Rais wa Uganda, Yoweri Museveni
amewataka viongozi wawili waandamizi wa upinzani nchini Uganda kuacha mapambao
ya kisiasa wasiyoweza kushinda na badala yake wajiunge na chama tawala cha
National Resistance Movement-NRM.
Bwana Museveni alimshutumu mpinzani
wake Kizza Besigye na meya wa Kampala, Erias Lukwago kwa kupinga program za
maendeleo za serikali na kutangaza uongo. Alitaka aombwe msamaha na wapinzani
hao wawili.
Lakini wote Besigye na Lukwago
walipuuza wito wa Museveni wakiuita mchezo wa kisiasa wa kutaka kupata uungaji
mkono wa chama tawala katika mji mkuu ambako wapiga kura mara nyingi hawakiungi
mkono chama tawala.
Rais Museveni na chama chake tawala
cha NRM wamekuwa madarakani tangu mwaka 1986. Lakini Lukwago anasema matamshi
ya karibuni ya Museveni ni matokeo ya kile anachosema kinaonekana ni mgawanyiko
katika chama tawala.
Lukwago alisema maafisa wa utawala
mara kwa mara wanakataa kufanya kazi na wapinzani kuhusu wasi wasi wa umma
shutuma ambazo wawakilishi wa chama tawala wanazikanusha hazina ukweli.
Wanaushutumu upinzani kwa kuzorotesha juhudi za serikali za kuendeleza sheria
na kanuni na kuhakikisha amani na uthabiti nchini humo. Kitu ambacho Lukwago
hakubaliani nacho.
Chanzo: voaswahili
No comments:
Post a Comment