MAKALA YA
CHIWAMBO
Kwa wale
waliofuatilia Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wiki iliyopita na mwanzoni
mwa wiki hii anaweza kuthibitisha kuwa Bunge letu limepoteza mwelekeo na
kugeuzwa kuwa kijiwe cha wahuni. Pia unaweza kufananisha na shule za kata
ambazo hufanya kazi ya kukuza watoto wanaomaliza darasa la saba.
Wabunge kutoka
nje ya kikao cha Bunge ilikuwa kama fasheni ya
vyama vya upinzani hasa Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo (CHADEMA) pale
walipoona hoja zao hazisikilizwi. Kwa safari hii waliamua kutumia njia zote
mbili yaani kutoka nje ya Bunge siku ya Jumatatu na siku ya Jumanne kutumia
njia mbadala ambayo wanadhani kuwa ni njia mzuri kuliko zote ni kuzomea zomea
bila utaratibu ambapo Muheshimiwa Tundu Lisu, John Mnyika, Na Nasari ndio
wanaosemekana kuwa ni chokochoko la zomea zomea kule mjengoni.
Kwa wale
niliosoma nao Chuo Kikuu kimoja hasa wale wanaosoma Shahada ya Sosholojia na
Maendeleo ya jamii nimewai kuwaeleza kwamba “Hata motto mdogo ukimnyanyasa na
kumonea kila ukutanapo, basi ujue kuwa siku moja atakugeukia na kukurudishia
matusi au kukurusha mawe kama silaha yake
dhidi ya uonevu, 2012”.
Hili ndilo
linalotokea ndani ya Bunge letu. Hoja za wapinzani kwa miaka mingi hasa Bunge
la Kumi limekuwa hodari kwa kuweka kapuni Hoja z wabunge wa upinzani na matokeo
ya haya ni vurugu kubwa zilizotokea wiki hii. Ni hatari sana
kuona Bunge linafanywa kama sehemu ya
kuendeleza ubabe wa kisiasa na si kujadili hoja zenye maslahi kwa Watanzania.
Katika historia
ya Mabunge Duniani ni kwamba vurugu Bungeni ni sehemu ya kawaida kwa baadhi ya
nchi na linaonekana ni jambo la kawaida ila kwa upande wan chi yetu ni jambo
geni licha ya wabunge wa Tanzania
kutaka kuzichapa Mwaka 2011. Wiki hii waliona bora kumzomea Naibu Spika, Job
Ndugai.
Kutokana na mahojiano
yaliyofanywa na mwandishi wa Gazeti la Raia Mwema na Mbunge wa Iringa Mjini
Mchungaji P. Msigwa alisema kwamba “ipo siku watavunja viti vya Bunge……” na
mwishowe alimalizia kwa kusema hatua zichukuliwe ili wasifike huko.
Kuna jambo
linanishangaza sana hasa kwa Wabunge wetu na
jambo hilo
ndilo linalofanya Bunge letu lipoteze mwelekeo. Jambo kuu ni lile la Mbunge
kupinga uozo wa wizara husika kwa kuongelea zaidi madudu yaliyomo katika Wizara
husika na wakati wa kuhitimisha hoja yake anamalizia kwa kuunga mkono hoja
iliyopo.
Huu ni undumila
kuwili ambao unalifanya Bunge letu kupoteza Mwelekeo. Kuna Rafiki yangu mmoja
siku moja aliniambia kwa sasa kuangalia Bunge ni sawa na kusoma gazeti la udaku.
Nilimuuliza kwanini? Hakuweza kunipa jibu. Kwa hakika kauli yake ina uhalisia
katika Bunge letu.
Watanzania
wenzangu, wasomaji wa makala ya Chiwambo, ni maoni yangu kwamba Bunge hili
linaloongozwa kivyama zaidi ifike siku liongozwe na mtu asiye mwanachama wa
chama chochote hapa nchini ili lilete ufanisi zaidi kuliko tunayoyashuhudia
huko Dodoma
kila unapofanyika Mkutano wa Bunge.
No comments:
Post a Comment