Friday, February 22, 2013

UWIANO KATI YA SHULE ZA KATA NA SHULE ZA MIJINI KATIKA KUSHINDANIA DIV. ZERO

                                                   Source: Facebook.com/tz
Huu ni mfano wa Wanafunzi wetu wanaosoma shule zetu za sasa. Hii ni moja ya familia Bora ambayo yenyewe inakuwa ya kwanza kumnunulia mtoto computer. Hivi unategemea nini baada ya kumnunulia. Hapa unatengeneza mtoto huyo kuwa creative and innovative kupitia computer yake hivyo akiingia na kushinda ndani ya facebook ni kawaida. Kwa sasa hali hii imeathiri na kufikia katika elimu ya juu Vyuo vikuu. Wao ndio namba moja kutumia faceook/ twitter huku Lecture akiwa anafundisha. Tunawacheka madogo huku sisi wenyewe wanacyuo hatujijui kama tunatumia. Kwa kiasi kikubwa hizi faceook zinapatikana sana kwa wanafunzi wa mjini ambao sawa na asilimia 20% tu na wale wa shule za vijijini sababu ni hipi?
                                       Picture Source: DWswahil.com 
Shule kama hii wanayokalia Madawati mazuri uwakika wa kufahuru ni mia kwa mia. Kwa saabu mwanafunzi hafikilii kama kesho atapata kiti cha kukalia au la. sasa nchi yetu misitu kule kanda ya kusini, na nyanda za juu kusini ipo kibao ila wanafunzi wanakalia sakafu kufanya viti. unategemea mwanafunzi anayekalia tofali, jiwe, magogo, na sakafu huku usiku akilala uvungu wa kitanda unafikiri huyu mtoto atajengeka kweli kielimu.
                                            Source: Facebook.com/Mohamed Athumani
 Umbali wa shule pia ni tatizo. ijapokuwa tuna shule za kata ila bado zinaonekana ziko mbali. Hapa Mwanafunzi hukatiza Msitu mnene hadi Shule. Je akiwa darasani huyu mtoto si atawaza namna atavyorudi maana kule Kwetu Tunduru wakianza kusumbua Simba inakuwa balaa usipime Ndugu yangu.
 Hii ni picha iliyochukuliwa kwenye shule ya kata na kukutwa online. Source: Facebook.com
                                        Source: www.jamiiforum.com
Je baada ya Madereva Daradara Jijini Dsm kugoma kuwabeba Wanafunzi ndo tuseme kuwa wanafunzi sasa wameamua kutumia magari ya Mchanga. Jana Magazeti yalilipoti kuwa Madereva daradara sasa wagoma kuwabeba wanafunzi kwa kuwa wanapata ziro
                                    Source: Facebook.com
Hiki ni kizazi cha miaka ijayo amao watatulisi sisi. Miongoni mwa hawa ndio wanaosoma shule za kata na kuishia huko huko vijijini na baadaye kuoa baada ya kufeli mitihani yao. Watoto hawa ni wabunifu. Hiyo ni picha ya ajaji Waliyoitengeneza wenyewe na sio kutengenezewa. Kwa nchi nyingine kama zile zilizoendelea Watoto hawa walitakiwa kupelekwa shule za vipaji maalumu ili iwe faida kwa baadaye. Lakini hapa kwetu hali ni tete usipime mtu wangu. kati ya hawa watoto pichani wengine hawatakwenda shule kabisa.

No comments: