Wednesday, April 9, 2014
RAIS UHURU KENYATTA ATIMIZA MWAKA MMOJA MADARAKANI
Leo unatimia mwaka mmoja tokea Rais
Uhuru Kenyatta aanze kuiongoza Kenya.Katika hotuba yake ya kuingia madaraka
Kenyatta alitoa ahadi nyingi. Jee amezitekeleza kwa kiasi gani. Ni mwaka mmoja,
tokea Rais Kenyatta aapishwe kuanza kulitumikia taifa la Kenya .
Alitoa ahadi nyingi; ikiwa pamoja na
kuuendeleza uchumi, kuuimarisha umoja wa taifa na kuweka utaratibu wa huduma za
afya zinazoweza kulipiwa na kila mwananchi .Rais Kenyatta pia aliahidi kuleta
uhakika wa chakula, kutenga nafasi za ajira kwa vijana na kugawa
"Laptop" kwa watoto wote wa shule za msingi.Lakini aliyoweza
kuyafanya ili kuzitekeleza ahadi hizo ni machache hadi sasa.
Bei za vyakula zimezidi kupanda,
ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana bado ni wa kiwango cha juu na hasa katika
sehemu za mashambani .Aidha mpango wa kugawa "Laptop" kwa watoto wa
shule umesahauliwa ndani ya mtoto wa meza kufuatia kashfa.
Mwandishi habari mmoja Inchikirwa
Ndelejai amesema serikali ya Kenyatta haijafanya mengi. Amesema serika ya
mfungamano wa Jubilee haijafanya ya kutosha. Ameeleza kwamba serikali
haikufanya kama ilivyoahidi.
Mwandishsi habari huyo amesema ,ikiwa
mtu atawapima wanasiasaa katika msingi wa ahadi walizozitoa, basi
kilichofanyika hadi sasa ni cha kusikitisha.
Hatua fulani zapigwa
Hata hivyo hatua kadhaa zimepigwa na
serikali ya Kenyatta katika kuzitekeleza baadhi ya ahadi. Mara tu baada ya
kuchaguliwa Kenyatta alianza kuutekeleza utaratibu wa kutoa huduma kwa ajili ya
wajawazito bila ya malipo.Akina mama hawalipii gharama za kupimwa wanapokuwa
wajawazito na pia hawalipii gharama za kujifungua.Katika hotuba yake Rais
Kenyatta ,alisifu mafanikio yaliyopatikana katika uchumi na hatua
zilizochukuliwa katika kupambana na ufisadi.
Hatua fupi katika kupambana na
ufisadi
Hata hivyo kuhusu ufisadi ndani ya
polisi,mwakilishi wa Wakfu Ujerumani wa " Heinrich Böll" nchini Kenya
Katrin Seidel amesema kwamba maafisa wengi wa polisi waliohusika na vitendo vya
ufisadi vilivyoweza kuthibitishwa bado wanaendelea na kazi na bado wamo katika
ngazi za uongozi pia katika idara ya usalama. Mwakilishi huyo wa Wakfu wa
Ujerumani ,bibi Seidel amesema watu wengi nchini Kenya wanahisi kwamba
hawahudumiwi kwa kiwango cha kutosha katika suala la usalama.
Kutokana na shambulio la magaidi
kwenye jengo la maduka,Westgate mjini Nairobi mwezi Septemba mwaka uliopita
Wakenya wengi wamepoteza imani juu ya idara za usalama. Lakini juu ya suala la
usalama Rais Uhuru Kenyatta amesema " usalama wa watu wetu na ulinzi wa
mipaka ya nchi ni miongomi mwa wajibu wangu mkuu." Rais Kenyatta amesema
vitisho vyovyote dhidi ya mipaka ya Kenya vitakabiliwa kwa uwezo na nguvu zote
za watu wa Kenya.
Umaarufu wa Kenyatta katika utaifa
Katika upande mwingine Rais Kenyatta
anatumia turufu ya utaifa ili kuhakikisha umaarufu wake. Hata kesi inayomkabili
kwenye Mahakama Kuu ya Kimataifa ya ICC inapalilia umaarufu wake.
Rais Kenyatta anakabiliwa mashkata ya
uhalifu dhidi ya binadamu. Katika ghasia zilizotokea nchini Kenya kufuatia
uchaguzi wa Rais mnamo mwaka wa 2007 inadaiwa kuwa Kenyatta ambae wakati huo
alikuwa kiongozi wa chama ndiye aliehamamisha makundi yaliyowatimua watu wa
makabila mengine,yaliyofanya ubakaji na kuwaandama watu wa jamii nyingine.
Mwandishi:Fischer ,Hilke,
Tafisiri:Mtullya Abdu.
Mhariri:Yusuf Saumu
DW.DE
SHANGAZI WA RAIS OBAMA AFARIKI DUNIA.
