Sunday, April 6, 2014

Rwanda yaishtumu Ufaransa kuhusu mauaji

Serikali ya Ufaransa imetangaza kuwa inajiondoa katika maadhimisho ya miaka 20 tangia mauaji ya halaiki nchini Rwanda.
Uamuzi huo unafuatia shtuma kutoka kwa rais wa taifa hilo Paul kagame kwamba Ufaransa ilishiriki katika mauaji hayo ya kimbari mnamo mwaka 1994.

Rais Kagame aliwahi kutoa madai kama hayo hapo awali.
Msemaji wa wizara ya maswala ya kigeni nchini Ufaransa Romain Nadal amesema kuwa matamshi hayo yanaenda kinyume na harakati za maridhiano kati ya mataifa hayo mawili.
Amesema kuwa waziri wa maswala ya haki Christiane Taubira alivunjilia mbali ziara yake ya kushiriki katika maadhimisho hayo mjini Kigali siku ya jumatatu.

Chanzo: BBC

No comments: