Friday, February 1, 2013

AJALI YAUA WATANO YAJERUHI 130 MBARALI MBEYA NI VIBARUA WA KAMPUNGA

 
WATU watano wamepoteza maisha na wengine 130 wamejuruhiwa vibaya  huku hali zao zikiwa mbaya baada ya Lori walilokuwa wakisafiria shambani kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha  Mapogolo kata ya Itamboleo  Wilayani Mbarali Mkoani hapa.
Ajali hiyo imetokea leo saa 1:30 asubuhi ambapo lori hilo  ambalo ni mali ya Mwekezaji wa shamba la Kapunga Rice Project, na kwamba watu hao walikuwa wakielekea kwenye shamba la mwekezaji huyo lililkuwa limebeba vibarua hao zaidi ya 200 ambao ni wakazi kitongoji cha  Kapunga.
 Lori hilo lenye namba za uasjili T398 BSE Scania Tipa, ambalo lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyejulikana kwa jina  Baraka Moreli, lilionekana likiwa katika mwendo kasi na   dereva huyo akiwa na lengo la kutaka kuipita pikipiki  iliyokuwa mbele yake. huku akishangiliwa na vibarua hao ipite ipite hiyo pikipiki haiwezi kutushinda sisi gari kubwa moja ya majeruhi alisema. ndipo walipofika kwenye kona dereva lilimshinda gari hilo na kupinduka
Akiwa Hospitalini hapo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro ambaye aliweza kufika hospitalini hapo alisema kuwa mara baada ya kupata taarifa ya ajali hiyo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya ,Mbarali Gullam Hussein Kiffuu, huku akiombwa kupatiwa msaada wa kuongezewa madaktari, kuongezewa vifaa vya mataibu sambamba na uwezekano wa kupata damu kwa ajili ya kuwaongezea majeruhi hao alifanikiwa kuwasiliana na uongozi wa hospitali ya Rufaa ya Mbeya, hospitali ya Mkoa ili kuweza kuona namna ya kwenda kuokoa maisha watanzania hao.
Kandoro, alisema kuwa  katika ajali hiyo wanaume wanne wamefariki na mwanamke mmoja. watatu wametambuliwa
Samweli Mapugilo mbena 30 mkazi wa Ilembula
Bon Mfupa 27 mkazi wa mapogolo na Edgar Mwakipesile 35 mkazi wa Nonde Mbeya
   Aidha, Kandoro alisema kuwa idadi ya majeruhi katika  ajali hiyo kuwa ni 130 ambapo wanawake ni 40 na wanaume 89 huku idadi ya watoto waliokuwa wameongozana na wazazi wao haikuweza kufahamika kwa haraka.
Pcha Mbeya yetu na Kamanga
Source: http://francisgodwin.blogspot.com

No comments: