Hague alielezea uhakika kwamba gesi ya sumu ilitumiwa na
vikosi vitiifu kwa rais Assad. Uchunguzi wa karibu juu ya shambulio hilo
unaendelea kufanywa na wakaguzi wa Umoja wa Mataifa. Iwapo watabainisha kuwa
kweli gesi hii ilitumiwa na upande wa serikali, hakuna kitakachozuia
mashambulizi ya kijeshi.
Rais wa Marekani Barack anasema
utawala wa Assad laazima uwajibishwe. ***FREI FÜR SOCIAL MEDIA*** Rais wa
Marekani Barack anasema utawala wa Assad laazima uwajibishwe.
Muungano wa hiari
Kulingana na muktadha wa sheria hata
hivyo, mashambulizi hayo yatakuwa yanakiuka sheria za kimataifa, kwa kuwa
uhalali wake unaweza kutokana tu na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa,
ambako China na Urusi zinaweza kuzuia mpango huo kwa kutumia kura zao za
turufu. Kwa nchi hizo mbili, uingiliaji kijeshi kutoka mataifa ya nje siyo njia
ya kuleta suluhu.
Kama litafanyika shambulizi la
kijeshi, haitakuwa mara ya kwanza kwa Marekani kuchukua hatua kama hiyo pasipo
idhini ya Umoja wa Mataifa. Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush, kupitia
kile alichokiita muungano wa hiari, aliyaongoza mataifa kadhaa kuivamia Iraq
mwaka 2003, kwa madai ya kuikomboa kutoka mikononi mwa Saddam Hussein.
Kabla ya uvamizi huo, Marekani ilijaribu
kupitisha hoja yake ndani ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, kuonyesha
kuwa kulikuwepo silaha za maangamizi nchini Iraq, ambapo waziri wa ulinzi wa
wakati huo Collin Powell aliwasilisha ushahidi wa madai hayo katika baraza.
Hata hivyo, kulikuwa na mashaka
makubwa kwa upande wa Ufaransa, Urusi na Ujerumani kuhusiana na ushahidi huo,
na waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Joschker Fischer, alieleza bayana
kuwa hakuridhika na ushahidi wa Marekani. Na kwa hakika mashaka yake yalikuja
kutimia, baada ya kubainika kwamba ushahidi uliyowasilishwa katika umoja wa
mataifa ulikuwa wa kughushi. Collin Powell alikiri kufanya makosa na kujiondoa
katika ulingo wa siasa.
Waziri mkuu wa Uingereza David
Cameron anakutana na maafisa wa juu serikalini na jeshi kujadili mikakati.
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron anakutana na maafisa wa juu serikalini
na jeshi kujadili mikakati.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande
Ulinganisho na Kosovo
Lakini kwa Manfred Eisele, Meja
Jenerali mstaafu wa jeshi la Ujerumani Bundeswehr, mazingira ya uingiliaji kati
nchini Iraq siyo sawa na yaliyopo nchini Syria hivi sasa. Lakini anaona
ulinganifu kati ya Syria na Kosovo mwaka 1999, ambako waasi wa kabila la
Albania walipigana vita vya kujitenga na serikali ya Yugoslavia.
Wakati wa mgogoro huo zilijitokeza
ripoti za mara kwa mara juu ya ukiukaji wa haki za binaadamu na mauaji ya
kimbari yaliyokuwa yakifanywa na jeshi la Yugoslavia. Urusi ilikubali katika
baraza la usalama lakini ilipinga uingiliaji kati wa vikosi vya kimataifa, hali
iliyoilaazimu jumuiya ya kujihami NATO kuingilia kati bila idhini ya Umoja wa
Mataifa.
Andreas Bock, mtaalamu wa siasa
kutoka chuo kikuu cha Augsburg anakubaliana na maoni ya Eisele, na anasema
Kosovo kulikuwepo na ukiukaji wa dhahiri wa haki za binaadamu uliohalalisha
uingiliaji kati. Anasema hata kama hatua hii ilikuwa inakwenda kinyume na
sheria za kimataifa, kulikuwepo na wajibu wa kimaadili kwa jamii ya kimataifa
kusimama pamoja.
Haki dhidi ya maadili
Hata hivyo, uingiliaji wa namna hiyo
kwa misingi ya ubinaadamu bila idhini ya Umoja wa Mataifa ulisitishwa mwaka
1990, pale vikosi vya jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika magharibi
ECOWAS, vilipoingilia kati nchini Liberia vikiongozwa na Nigeria. Eisele
anasema wakati huo dunia haikuwa na maslahi na kilichokuwa kinaendelea nchini
Liberia, kwa sababu mauaji yalikuwa yakitokea barani Afrika. Lakini anasema
hali iliyokuwepo wakati huo ilikuwa inalinganishwa na hali ya Kosovo.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande
alisema hata bila idhidi ya Umoja wa Mataifa laazima Assad achukuliwe hatua.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande alisema hata bila idhidi ya Umoja wa Mataifa
laazima Assad achukuliwe hatua.
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron
Sheria mpya
Ili jamii ya kimataifa iweze
kuingilia kati hali kama hizo bila kuzuiwa na kura za turufu za wanachama
watano wa kudumu wa baraza la usalama, serikali ya Canada ilianzisha dhana ya
sheria ya wajibu wa ulinzi mwaka 2001, na kuendelezwa na kamati ya wataalamu wa
sheria za kimataifa. Kulingana na dhana hiyo, kanuni ya kutoingilia kati
masuala ya ndani ya nchi nyingine inasita kutumika pale unapotokea ukiukaji
mkubwa wa haki za binaadamu. Kwa kuwa hakuna msimamo wa pamoja katika baraza la
usalama, Marekani, Uingereza na Ufaransa zinaweza kutumia dhana hii kuingilia
kati nchini Syria.
Mwandishi: Marcus Lütticke
Tafsiri: Iddi ISmail Ssessanga
Mhariri: Daniel Gakuba
PT
Rais Barack Obama wa Marekani na
waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron wameafikiana kuwa ni dhahiri silaha za
kikemikali zilitumika katika mashambulio ya wiki jana nchini Syria na kwamba
serikali ya rais Bashar Al Assad ndiyo iliyohusika.
Hata hivyo waziri mkuu David Cameron
hajatoa ishara yoyote ikiwa watatumia nguvu za kijeshi kutatua mzozo huo Syria
.
Lakini katika mahojiano na BBC na
vyombo vingine vya habari alisisitiza kuwa hatua yoyote itakayochukuliwa
italenga kujibu matumizi ya silaha za kemikali.
Licha ya kwamba chama cha upinzani
cha Labour kimeonysha ishara kwamba kinaweza kuunga mkono uingiliaji kati wa
jeshi nchini Syria wengi wa wanasiasa bado hawajaamua.
Balozi wa Uingereza katika Umoja wa
Mataifa anatarajiwa kuwasilisha azimio kuhusu Syria wakati wa mkutano wa Baraza
la usalama wa Umoha wa Mataifa
Cameron amesema azimio hilo ni la kulaani
serikali ya rais Bashar Al Assad kwa kutumia silaha za kemikali dhidi ya raia
wake na pia kuidhinisha mikakati maalum ya kulinza raia wa Syria.
Bwana Cameron amesema serikali yake
inataka Umoja wa Mataifa kuwajiabika katika mzozo huo wa Syria.
Tangazo hilo limetolewa baada ya rais
Obama kushauriana kwa njia ya simu na rais Barrack Obama wa Marekani.
Marekani bado haijatoa ripoti yake ya
ujasusi kuhusu shambulio hilo, lakini vyombo vya habari nchini marekani vinadai
kuwa uchunguzi huo ulidukua mawasiliano kati ya maafisa wa wizara ya ulinzi
nchini Syria wakikubali kutekeleza shambulio hilo.
No comments:
Post a Comment