Mabango ya uchaguzi
mkuu uliofanyika mwaka 2008
Mkuu wa tume ya uchaguzi nchini
Zimbabwe amejiuzulu kwa sababu za kiafya
Hatua ya Bwana Simpson Mutambanengwe,
inakuja huku Zimbabwe ikijiandaa kwa kura ya maoni kuhusu katiba mpya pamoja na
uchaguzi utakaofanyika baadaye mwaka huu.
Waziri mkuu Morgan Tsvangirai, amekuwa
akishinikiza kufanyika mageuzi katika tume ya uchaguzi ili kuhakikisha kuwepo
uchaguzi huru na wa haki.
Uchaguzi huo utakuwa ishara ya
kumalizika kwa utawala wa serikali ya Muungano iliyoundwa baada ya ushindi wa
Rais Robert Mugabe katika uchaguzi uliofanyika 2008 na uliokumbwa na ghasia na
vurugu.
Bwana Tsvangirai, kiongozi wa chama cha
MDC alisusia duru ya pili ya uchaguzi mwaka huo baada ya kudai kuwa alipokonywa
ushindi wake katika duru ya kwanza.
Tsvangirai pamoja na Mugabe
wanatarajiwa kugombea urais katika uchaguzi huo.
Chama cha Rais, Mugabe, Zanu-PF, pia
kilidaawa kufanya ghasia dhidi ya wafuasi wa upinzani, madai aliyoyakanusha.
Waziri wa sheria, Chinamasa, alisema
kuwa Mugabe alikubali kujiuzulu kwa Bwana Mutambanengwe, ambaye ni jaji
mstaafu, aliyechukua wadhifa huo baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata mwaka
2008.
"sababu za kiafya ndizo
zimempelekea kujiuzulu,'' alisema Chinamasa
Mrithi wa Mutambanengwe, atateuliwa
baada ya majadiliano kati ya viongozi wa serikali ya Muungano.
Mwezi jana shirika la kutetea haki za
binadamu, Human Rights Watch, liliitisha mageuzi katika tume ya uchaguzi ,
idara ya mahakama na vyombo vya habari likidai kuwa zinaunga mkono chama cha
Zanu PF
No comments:
Post a Comment