Friday, August 9, 2013

TINDIKALI TANZANIA KWA SASA NI JANGA LA KITAIFA


Na Chiwambo Ausi,


Zengwe la kumwagia Tindikali watu wa aina Mbalimbali Tanzania sasa limekuwa janga la kitaifa na ni wimbo wa Taifa kwa sasa. Huko nyuma tulitumia kwa shughuli za Kimaabara na mahospitalini lakini leo matumizi ya tindikali yamegeuzwa na kuwa silaha ya kuwaalibu watu sura zao, kuua kwa kutumia tindikali au kumwagia tindikali. Kwa sasa tindikali Tanzania imegeuzwa kuwa silaha dhidi ya watu fulani.

Katika miaka ya hivi karibuni Tanzania tumeshudia namna watu wa aina Mbalimbali walivyomwagiwa Tindikali pasipo kukamatwa mtu yeyote yule. Kwa mfano, hivi majuzi Wazungu wawili kutoka Wiingereza wamemwagiwa tindikali na watu wasiofahamika. Pia katika chaguzi mbalimbali nchini ikiwemo ule wa Igunga ulitawaliwa na mada ya Tindikali.

Pia Waandishi wawili wa Gazeti la Kila wiki la Mwanahalisi (Lililofungiwa na serikali) akiwemo Saed Kubenea na mwenzake mmoja walimwagiwa Tindikali wakiwa ofisini. Watanzania Tujiulize, kwanini haya yanatokea? Kwanini wahalifu hao hawakamatwi? Je huu ni uzembe wa nani? Serikali haina budi kutafuta chanzo cha tatizo na kuzuia moja kwa moja.

Kwa miaka michache iliyopita Tindikali ilikuwa ni suala la kitaifa tu, ila kwa sasa wamevuka mipaka na kuwamwagia Tindikali hadi Wageni waliofika Tanzania kutoka nchi nyingine. Watanzania tulaani Vikali sana sulala hili kwani ni aibu ya kitaifa.
Mwandishi wa RFI Kiswahili Ndugu Emmanuel Richard Makundi alilipoti taarifa ifuatayo; Raia hao wawili wasichana wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 wanaaminika kuwa walikuwa wakifanya kazi za kujitolea visiwani humo na kwamba tukio hili ni la kwanza kufanywa kwa raia wa Kigeni.

Kaimu kamanda wa Polisi Visiwani Zanzibar, Mkadam Khamis amewaambia waandishi wa habari visiwani humo kuwa watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki waliwakaribia wasichana hao na kisha kuwamwagia tindi kali.
Wizara ya mambo ya nje ya Tanzania imekiri kuwa na taarifa hizo na kwamba wanafanya kila linalowezekana kuhakikisha raia hao wanapatiwa matibabu ya haraka kuwanusuru na madhara zaidi ya acid hiyo.

Polisi wanasema bado wanaendelea na uchunguzi na kwamba mpaka sasa watu waliohusika na shambulio hilo hawajafahamika ila uchunguzi bado unaendelea na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano kubaini wahusika.
Wizara ya mambo ya nje imesema kuwa zaidi ya raia elfu 75 wa Uingereza ambao huetembeala Tanzania kila mwaka, hivi karibuni kumekuwa na mashambulizi yakuwalenga raia wakigeni jambo ambalo linahatarisha usalama wao.

Wizara hiyo imeongeza kuwa kumekuwa na matukio ya uporaji wa mizigo ya raia wa kigeni hasa kwenye baadhi ya mitaa ya jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine hali ambayo hivi sasa inaonekana kuota mizizi.

Hivi Karibuni watu wasiofahamika walimwagia tindi kali mufti msaidizi wa Zanzibar pamoja na kumpiga risasi padri wa kanisa Katoliki.”
Ni matumaini yangu kuwa serikali itasikiliza kilio hiki na kuchukua hatua stahiki ili lisije kujirudia na uwe wimbo uliopita na muda “The Song of the past”.

No comments: