*Ni kuhusu taarifa yake kuhusu ukaguzi wa mahesabu ya vyama vya siasa
*Adai Chadema ndiyo inaongoza kwa hesabu zake kutokaguliwa
*Asema CCM imekuwa ikitii kukaguliwa hata kabla ya vyama vingi nchini
NA MWANDISHI WETU
SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, kutoa taarifa zinazoshutumu kuwa vyama vya siasa nchini havijafanyiwa ukaguzi wa mahesabu kwa muda mrefu, CCM imeibuka na kuitwisha Chadema tuhuma hizo.
SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, kutoa taarifa zinazoshutumu kuwa vyama vya siasa nchini havijafanyiwa ukaguzi wa mahesabu kwa muda mrefu, CCM imeibuka na kuitwisha Chadema tuhuma hizo.
Imesema yenyewe (CCM) imekuwa
ikiitika mwito wa sheria hiyo na kwamba hesabu zake zimekuwa zikikaguliwa kwa
miaka mingi sasa, hata kabla ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi vya siasa hapa
nchini.
Akizungumza na Waandishi wa habari
leo jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye amesema,
ni sahihi kwa hesabu za vyama vya siasa kukagukiwa kwani ni kwa mujibu wa
sheria, na ndiyo sababu CCM imekua ikitekeleza sheria hiyo kwa miaka mingi hata
kabla ya kuanzisha mfumo wa vyama vingi vya siasa.
Nape alisema, badala yake chama
kinachopaswa kutiliwa shaka kuhusu ukiukaji wa sheria hiyo, ni Chadema, chama
ambacho alidai kimekuwa na tabia ya kufanya mambo mengi kinyume cha sheria kwa
kisingizio cha mwavuli wa siasa.
"Chama Cha Mapinduzi kimekuwa
kikiitekeleza sheria hii vizuri. Kwa mfano hesabu za CCM zilikaguliwa na
wakaguzi wa nje TAC (Tanzania Audit Corporation) kuanzia mwaka wa Fedha
1977/1978 hadi mwaka 2002/2003. Kuanzia mwaka 2003/2004 hadi 2010/2011
tulikaguliwa na TAC- Associates, shirika hili linatokana na Tanzania Audit
Corporation lililobinafisishwa", alisema Nape.
Alisema, 29/01/2013 CCM iliandika
barua yenye kumbukumbu CMM/F. 20/80/89 kuwasilisha rasimu ya hesabu za mwaka wa
fedha wa 2011/2012 ili Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) aipangie
mkaguzi.
"Kufuatia barua hiyo, CAG
alitupangia TAC-Associates kukagua hesabu hizo za mwaka 2011/2012.
Kwa kawaida muda wa wakaguzi ni miaka
mitatu hivyo TAC- Associates watakua wakaguzi wetu mpaka mwaka wa fedha wa
2013/2014, baada ya hapo CAG anaweza kuteua wakaguzi wengine", alisema
Nape.
Nape alisema, hesabu za CCM
zilizokaguliwa na wakaguzi wa nje TAC- Associates mwaka wa fedha 2009/2010 na
2010/2011 zilikwishawasilishwa kwa CAG na kwamba hesabu za mwaka wa fedha
2011/2012 bado ziko kwa wakaguzi wa nje, wakishakamilisha nazo zitawasilishwa
kwenye vikao vya Chama na hatimaye kwa CAG.
Alifafanua kwamba, hesabu hizo
zikikaguliwa kwa mujibu wa utaratibu, anapelekewa CAG ambaye ndiye anazipeleka
kwa Msajili wa vyama vya siasa.
Nape alisema kutokana na maelezo haya
CCM haihusiki na agizo la PAC na kama kamati ya bunge ikitaka CCM ipo tayari
kwenda kukutana kamati hiyo, huku CCM ikiwa na mahesabu yake yaliyokaguliwa.
"Mwito wetu kwa Zitto aanze kwa
kutoa boriti kwenye jicho lake ndipo aone kibanzi kwenye jicho la mwenzake.
Tunaamini kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kuwa na vyanzo vya fedha visivyo
visafi na tabia iliyokubuhu ya kupenda kukiuka kila sheria nchini wakidhani
ndio staili ya kujenga chama chao, si ajabu kuwa Chadema wanaweza kuwa
hawajakaguliwa kwa miaka yote hiyo. Zitto kama Naibu Katibu Mkuu wa Chama chake
anapaswa kuwajibika kwa hili, yeye na Chama chake", alisema Nape na
kuongeza;
"Wote tunakumbuka kelele
zilizopo mtaani juu ya matumizi mabaya ya ruzuku zinazoelekezwa na Chadema na
viongozi wake kutoka kwa wanachama wao, hivyo si ajabu wakawa wanakiuka sheria
hii na ndio chanzo cha kelele hizo za wanachama wao".
Nape alitaka ikibainika kuwa ni kweli
Chadema wamekiuka sheria hiyo muhimu, basi viongozi wa vyama husika wawajibike
kwa kuwa si busara kuwa na viongozi wa kisiasa walikubuhu kwa kuvunja sheria za
nchi na kujificha chiniya mwamvuli wa siasa.
"Uvunjaji wa sheria hii kwa
wenzetu sio kwa bahati mbaya kwani wamezoea kutoheshimu sheria za nchi mpaka
kufikia mahali pa kutangaza hadharani kuwa wanatamani nchi isitawalike. Ni
muhimu kujenga utamaduni", alisema Nape.
Chanzo: Mjengwa
No comments:
Post a Comment