Friday, February 22, 2013

VIONGOZI MALIMBALI WANENA KUHUSU ANGUKO LA ELIMU TANZANIA KUPITIA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE, 2012

Vigogo watema cheche

WAKATI Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiinyooshea kidole Serikali kwa kuzitelekeza shule za sekondari za kata, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa amesema hatajiuzulu ng’o kutokana na matokeo mabaya ya kidato cha nne.

Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), nalo limetishia kuitisha maandamano ya nchi nzima kwa kushirikisha wanafunzi wote waliopata sifuri ikiwa waziri huyo hatajiuzulu.

Taifa limeshikwa na mshtuko kutokana na matokeo hayo ambayo yanaonyesha kuwa asilimia 60 ya wanafunzi waliofanya mtihani huo mwaka jana, walipata sifuri.

Dk Kawambwa
Akizungumza jana katika uzinduzi wa Mpango Maalumu wa Mafunzo ya Kompyuta katika Shule ya Msingi ya Majengo wilayani Bagamoyo, Dk Kawambwa alisema hawezi kuachia ngazi kwa shinikizo la wanasiasa.

Alisema yeye si wa kulaumiwa kutokana na wanafunzi hao kufanya vibaya kwenye mtihani wa kidato cha nne na kwamba wanaosema waziri anapaswa kujiuzulu hawana hoja za msingi zaidi ya kutaka kujipatia umaarufu kwa kudandia hoja zinazokuwapo kwa wakati husika.

“Unajua katika mfumo wa vyama vingi, kila linapotokea jambo baya basi wanaona dawa ni kiongozi mhusika kung’oka. Unapozungumza waziri kujiuzulu hiyo ni lugha ya kisiasa lakini hata akijiuzulu inakuwa bado tatizo halijaweza kupatiwa ufumbuzi,” alisema.

Dk Kawambwa alisema hata Serikali haijafurahishwa na matokeo hayo mabaya na kushauri njia nzuri ni kutafuta dawa ya kukabiliana na tatizo la wanafunzi kufeli huku akiahidi kuwa wizara yake inaangalia tatizo hilo kwa karibu zaidi ili kujua chanzo chake.

Alisema amesikitika kuona hata shule ambazo zilikuwa zinategemewa kufanya vizuri zikiwamo za seminari, watu binafsi na kongwe za Serikali, nazo zimefanya vibaya.
Aliunga mkono maoni ya kutaka mfumo mzima wa elimu nchini uangaliwe upya kwa kushirikisha wadau mbalimbali wa elimu.

Lowassa
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Lowassa alisema matokeo hayo ni aibu kwa taifa na kuilaumu Serikali kwa kuzitelekeza shule za sekondari za kata.
Alisema taifa kwa sasa linazalisha wabeba kuni na maji na siyo wasomi ambao wanaweza kushindana kwenye soko la ajira.

Alisema sekondari za kata ambazo zilianzishwa chini ya usimamizi wake akiwa Waziri Mkuu, zilikuwa ukombozi kwa Watanzania wengi wa kipato cha kawaida na ndiyo sababu waliitikia wito kwa kuchangia ujenzi, hatua ambayo alisema ilimpa faraja kubwa.

“Serikali tuliahidi kuzikamilisha shule hizo kwa kuzijengea maabara na kuhakikisha zina walimu. Ni wajibu wake kutimiza. Mimi ndiyo maana hata kwenye Katiba Mpya nilipendekeza uwezekano wa elimu ya sekondari kuwa bure, elimu ni kama mapigo ya moyo ya taifa ukiona hayaendi vyema lazima ujiulize,” alisema.

Lowassa, ambaye alijiuzulu uwaziri mkuu mwaka 2008, alisema tangu aondoke madarakani, shule hizo nazo zimetelekezwa.

Alimwomba Rais Jakaya Kikwete kuchukua hatua za makusudi, ikiwa ni pamoja na kuunda tume ili ichunguze kwa makini kiini cha matokeo hayo mabaya.

“Matokeo hayo ni aibu kwa taifa, walimu, wazazi na wanafunzi wenyewe. Namwomba kwa dhati Rais afanye kitu cha ziada, natambua mchango wa juhudi zake katika sekta nyingine ikiwamo ujenzi wa barabara nchini lakini elimu ndiyo iwe ya kwanza,” alisema.

Alitaka ufike wakati nchi iamue kuwekeza katika elimu tofauti na ilivyo sasa kwa Tanzania kuwa nchi inayotenga fedha kidogo zaidi katika sekta hiyo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Alisema Tanzania inatumia asilimia 1.4 ya bajeti yake, Kenya asilimia saba, Rwanda 5.8%, Uganda 4.8% na Burundi ni 3.2%.

Bavicha na maandamano
Bavicha imetishia kuitisha maandamano hayo yatakayowahusisha wanafunzi wote waliofeli ikiwa Waziri Kawambwa hatajiuzulu ndani ya siku 14 kama Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alivyomtaka Jumanne wiki hii.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Bavicha, Deogratius Munishi alisema wameshaanza kuwajulisha viongozi wa mikoa na wilaya kuhusu taratibu zote za kuandaa maandamano hayo.

Alisema kuwa lengo la maandamano hayo ni kutaka kushinikiza pia Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Shule za Sekondari wa Wizara ya Elimu kujiuzulu ili kupisha wengine watakaosimamia kikamilifu mabadiliko ya mfumo wa elimu nchini.

“Tunaitaka pia Serikali ya CCM ieleze hatima ya maisha ya vijana waliofelishwa na mfumo mbovu wa elimu,” alisema na kuongeza kuwa kuna wanafunzi 800,000 waliofeli ambao wako mitaani tangu tatizo la matokeo ya kidato cha nne lilipoanza mwaka 2009.
Alisema Serikali ya CCM ilikuwa na lengo la ufaulu wa asilimia 70 kwa kidato cha nne tangu mwaka 2009 lakini imekuwa kinyume chake.

“Ukweli usiofichika ni kuwa Serikali ya CCM haiwezi kufikia lengo la kuwa na taifa lililoelimika ifikapo 2025 kama ilivyobainisha kwenye dira yake ‘Vision 2025’ na badala yake itajenga taifa la watu mbumbumbu kwa wakati huo,” alisema.

Imeandikwa na Julieth Ngarabali, Bagamoyo, Beatrice Moses na Nuzulack Dausen, Dar.
Source: www.mwananchi.co.tz
 

UWIANO KATI YA SHULE ZA KATA NA SHULE ZA MIJINI KATIKA KUSHINDANIA DIV. ZERO

                                                   Source: Facebook.com/tz
Huu ni mfano wa Wanafunzi wetu wanaosoma shule zetu za sasa. Hii ni moja ya familia Bora ambayo yenyewe inakuwa ya kwanza kumnunulia mtoto computer. Hivi unategemea nini baada ya kumnunulia. Hapa unatengeneza mtoto huyo kuwa creative and innovative kupitia computer yake hivyo akiingia na kushinda ndani ya facebook ni kawaida. Kwa sasa hali hii imeathiri na kufikia katika elimu ya juu Vyuo vikuu. Wao ndio namba moja kutumia faceook/ twitter huku Lecture akiwa anafundisha. Tunawacheka madogo huku sisi wenyewe wanacyuo hatujijui kama tunatumia. Kwa kiasi kikubwa hizi faceook zinapatikana sana kwa wanafunzi wa mjini ambao sawa na asilimia 20% tu na wale wa shule za vijijini sababu ni hipi?
                                       Picture Source: DWswahil.com 
Shule kama hii wanayokalia Madawati mazuri uwakika wa kufahuru ni mia kwa mia. Kwa saabu mwanafunzi hafikilii kama kesho atapata kiti cha kukalia au la. sasa nchi yetu misitu kule kanda ya kusini, na nyanda za juu kusini ipo kibao ila wanafunzi wanakalia sakafu kufanya viti. unategemea mwanafunzi anayekalia tofali, jiwe, magogo, na sakafu huku usiku akilala uvungu wa kitanda unafikiri huyu mtoto atajengeka kweli kielimu.
                                            Source: Facebook.com/Mohamed Athumani
 Umbali wa shule pia ni tatizo. ijapokuwa tuna shule za kata ila bado zinaonekana ziko mbali. Hapa Mwanafunzi hukatiza Msitu mnene hadi Shule. Je akiwa darasani huyu mtoto si atawaza namna atavyorudi maana kule Kwetu Tunduru wakianza kusumbua Simba inakuwa balaa usipime Ndugu yangu.
 Hii ni picha iliyochukuliwa kwenye shule ya kata na kukutwa online. Source: Facebook.com
                                        Source: www.jamiiforum.com
Je baada ya Madereva Daradara Jijini Dsm kugoma kuwabeba Wanafunzi ndo tuseme kuwa wanafunzi sasa wameamua kutumia magari ya Mchanga. Jana Magazeti yalilipoti kuwa Madereva daradara sasa wagoma kuwabeba wanafunzi kwa kuwa wanapata ziro
                                    Source: Facebook.com
Hiki ni kizazi cha miaka ijayo amao watatulisi sisi. Miongoni mwa hawa ndio wanaosoma shule za kata na kuishia huko huko vijijini na baadaye kuoa baada ya kufeli mitihani yao. Watoto hawa ni wabunifu. Hiyo ni picha ya ajaji Waliyoitengeneza wenyewe na sio kutengenezewa. Kwa nchi nyingine kama zile zilizoendelea Watoto hawa walitakiwa kupelekwa shule za vipaji maalumu ili iwe faida kwa baadaye. Lakini hapa kwetu hali ni tete usipime mtu wangu. kati ya hawa watoto pichani wengine hawatakwenda shule kabisa.