Shangazi wa rais Obama Zeituni
Onyango ambaye kwa wakati fulani
alinyimwa hifadhi hapa Marekani lakini akaendelea kuishi kinyume cha sheria kwa
miaka kadhaa katika jimbo la Masachussets
amefariki dunia akiwa na umri wa
miaka 61.
Wakili wa masuala ya Uhamiaji wa Onyango amesema amefariki katika hospitali
moja baada ya kuugua ugonjwa saratani na matatizo ya kupumua . Aliugua tangu
mwezi January.
Onyango alihamia Marekani kutoka
Kenya mwaka 2000 na alinyimwa hifadhi ya kisiasa na jaji wa Uhamiaji mwaka
2004. Hakuondoka nchini na aliendelea kuishi kwenye nyumba za umma huko Boston.
Hali yake ya ukaazi wa Marekani
ilitangazwa hadharani siku chache
kabla ya Bw.Obama kuchaguliwa rais Novemba 2008.
Chanzo: VOA
UKRAINE WARNS PRO-RUSSIAN SEPARATISTS
Authorities say they are prepared to
use force to clear buildings occupied by pro-Russian separatists in country's
east. Ukrainian authorities have warned they are prepared to use force to clear
several government buildings seized by pro-Russian separatists in the east of
the country.
Wednesday's warning came as
protesters continued to occupy the headquarters of Ukraine's Security Service
in the eastern city of Luhansk.
Hundreds of supporters camped outside
and shouting "Putin! Putin!" in support of the Russian President, the
Associated Press news agency reported.
Arsen Avakov, the Ukrainian interior
minister, said the standoff in Luhansk and the two neighbouring Russian-leaning
regions of Donetsk and Kharkiv must be resolved within the next two days.
"I want to repeat that there are
two options: political settlement through negotiations and the use of
force," Avakov told reporters. "We are ready for both options."
Avakov was speaking as
anti-government protesters in Luhansk erected high barricades along a
thoroughfare running in front of the security service premises.
The Security Service had earlier said
that the separatists inside the building, armed with explosives and other
weapons, allowed 56 hostages to leave the building during the night. A
spokeswoman said there were no other hostages.
But Tetyana Pohukay, a regional
police spokeswoman, disputed that statement, saying there had never been any hostages
inside, according to the Interfax news agency.
The Luhansk security services
building was among several government offices seized by pro-Moscow groups on
Sunday in an escalation of protests against the interim government in power
since President Viktor Yanukovich was forced to quit in February after months
of protests against his decision to ditch an EU trade pact in favour of closer
ties with Moscow.
Peaceful solution
Serhiy Tyhipko, a lawmaker associated
with the previous Ukraine government, urged the authorities not to storm the
building in Luhansk, calling for a negotiated peaceful solution.
Tyhipko said the protesters were
demanding to turn Ukraine into a federal state with broad regional autonomy,
not to secede.
"The people are not bringing up
the issue of breaking off from Ukraine and are not calling for the help of foreign
countries,'' Tyhipko said on his Facebook page.
Turning Ukraine into a federation is
Russia's key demand and the new government in Kiev has refused to fulfill it,
calling it a precursor to a break-up.
In Donetsk, where protesters were
still occupying the government building, the regional governor was meeting with
key figures in the pro-Russian protest movement to try to find a solution to
the crisis.
"The ultimatum made put the
pressure on people here in Donetsk," Al Jazeera's Kim Vinnell said,
reporting from the eastern region.
She added that negotiations were
under way between both separitists and police in Donetsk and Luhansk.
"Now, with this ultimatum, it
will be a question of what kind of deal can both sides come to. Both protesters
and police are very keen to avoid any bloodshed," she said.
All the cities affected by the
uprisings are in Ukraine's industrial Russian-speaking heartland in the east,
which has a large population of ethnic Russians and where economic and cultural
ties to Russia are strong, according to AP.
Many residents are suspicious of the
government that took power in February.
Overnight, speakers at a gathering in
front of the building condemned the government in Kiev and renewed demands to
be allowed to hold a referendum on declaring autonomy for their region.
That demand is similar to one that
preceded Crimea's annexation by Russia.
Source: Al Jazeera And AP
Hofu yatanda malumbano makali kuibuka kesho
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa,Peter Kuga Mziray.
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Peter Kuga Mziray, ameonyesha
wasiwasi wake kwamba huenda mvutano mkubwa ukazuka bungeni kesho na Ijumaa
wakati kamati 12 za Bunge Maalum la Katiba zitakapowasilisha taarifa bungeni baada
ya kupitia na kuchambua sura mbili za Rasimu ya Katiba, ya kwanza na ya sita.
Sura ya kwanza inazungumzia Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alama na
Sikukuu za Taifa, Lugha za Taifa na lugha za alama na Tunu za Taifa.
Sura ya sita inazungumzia muundo wa
Muungano, vyombo vya utendaji vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mamlaka ya
serikali ya Muungano, mambo ya Muungano, nchi washirika, mamlaka ya nchi
washirika, mahusiano kati ya nchi washirika, mawaziri wakaazi, mamlaka ya
wananchi na wajibu wa kulinda Muungano.
Akizungumza na NIPASHE jana, Mziray
alisema mambo yalikwenda vizuri katika vikao vya kamati, lakini kujadili sura
hizo mbili ndani ya bunge zima mabishano yataanza.
“Hizo sura mbili ndizo zinaleta ugumu,
ndipo kwenyewe,” alisema Mziray ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge hilo na kuongeza:
“Hali bado siyo nyepesi, bado sura hizo ndizo ngumu na ndizo zinaleta mambo.”
Aprili Mosi, mwaka huu kamati 12 za
Bunge hilo zilitawanyika katika maeneo manne kwa ajili ya kuchambua na kujadili
sura ya kwanza na ya sita ambazo ndizo zenye mvutano mkali.
Miongoni mwa mambo ambayo yalizua
utata katika Sura ya Kwanza ni ibara 1(1)
inayosema Tanzania ni nchi na
Shirikisho lenye mamlaka kamili ambalo limetokana Jamhuri ya Watu wa Zanzibar
ambazo kabla ya Hati ya Makubalino ya Muungano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi
huru.
Katika ibara hiyo wajumbe kadhaa
walitaka neno shirikisho ilitoke badala yake iwe Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ni nchi yenye mamlaka kamili.
Hali hiyo ilisababisha baadhi ya
kamati kukosa theluthi mbili ya kura kutoka katika kila upande wa muungano
ambazo zinatakiwa kwa mujibu kanuni 64 (1).
Eneo lingine lililozua mvutano ni
Ibara 1(3) inayosema Hati ya Makubaliano
ya Muungano iliyorejewa katika Ibara ndogo ya kwanza ndiyo msingi mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba hii kwa kadri itakavyorekebishwa,
itakuwa ni muendelezo wa makubaliano hayo.
Kutokana na hali hiyo, wajumbe kadhaa
walitaka ufafanuzi kuhusu Hati ya Muungano na kutaka kuiona.
Hali hiyo ilisababisha kamati Na 2 na
8 kumuita aliyekuwa Katibu wa Bunge wakati wa Muungano, Pius Msekwa, kwenda
kutoa maelezo. Hata hivyo, suala hilo bado halijapata ufumbuzi hususani mahali
ilipo hati hiyo na madai ya utata wa saini.
Katika hatua nyingine, Mziray alisema
kuwa baraza lake liliandaa mkutano wa dharura wa viongozi wa vyama vya siasa kwa ajili ya kupata mwafaka na kuwekana
sawa kufuatia matukio kadhaa ya mivutano katika Bunge Maalumu la Katiba Jumatatu
iliyopita, lakini uliahirishwa kutokana na uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la
Chalinze na Siku ya Kumbukumbu ya Karume.
Alisema siku inayoweza kupangwa ni
Jumapili ambayo ni rahisi kuwapata viongozi wengi kwa kuwa hakuna vikao vya
Bunge.
Naye Katibu wa Baraza hilo, Jaji
Francis Mutungi, aliiambia NIPASHE kuwa wanauandaa tena mkutano huo ili
ufanyike kati ya Aprili 22 na mwisho wa mwezi.
Jaji Mutungi ambaye pia ni Msajili wa
Vyama vya Siasa, alisema watawawaalika watu wengine wakiwamo viongozi wa dini
na kwamba kabla ya mkutano huo, atakutana na baadhi ya makatibu wakuu wa vyama
vya siasa.
CHANZO: NIPASHE
Uganda yatuma ujumbe polisi wake kuvamia Tanzania
Ujumbe wa askari wa Jeshi la Polisi la Uganda
umewasili nchini kwa kile kinachodaiwa kuja kufanya mazungumzo ili kupata
maridhiano kufuatia kitendo cha askari wake wakiwa na bunduki kuvamia eneo la
Mutukula, mkoani Kagera, na kurusha risasi ovyo zilizojeruhi Watanzania wawili.
Habari zilizopatikana jana zinaeleza
kuwa askari hao ujumbe wa askari hao umewasili nchini wakiongozwa na mmoja wa
viongozi wakuu wa Jeshi la Polisi Mbarara, nchini humo.
NIPASHE, ambayo ilifika katika Kituo
Kikuu cha Polisi jana asubuhi iliwashuhudia askari wanne wa Uganda waliovalia
sare, wakiwa nje ya kituo hicho, ambako mwenzao mmoja anashikiliwa kwa tuhuma
hizo.
