Papa anatarajiwa kujiuzulu rasmi mwishoni mwa mwezi Februari
Source: http://www.bbc.co.uk/swahili
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani,
Papa Benedict wa kumi na sita amewashukuru waumini kwa maombi yao kwake katika
hotuba yake ya kwanza hadharani tangu kutangaza kuwa anajiuzulu
Papa alishangiliwa na maelfu ya watu
alipokuwa anajianda kutoa hotuba yake ya kila wiki mjini Vatican.
Alisema anajiuzulu kwa sababu anaelewa
fika kuhusu hali yake ya kiafya inavyoendelea kudhoofika na anavyoishiwa na
nguvu kutekeleza majiku yake.
Baadaye leo ataongoza misa yake ya
mwisho katika kanisa ya St Peter's Basilica.
Tangazo la kujizulu alilitoa mwishoni
mwa Februari,
Papa mwenye umri wa miaka 85, na ambaye
jina lake kamili ni Kadinali Joseph Ratzinger ataendelea na majuku yake kama
kawaida hadi siku atakapojiuzulu rasmi.
Katika muda wa wiki sita zijazo, Papa
mpya anatarajiwa kuteuliwa.
Akiwa na umri wa miaka 78, kadinali
Joseph Ratzinger, alikuwa mmoja wa Papa wazee zaidi kuwahi kuteuliwa kuongoza
kanisa
Alichukua wadhifa wake wakati ambapo
kanisa lilikuwa linakumbwa na kashfa nyingi ikiwemo visa vya kuwaharibu watoto
vilivyofanywa na makasisi wa kanisa hilo.
No comments:
Post a Comment