NAMNA BARABARA YA MWAI KIBAKI ILIVYOFUNGULIWA PAMOJA NA PICHA ZAKE @Chiwambo's Blog






Barabara ya Old Bagamoyo sasa yapewa jina la Mwai Kibaki Road
Source: kajunason.blogspot.com

Saturday, February 16, 2013

IMAGENE IMEMUONA WEWE UKIWA KAMA MWALIMU MKUU UNGEFANYAJE

source: facebook

PICHA ZA ASKARI ZIKIONYESHA NAMNA WALIVYOSAMBARATISHA MAANDAMANO YA WAFUASI WA SHEKHE PONDA





MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI 16-02-2013







PICHA MBALIMBALI ZINAZOONESHA NAMNA POLISI WALICYOZIMA MAANDAMANO YA WAISLAMU JANA JIJINI DAR ES SALAAM








(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWEBLOG)

JIJINI MBEYA JANA USIKU ILITOKEA AJALI MBAYA YA KUGONGANA MAGARI USO KWA USO

 Kisa cha ajali ni Dereva Mwenye Gari Nyekundu kulewa kupita kiasi. Hata Baada ya kutokea ajali hiyo Dereva wa Gari nyekundu alikuwa ajitambui kwa sababu alikuwa amekunywa pombe kupitiliza.
 MAGARI YALIYOGONGANA USO KWA USO NI HAYA (Hapa ni Baada ya Kusogezwa Barabarani. Gali la Mbele lilisukumiwa kwenye Mtaro wa Maji Lakini picha za Asubuhi hii kama zinavyoonekana ni baada ya Kuondolewa kwenye Mtaro. Picha na Chiwambo

Dereva wa hili gari ndiye Msababishaji wa Ajali. Baada ya Matengenezo alikuwa analijaribu kama limepona baada ya kulewa

 PICHA ZA HAPA JUU NI AJALI ILIYOTOKEA JANA. AJALI MBAYA YA ILIYOHUSISHA KUGONGANA MAGARI USIKU HUU YATOKEA JIJINI MBEYA MAENEO YA BLOCK "T" NYUMA YA TEKU UNIVERSITY. CHANZO CHA AJALI NI DEREVA WA GARI LENYE USAJILI NO. T940 AAG KULEWA KUPITA KIASI AMBAPO ALILIGONGA GALI NO. T228 ALC. HADI TUNARUSHA MTAMBONI GARI ASKARI WA USALAMA BARABARANI WALIKUWA WAMEWASIRI.



Picha hizi Tatu za Chini ni ajali nyingine iliyotokea Mwishoni mwa wiki iliyopita  karibu na eneo la ajali ya jana Maeneo ya Block "T" TEKU university.