Hata hivyo, habari nyingine zilieleza
kuwa mbali na kuja kutafuta maridhiano baina yao na wenzao wa Tanzania, ujumbe
huo pia umekuja nchini kwa ajili ya kumchukulia dhamana mwenzao anayeshikiliwa
na polisi wa Tanzania.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, George
Mayunga, alipotakiwa jana kuelezea suala hilo, alisema hadi jana alikuwa
hajapata kibali cha kuzungumzia suala hilo kutoka Makao Makuu ya Polisi, jijini
Dar es Salaam.
Msemaji wa Jeshi hilo nchini, Advera
Senso, jana hakupatikana kuzungumzia kinachoendelea kuhusiana na kadhia hiyo na
hata alipopigiwa simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita bila kupokelewa.
Hata hivyo, juzi alikaririwa akisema
kinachopfanywa na Jeshi la Polisi ni kuchunguza ili kujua sababu za askari hao
kuendesha operesheni hiyo nchini bila kuwaarifu wenzao wa Tanzania kama sera ya
Interpol (Polisi wa Kimataifa) inavyotaka.
Askari saba kutoka Uganda Jumamosi
wiki iliyopita wakiwa na silaha hizo, walivamia eneo hilo kwa kile kilichodaiwa
kuwa walikuwa wakiwatafuta watuhumiwa wa wizi wa pikipiki waliokimbilia
Tanzania.
Chanzo: Nipashe
Necta kuongeza kiwango cha ufaulu sekondari
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Jenista Mhagama.
Baraza la Mitihani la Tanzania
(Necta), limejipanga kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa sekondari
nchini kwa kusambaza vitabu vya tathimini ya uchambuzi wa ufaulu kwa kila
mtihani uliofanywa.
Usambazaji wa vitabu hivyo
utakafanyika kwa shule zote nchini ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa Matokeo
Makubwa sasa (BRN) ili kuwawezesha walimu na wanafunzi kubaini makosa kwenye
mitihani mbalimbali iliyofanywa.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Jenista Mhagama, akizindua vitabu hivyo mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, alisema
vitaonyesha tathimini ya ufaulu kwa kila swali katika kila somo, matakwa ya
maswali na jinsi watahiniwa walivyoyajibu kwa kupata au kukosa.
“Uchambuzi huu utawasaidia
walimu na wanafunzi kubaini makosa
mbalimbali yanayofanywa na watahiniwa wakati wa kujibu maswali na hivyo
kujifunza mbinu bora za kujibu maswali hayo, itasaidia kuboresha kiwango cha
ufaulu cha watahiniwa kwa miaka ijayo,” alisema.
Alisema ni vema vitabu hivyo
vikawekwa kwenye tovuti ili wadau wengi waweze kuvisoma kwa njia ya mtandao na
kupata taarifa sahihi ya tathimini ya ubora wa elimu na hivyo kutekeleza
mikakati mbalimbali ya kuboresha kiwango cha elimu.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Dk.
Charles Msonde, alisema jitihada za pamoja katika kuboresha ufundishaji na
ujifunzaji zinahitajika ili kuongeza ubora wa elimu kwenye masomo yote kwa kuwa
ufaulu kwenye masomo yote uko chini ya asilimia 50.
Alisema chini ya BRN, Wizara
ilijiwekea mikakati tisa ya kutekeleza ambayo ni upangaji wa shule kwa ubora wa
matokeo, utoaji wa tuzo kwa shule zilizofanya vizuri, kuwa na kiongozi cha
usimamizi wa shule, upimaji wa kitaifa wa stadi za kusoma.
Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (Tamisemi) (Elimu), Kassim Majaliwa, alisema vitabu hivyo
vitawasaidia walimu na wanafunzi kubainia mambo yenye changamoto katika
ujifunzaji na ufundishaji na sababu za kuwafanya watahiniwa washindwe kujibu
maswali.
Majaliwa aliwaagiza maafisa elimu wa
mikoa, wilaya na kata kufuatilia matumizi ya vitabu hivyo na kuhakikisha kila
shule inapata nakala kwa kuwa ni nyenzo
muhimu katika kufanya kazi.
CHANZO: NIPASHE
Watu wenye ulemavu watengewe bajeti`
`
Diwani wa Kata ya Ngarenaro, Isaya
Doita, (Chadema), amezitaka halmashauri kutenga bajeti kwa ajili ya watu wenye
ulemavu kupata mahitaji yao badala ya
halmashauri hizo kutenga asilimia 10 kwa ajili ya wanawake na vijana pekee.
Aidha, watoto wenye ulemavu wa
kutosikia, wameiomba jamii kuachana na tabia ya kuwaficha majumbani badala yake
wawapeleke mashuleni kwa ajili ya kupata elimu na kujikomboa kimaisha.
Akizungumza na watoto wenye ulemavu
pamoja na wananchi mbalimbali waliokusanyika kuwasikiliza viwanja vya Soko Kuu jijini Arusha.
Alisema wakati umefika sasa kila kata
kutambua watu wenye ulemavu ili waweze kutengewa bajeti yao na kupata misaada mbalimbali
waweze kuinuka badala ya kuonekana ni mzigo ndani ya familia zao.
Alisema ikiwa halmashauri inatenga
asilimia 10 yaani asilimia 5 inakwenda kwa kinamama na tano inakwenda kwa
vijana huku jamii yenye ulemavu ikiwa haitengewi bajeti .
Naye mwakilishi wa kutetea haki za
watoto pamoja na watoto wenye ulemavu mkoani Arusha, Hafsa Mgaza, aliiomba
jamii kuacha tabia ya kunyanyasa watoto hususan wenye ulemavu kwani kila mtu ni
mlemavu mtarajiwa bali walindwe na kuheshimiwa kama jamii nyingine zenye
mahitaji.
Pia alisisitiza kuwa si jambo jema
kumuona mlemavu akinyanyasika na mwenye viungo akimwangalia.
Aidha, aliiomba serikali pamoja na
taasisi mbalimbali kuhakikisha wanapojenga majengo yanakuwa ni rafiki kwa jamii
hiyo hususan vyooni kwani baadhi yao hupata taabu wanapohitaji kwenda msalani
na maeneo mbalimbali kwa ajili ya mahitaji yao.
Ofisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa
Arusha, Blandina Mkini, alisema serikali itaendelea kushirikiana na jamii hiyo
katika kuhakikisha haki zao zinalindwa na kutoa rai kwa jamii kuacha tabia ya
kuwabaka watu wenye ulemavu.
CHANZO: NIPASHE
Kerry says Russia stirs 'chaos' in Ukraine
President Obama
US secretary of state says Russia
sent "agents" to destabilise Ukraine, as pro-Russians seize offices
in eastern cities. The US secretary of state, John Kerry, has bluntly blamed
Russia of "unmistakable involvement in destabilising" Ukraine by
sending "agents" to its eastern cities.
Kerry on told US Congress on Tuesday
that the Kremlin was seeking to "create chaos" in Donetsk, Kharkiv
and Luhansk as a pretext for more military intervention. "Everything that
we've seen in the last 48 hours, from Russian provocateurs and agents operating
in eastern Ukraine, tells us that they've been sent there determined to create
chaos," Kerry said, adding that he would next week meet his Russian
counterpart, Sergei Lavrov, to discuss the crisis.
Shortly after Kerry's comments,
Ukraine's SBU state security service said pro-Russian activists had placed
explosives in a seized government office in Luhansk, and were holding about 60
people hostage.
"These actions are extremely
dangerous and endanger the lives of people both inside and outside of the
building. They are using terrorist measures," and SBU statement said.
Luhansk pro-Russian protesters
quickly denied the claims.
"There are no explosives, no
hostages. We do not need hostages to get what we want," said Anton, one of
the protesters who described himself as a coordinator of the action.
In recent days pro-Russian activists
seized government buildings in several cities in Ukraine's east, declaring
independence and vowing to vote on splitting from Ukraine.
Ukrainian police cleared protesters
from a regional administration building in Kharkiv in a lightning nighttime
operation on Monday, but others held out in the eastern cities Luhansk and
Donetsk.
Russian efforts
Lavrov and Catherine Ashton, the
European Union foreign policy chief, on Tuesday discussed possible
international efforts to find a solution to the Ukraine crisis, the Russian
foreign ministery said in a statement.
In a telephone conversation initiated
by Ashton, Lavrov reaffirmed Russia's proposal for "an authentic
Ukraine-wide dialogue involving all political forces and regions" aimed at
reaching agreement on constitutional reforms, the statement said.
Russia has long been suggesting
"federalisation" of Ukraine in order to give more autonomy to the
regions of the country, claiming it would make sure ethnic Russian population
were not marginalised by Kiev's central government.
Ukrainian government sees the Russian
plan as an effort to break up the country.
Source: Reuters
Matapeli wajipenyeza TCRA
MAMLAKA ya Mawasiliano imebaini kuwa
uwepo wa mtandao wa matapeli wanaotumia jina la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) kwa kutumia tovuti iitwayo “TCRA Foundation”, inayodanganya kutoa mikopo
kwa maendeleo kwa watu.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo kwa vyombo
vya habari iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Prof. John Nkoma, tovuti
inayotumika ni http://tcra-foundation.wix.com/tcrafoundation.
Alisema mtandao huu umetengenezwa kwa
kutumia picha zilizopo kwenye mitandao mbalimbali zikiwaonyesha Rais Jakaya Kikwete, Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makawe Mbarawa na Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Mawasiliano Prof. John Nkoma.
Aidha mtandao huu unadai kuwa mamlaka
kwa kushirikiana na kampuni za simu za Vodacom na Tigo pamoja na Benki ya CRDB
na NMB zinashirikiana kuendesha foundation hiyo.
“Mamlaka ya Mawasiliano
inawatahadharisha wananchi kuwa haina “Foundation” yoyote ya kutoa misaada ya
fedha. Mtandao huu unatumika kuwalaghai wananchi na kuwaibia fedha zao kwa
kuwataka watume fedha za kujiunga na mtandao huo kwa namba za simu za Tigo na
Vodacom zinazoonyesha kusajiliwa kwa jina la Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania. Sio kweli na ni wizi na udanganyifu,” alisema.
Prof. Nkoma alisema Mamlaka ya
Mawasiliano inawataka wananchi kuwa na tahadhari na watu hawa ambao hutumia
mitandao ya mawasiliano ya simu na intaneti kufanya utapeli kwa kutotuma fedha
wala kujiunga na mitandao ya namna hiyo.
Chanzo: Tanzania Daima
Mnyika ashupalia sheria ya kuzuia bodaboda
MADEREVA wa pikipiki (bodaboda)
jijini Dar es Salaam wamelalamikia kitendo cha Jeshi la Polisi kuwazuia kuingia
ndani ya kivuko cha Kigamboni kwa madai ya kuziondoa pikipiki hizo katikati ya
jiji.
Wakizungumza kwa jazba jana asubuhi
baada ya kuzuiliwa kuingia kwenye pantoni kutoka Kigamboni kwenda Feri, baadhi
ya madereva hao walisema hawajatendewa haki kwa kuwa sio wote wanaofanya
biashara ya kupakiza abiria, wengine wanazitumia kwa usafiri binafsi.
Bakari Musa, mmoja wa madereva hao,
alisema jeshi hilo halikuwapa taarifa ya zuio la wao kuvuka na pikipiki zao
hadi watakapokuwa na kibali maalumu.
Alisema kitendo kilichofanywa leo si
cha kiungwana kwani kimesababisha wengi wao kuchelewa kazini baada ya kufika
Kivukoni na kuzuiwa.
Wakati madereva hao wakilalamikia
usumbufu huo, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, amesema Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Said Meck Sadick ameudanganya umma kwamba Bunge lilitunga sheria ya
kuzuia bodaboda na bajaj kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
“Si kweli kwamba kuna sheria
ilipitishwa Machi 12, 2010 kama ilivyoelezwa na mkuu huyo wa mkoa, badala yake
tarehe hiyo ni siku ambayo aliyekuwa Waziri wa Miundombinu Dk. Shukuru Kawambwa
alitunga kanuni.
“Hata hivyo, kanuni hizo nazo
hazikupiga marufuku bodaboda na bajaj kuingia katikati ya jiji bali zilikasimu
mamlaka kwa halmashauri za Serikali ya Mitaa kuweka utaratibu wa namna vyombo
hivyo vya usafiri vitakavyoingia mjini,” alisema Mnyika.
Alisema kwa kuzingatia maelezo hayo,
alimtaka mkuu wa mkoa asitishe agizo lake na halmashauri za jiji hilo ziweke
utaratibu kwa mujibu wa kanuni na kuzingatia malengo ya kulinda usalama,
kupunguza foleni, kuhakikisha fursa za ajira kwa vijana na usafiri wa gharama
nafuu kwa wananchi.
Kwa mujibu wa Mnyika, sheria ya
Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) haikutungwa mwaka 2010 bali
ilitungwa mwaka 2001 huku akisisitiza kwamba mwaka 2010 zilitungwa kanuni za
Transport Licensing (Motor Cycles and Tricycles) zilizochapwa kwenye gazeti la
serikali namba 144 la Aprili 2 mwaka huo.
Hivi karibuni Jeshi la Polisi,
Sumatra na viongozi wa madereva, waliwataka madereva wa pikipiki kuendelea
kutii amri ya kutoingia mjini kwa pikipiki za miguu miwili (bodaboda) na mitatu
(bajaj).
Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam, Suleiman Kova, alikaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa
operesheni ya kuzuia vyombo hivyo kuingia katikati ya jiji ni endelevu.
“Tutaendelea na operesheni hii, lengo
si kuwakomoa bali ni sheria zipo wazi na lazima zifuatwe,” alisema na kuongeza
kuwa wanazuia pia kutokana na uhalifu wa kutumia pikipiki uliokithiri hasa
maeneo ya katikati ya jiji.
Chanzo: Tanzania Daima
WHO: uvumi wa maambukizi ya Ebola ukome
Shirika la Afya Duniani, WHO,
limesema kuwa kuzuka kwa Homa ya Ebola Magharibi mwa Afrika ni mojawapo ya
changamoto kubwa zaidi ambazo limewahi kukabiliana nayo.
Shirika hilo limesema kuwa
italichukua hadi miezi minne kuthibiti ugonjwa huo. Wakati huohuo shirika la
kutoa misaada ya matibabu ya bure, Medicins Sans Frontieres, limesema kuwa
linaendelea kufanya mashauriano na viongozi wa kijamii katika Wilaya moja
Kusini mwa Guinea, ambalo lilisimamisha shughuli zake baada ya vituo vyake
kadhaa kushambuliwa na wakaazi wa eneo hilo.
Msemaji wa shirika hilo katika mji
mkuu wa Guinea wa Conakry - Sam Taylor - amesema inaeleweka kwamba watu wana
uoga mkubwa.
"Sio taharuki, kimsingi huu ni
uoga. Na tunaelewa hilo. Ni ugonjwa wa kugovya na pia ni mpya nchini Guinea, na
kuna uvumi unaosambaa na pia kuna habari za kuotosha zinazoenea; na
tunachohitaji kuona kwa wingi sasa ni watu kwenda kwa jamii mbalimbali kueleza
ugonjwa huu, jinsi unavyoenea, na jinsi usivyoenea," alisema Bwana Taylor.
Ugonjwa huo umewaua watu 111 katika
nchi za Guinea na Liberia tangu uchipuke mwezi uliopita.
EIGHT PEOPLE KILLED AND 20 INJURED IN PAKISTAN MARKET
Blast rips through Pakistan market
At least eight people killed and 20
injured in a powerful explosion in Rawalpindi near Islamabad. At least eight
people have been killed and 20 injured in a powerful explosion in Rawalpindi
near Islamabad.
The nature of Wednesday's blast in
Rawalpindi's Sabzi Mandi (Vegetable Market) area is yet unknown.
Police and rescue teams are headed to
the location.
The market is known to be crowded in
the mornings. Sources say the casualties may rise.
Source: Al-Jazeera
Mkono aikoromea serikali
Mbunge wa Musoma Vijijini
(CCM),Nimrod Mkono.
Aishangaa kutumia nguvu kubwa kulinda
wanyamapori kuliko binadamu
Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono,
ameishutumu serikali kwa kushindwa kudhibiti mauaji ya kikatili wanayofanyiwa
wanawake katika baadhi ya vijiji vya tarafa ya Nyanja jimboni mwake akisema
imekuwa ikitumia nguvu kubwa kulinda wanyama pori kuliko binadamu.
Mkono alitoa kauli hiyo juzi katika
kijiji cha Mugango baada ya watu wasiojulikana kumnyonga hadi kufa kwa kutumia
upande wa khanga, Anastazia Mang’ombe (42), baada ya kumbaka shambani kwake.
Mauaji ya mwanamke huyo ni mwendelezo
wa mauaji ya kinyama na kikatili yanayotokea katika vijiji vya mwambao wa Ziwa
Victoria vya Nyakatende, Etaro, Nyegina,
Mkirira katika tarafa hiyo yakihusisha wanawake.
Mpaka sasa, hao ni mauaji ya pili
kutokea katika kipindi cha wiki mbili katika jimbo hilo.
Katika tukio la kwanza, mwanamke
mwingine mkazi wa kijiji Kamguruki kata ya Nyakatende wilayani humo, aliuawa
katika mazingira yanayofanana na hayo.
Alisema tangu kuibuka kwa wimbi la mauaji
hayo ya kinyama ambayo hadi sasa yanahusishwa na imani za kishirikina, hakuna
hatua zozote zilizochukuliwa na serikali licha ya viongozi wake kutoa kauli za
kisiasa ambazo zimeshindwa kumaliza mauaji hayo na hivyo kuongeza hofu kubwa
kwa jamii hasa wanawake.
“Jamani, mauaji haya ya wanawake
mwisho wake utakuwa lini, hivi serikali iko wapi, mbona tembo mmoja tu akiuawa
tunasikia filimbi na ndege zinaruka huku na huku kuwasaka wauaji? Iweje leo
binadamu hasa hawa wanawake wanauawa bila hatia hatujasikia serikali imechukua
hatua?
“Akina mama zangu wanauawa,
wanachinjwa kama kuku, sijaiona serikali ikichukua hatua. Sasa ni wakati wa
Waziri Mkuu na Rais wetu waje hapa ili kutusaidia kukomesha mauaji haya ya
kikatili…hivi niwaweke wapi akinamama ambao sasa wanaishi kwa hofu kubwa?,”
Alisema Mkono huku akibubujikwa na machozi.
Kwa sababu hiyo, mbunge huyo alisema
serikali inaonekana kuwapuuza wananchi hao wanauawa kinyama kwani ina vyombo
vya kuwabaini wauaji wote na kuchukuliwa hatua za kisheria.
“Nakwenda bungeni kupigania hili
kwani ni janga la kitaifa. Ikiwezikana serikali itangaze operesheni maalum kama
ilivyofanya katika kupambana na ujangili,” alisema.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati
ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Angelina Mabula, pamoja na kulaani vikali
mauaji hayo, amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili
kuhakikisha wauaji hao wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
“Kwa kweli hali ni mbaya, nawaomba
muwe watulivu kwani matukio haya yametuchanganya. Wiki iliyopita wanawake
wawili wameuawa hivi hivi ukiangalia matukio yote yanafanana na yanafanyika
wazi. Sasa lazima tujiulize wote hapa kuna nini?," Alihoji.
Aliongeza: “Hata tufanyaje polisi
hawawezi kutosha kulinda wote, lazima tuweke mikakati ya pamoja katika
kushughulikia mauaji haya...kwa muda mfupi tu kwa eneo hili la kata nne,
wanawake wanane wameuawa kikatili na mauaji yote yanafanana,” alisema.
Kwa msingi huo, aliwaomba wananchi
kutoa taarifa za kina kwa vyombo vya dola zikiwamo ofisi za viongozi katika
kuhakikisha mauaji hayo yanakomeshwa.
Hata hivyo, litoa agizo kwa wanaume
kuwasindikiza wake zao mashambani na katika shughuli nyingine za kutafuta
kipato wakati vyombo vya dola vikipambana na vitendo hivyo.
Alisema viongozi wa serikali sasa
wameshindwa kuhamasisha shughuli za maendeleo kwani muda wote wamekuwa
wakishughulikia matukio ya mauaji kila uchao.
Kwa mujibu mujibu wa Mkuu huyo wa
Wilaya, hadi sasa watu watano wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji kama
hayo huku wanne wakishikiliwa polisi kwa uchunguzi.
Naye katibu wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) wilaya ya Butiama, Mercy Mollol, aliomba serikali kutangaza eneo hilo
kuwa kanda maalum ya kipolisi ili kuongeza idadi ya askari wa kukabiliana na
mauaji hayo.
“Kama Chama tumesikitishwa sana na
mauaji haya yanayoendelea katika eneo hili. Sasa tunaitaka serikali chini ya
Rais Jakaya Kikwete na IGP Mango, kutangaza operesheni ya watu wanaoua wanawake
kabla hatujatangaza maandamano makubwa ya kupinga ukatili huu,” alisema.
Kamanda wa Polisi mkoani Mara,
Ferdinand Mtui, akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu, alithibitisha kutokea
kwa tukio hilo.
Kamanda Mtui alisema hadi sasa watu
watatu wanashikiliwa polisi kwa mahojiano.
Chanzo: Nipashe
Diwani mbaroni kwa kufunga ofisi za serikali
Watu
watatu akiwamo Diwani wa Kata ya Mwendakulima ya Halmashauri
ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Ntabo Majhabi wanashikiliwa na polisi kwa
tuhuma za kufunga ofisi za serikali za mtendaji wa kata hiyo.
Wanadaiwa kutenda kosa hilo wiki
iliyopita asubuhi baada ya mtendaji wa
kata hiyo, Cecilia Clement kupigiwa simu
na mlinzi wa ofisi hizo, Joseph Katambi na kumpa taarifa za tukio hilo
liliofanywa na wananchi 15 walioambatana na diwani huyo.
Kwa mujibu mtendaji huyo, waliamua
kuibadilisha kamati ya sungusungu ya kata hiyo hali ambayo ilianza kuleta
malalamiko na minong’ono na kwamba huenda ni chanzo cha watuhumiwa hao kufunga
ofisi hizo.
Aliwataja wengine walikamatwa kuwa ni
fundi selemala,Hamisi Abbas na Makaka
Benedictor, wakazi wa kata hiyo.
Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Wilaya ya
Kahama, Benson Mpesya akiongozana na
kamati ya ulinzi ya kata na askari polisi, walifika katika ofisi hiyo kushuhudia mlango huo ulivyofungwa kwa
kuwekewa kipande cha bati na kupigiliwa misumari na mawe.
Mpesya alitoa amri ya kuvunjwa kwa bati hilo chini
ya ulinzi wa polisi na kuamuru waliohusika akiwamo diwani huyo kukamatwa na
kutiwa mbaroni.
Akizungumzia kitendo hicho Mpesya,
alisema ni fedheha na kisichoweza kuvumilika .
Chanzo: Ipp Media
Subscribe to:
Posts (Atom)