Mamia ya watu wamefariki katika vituo
vya kuwazuilia washukiwa wa uhalifu Kaskazini Mashariki mwa Nigeria huku jeshi
likijaribu kupambana vikali na kundi la wapiganaji wa kiisilamu Boko Haram
katika eneo hilo.
Shirika la kimataifa la Amnesty
International linasema kuwa vifo vya baadhi ya vimetokana na msongamano kwenye
magereza na wengine kutokana na kukosa chakula na mauaji ya kiholela.
Shirika hilo linaitisha uchunguzi wa
haraka kuhusiana na vifo hivyo.
Serikali, hata hivyo haijatoa kauli
rasmi kuhusu ripoti ya Amnesty.
Lakini jeshi la Nigeria limekanusha
madai hayo na mengine ya awali kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu.
Afisaa mmoja mkuu wa jeshi aliambia
Amnesty kuwa takriban watu 950 walifariki kwenye operesheni ya kijeshi, mapema
mwaka huu.
Wengi walisemekana kuwa uhusiano na
kundi la Boko Haram.
Boko Haram inapigana dhidi ya
serikali ya Nigeria ikitaka kubuni utawala wa kiisilamu na imefanya
mashambulizi kadhaa katika shule za umma.
Takriban wanafunzi 50 waliuawa mapema
mwezi huu wakiwa kwenye mabweni yao katika shambulizi ambalo kundi hilo
lililaumiwa kutekeleza.
Hali ya hatari ilitangazwa katika
majimbo matatu ya Kaskazini mwezi Mei , ikiwemo Yobe, Borno na Adamawa kama
hatua ya kuzuia mashambulizi yanayofanywa na Boko Haharam.
No comments:
Post a Comment