Tuesday, April 1, 2014

Kesi dhidi ya rais Kenyatta ni Oktoba

                                                           Rais Uhuru Kenyatta

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC imehairisha kesi dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta hadi tarehe saba Oktoba mwaka huu.

Rais Kenyatta anashtumiwa kwa makosa ya jinai kufuatia machafuko ya baada ya uchaguzi wa mkwaka 2007 - 2008, madai ambayo ameyakanusha.
Mahakama kuu ya ICC, kupitia mwendesha mashtaka Fatou Bensouda, imekuwa ikiitaka serikali ya Kenya kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuendesha kesi zinazowakabili Rais Kenyatta na naibu wake
bwana Ruto.

Hii ni mojawapo za sababu kuu za kubadili tarehe za kusikizwa kwa kesi hii.
Upande wa mashtaka umesema kuwa unaipa Kenya muda wa ziada ili kutafuta na kuwasilisha baadhi ya stakabadhi za benki zinazohitajika katika kesi hiyo.
Kumekuwa na malalamishi kutoka kwa upande wa mashtaka kuwa serikali ya Kenya inalenga kuzuia stakabadhi hizo kufikishwa mahakamani jambo ambala mawakili wa bwana Kenyatta wamekanusha.

Miongoni mwa yale yanayohitajika kotini ni pamoja na taarifa ya maelezo ya fedha anazomiliki bwana Kenyatta.
Kesi hii imekumbwa na matatizo ya mashahidi kujiondoa na shutuma za mahakma hii kuonea viongozi wa bara Afrika.

No comments: